mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Yametukia matukio mbalimbali fedheha na udhalilishaji wa kijinsia yenye kuwahusisha viongozi wa kidini wa kanisa Katoliki la Roma. Matukio haya ya aibu kubwa na ya kashfa za kingono yanawahusu vijana na watoto wenye umri wa chini ya miaka 18, wote wa kike na wa kiume yakiambatana na vitendo vya ubakaji ambayo yalianza kuibuliwa toka miaka ya 1950.
Baada ya kuwepo kwa ukimya wa muda mrefu kutoka kwa viongozi wa juu wa kanisa hili kubwa ulimwenguni kote, bado kuliendelea kuwepo kwa malalamiko na mashauri mengi ya kijinai yaliyokwisha kufunguliwa na familia za wahanga. Pamoja na hayo yote kutokea, bado mamlaka ya juu wa kanisa hili ulichokwisha kukijifanya ni kuomba tu msamaha wa jumla kwa wahanga pasipo hata kutaka kuwawajibisha wahusika ama kuonyesha nia ya kuwalipa fidia wahanga.
Leo imetolewa ripoti nchini Ufaransa kuhusu wahanga wapatao 330, 000 ambao waliathirika, ambao wanalihusisha dhehebu hili kubwa la Kikristo na lenye maarufu ulimwenguni kote.
Je! Mamlaka ya Vatikano inaguswa kwa dhati na kashfa hii ama itaweza kuja na kauli gani yenye kushawishi na kuweka mambo sawa?
Je! Hii kashfa kwa nini isiwe sababu ya kutengua kanuni za useja ili mapadri nao waruhusiwe kuoa ili kuepuka tamaa za kingono?