BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani imelalamikiwa kutompatia matibabu ya upasuaji wa henia ‘ngiri’ Bathromeo Mapunda, kisha kumfukuza hospitalini hapo kwa kukosa Sh250,000.
Awali, Batholomeo (46) aliambiwa atoe Sh450,000 na baada ya kuhangaika sana na kushindwa kufikisha kiasi hicho cha fedha, alipewa masharti ya kutoa Sh250,000 ndipo afanyiwe upasuaji.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi jana yaliyofanyika nyumbani kwake Jet Lumo wilayani Temeke, jijini hapa, Batholomeo, ambaye kwa sasa anapambana na maumivu makali, alisema aliondolewa hospitali hapo Jumatatu ya Agosti 15, mwaka huu.
“Namkumbuka yule daktari (anamtaja jina) ndiye aliyekuwa akizungumza na ndugu zangu wanatakiwa kutoa hizo fedha, nililala pale hospitalini usiku mmoja na asubuhi aliniambia niondoke nikatafute fedha, licha ya awali kuweka bondi simu yangu na kiasi cha Sh50,000,” alisema.
Akisimulia mkasa wake, Batholomeo alisema amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2019 na kwa kipindi chote amekuwa akitumia dawa za mitishamba.
Alisema dawa hizo amekuwa akizitumia pale anapoona anaumwa na ngiri na inapopoa huendelea na shughuli zake kama kawaida.
“Jumapili ndiyo nikaumwa sana, ndugu zangu wakanichukua na kunipeleka hospitali Kisarawe kwa kuwa inasifika kufanya upasuaji huo, walinipokea na kunipa huduma ya kwanza, ikiwemo kutundikiwa maji na mpira wa mkojo wakati huo nilikuwa nimepoteza fahamu, ndugu zangu walikuja kunihadithia baadaye,” alisema.
Batholomeo alisema hajaridhishwa na huduma ya hospitali hiyo. “Hata mjomba wangu, Mathias Madidi alifariki katika hospitali hii mwaka 2020 baada ya kucheleweshewa huduma, licha ya dawa zake za matibabu kununuliwa kwa wakati.
“Imebidi tuseme hii hali kwa maana kama familia imetukuta hii ni mara ya pili, watu wangapi wanapitia changamoto hii? Ni wengi sana. Hii ni changamoto, wafanye uchunguzi katika hospitali zetu za Serikali hali siyo nzuri,” alisema.
Ndugu wa Batholomeo, Maria Madidi aliyekuwa akimuuguza hospitalini hapo alisema baada ya mvutano mkubwa daktari huyo alishusha gharama mpaka Sh250,000, huku suala la dawa ya usingizi wakiambiwa ni lazima wanunue. “Nilimpigia simu mke wake nikamwagiza akanunua dawa ya usingizi na aje nayo ili mgonjwa afanyiwe upasuaji, kwani alikuwa katika maumivu makali. Lakini alizunguuka Gongolamboto na maeneo mengine jirani bila kupata dawa hiyo, aliporudi tukauliza tena hospitalini hapo tukaambiwa dawa hiyo ipo ila tutoe Sh 10,000,” alisema.
Alisema wakihangaikia matibabu ya ndugu yao walikwenda hadi kitengo cha ustawi wa jamii ndani ya hospitali hiyo, hata hivyo walielezwa kuwa wanatakiwa kuchangia gharama kwa punguzo la hadi Sh200,000, hata hivyo haikupatikana kwa haraka.
“Familia tulikuwa bado tunachangishana fedha na baadaye zilitimia Sh80,000 na tulivyowaambia hivyo, tulishangaa asubuhi daktari anamwandikia arudi nyumbani mpaka atakapopata fedha zote Sh250,000, mgonjwa amerudi nyumbani Lumo anaendelea kupata maumivu makali na hajaandikiwa dawa yoyote,” alisema Maria.
Mke wa Batholomeo, Nashra Manzi alionyesha dawa ambayo ilisitisha upasuaji wa mumewe kwa ndugu kuagizwa wakaitafute ambapo mpaka Agosti 14 saa 2 usiku, dawa hiyo haikuwa imepatikana, hali iliyosababisha mumewe asipelekwe chumba cha upasuaji.
Akilizungumzia hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kisarawe, Dk Yonah Kabatta alimtaka mgonjwa huyo kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kuendelea kupata matibabu aliyokuwa amekwishayaanza.
Alisema changamoto za aina hiyo zinapojitokeza wagonjwa wanashauriwa kufika katika uongozi wa hospitali kabla ya kuchukua jukumu la kuondoka.
“Angekuja moja kwa moja kwangu. Changamoto kama hizi zinaweza kutokea na kama kiongozi siwezi kujua kila kinachoendelea wanakopatiwa huduma.
“Mgonjwa wa dharura aliyekosa fedha akija kwanza anapokea matibabu ndipo suala la malipo lifuate kulingana na miongozo iliyopo, arudi hospitali. Kazi tuliyoapa kuifanya ni kutibu watu na kama wasiwasi wake ni kuhusu daktari aliyekuwa akimpa huduma tutamtafutia mwingine apokee matibabu,” alisema Kabatta.
MWANANCHI