PMNBuko
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 967
- 154
Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali ya JK imelazimika kuweka Mtihani wa aina yake kwa Sekondari zote za serikali kwa wanafunzi wa Kidato cha I kama Qualifying Test baada ya kutokuamini matokeo ya wanafunzi hao. Hii ni kashfa kubwa kwa maana mbili.
Moja, wanafunzi hao wamefanya Mtihani wa Taifa- kwa kutumia fedha za umma; wakasahihishwa mtihani huo - kwa kutumia fedha za umma; matokeo yakatangazwa - kwa kutumia fedha za umma; Selection ikafanyika - kwa kutumia fedha za umma; wanafunzi na wazazi wakajiandaa kujiunga na sekondari, vifaa vikanunuliwa, madawati na karo vikalipwa kwa kutumia gharama kubwa. Leo hii, shule zote za sekondari zimeagizwa kufanyisha QT kwa watoto hao na wale wataoshindwa mtihani huo, watarudishwa majumbani. Hapo hasara inarudi tena kwa upande wa mtoto na wazazi. Huu ni uharibifu wa rasilimali fedha na muda.
Pili, ni kashfa kwa sababu, sekondari za yeboyebo (kata) zimesababisha hali hii maana, sasa kila mtoto aliyefika darasa la saba anaamini kuwa atajiunga na sekondari bila kujali amefaulu au la. Kipimo cha kupima uwezo halisi wa mtoto hakipo kama ilivyokuwa zamani na mitihani ya darasa la saba imerahishwa ili shule za kata zisipate aibu ya kukosa watoto. Kurahisishwa kwa mtihani kunafanywa kwa makusudi na serikali ili kupima indicator ya number of enrollment na siyo quality ya elimu inayopatikana. Hii ni aibu kwa serikali.
Wadau, hii Serikali ya zima moto inatupeleka wapi? Naomba kuwasilisha!!