Kashfa nyingine kwa Serikali ya JK: Wanafunzi Kidato cha I kufanya Qualifying Test

Kashfa nyingine kwa Serikali ya JK: Wanafunzi Kidato cha I kufanya Qualifying Test

PMNBuko

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
967
Reaction score
154
Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali ya JK imelazimika kuweka Mtihani wa aina yake kwa Sekondari zote za serikali kwa wanafunzi wa Kidato cha I kama Qualifying Test baada ya kutokuamini matokeo ya wanafunzi hao. Hii ni kashfa kubwa kwa maana mbili.

Moja, wanafunzi hao wamefanya Mtihani wa Taifa- kwa kutumia fedha za umma; wakasahihishwa mtihani huo - kwa kutumia fedha za umma; matokeo yakatangazwa - kwa kutumia fedha za umma; Selection ikafanyika - kwa kutumia fedha za umma; wanafunzi na wazazi wakajiandaa kujiunga na sekondari, vifaa vikanunuliwa, madawati na karo vikalipwa kwa kutumia gharama kubwa. Leo hii, shule zote za sekondari zimeagizwa kufanyisha QT kwa watoto hao na wale wataoshindwa mtihani huo, watarudishwa majumbani. Hapo hasara inarudi tena kwa upande wa mtoto na wazazi. Huu ni uharibifu wa rasilimali fedha na muda.

Pili, ni kashfa kwa sababu, sekondari za yeboyebo (kata) zimesababisha hali hii maana, sasa kila mtoto aliyefika darasa la saba anaamini kuwa atajiunga na sekondari bila kujali amefaulu au la. Kipimo cha kupima uwezo halisi wa mtoto hakipo kama ilivyokuwa zamani na mitihani ya darasa la saba imerahishwa ili shule za kata zisipate aibu ya kukosa watoto. Kurahisishwa kwa mtihani kunafanywa kwa makusudi na serikali ili kupima indicator ya number of enrollment na siyo quality ya elimu inayopatikana. Hii ni aibu kwa serikali.

Wadau, hii Serikali ya zima moto inatupeleka wapi? Naomba kuwasilisha!!
 
Sasa watakaofaulu kwa kiwango cha maksi 100 - 250 ndio hao watakao ruhusiwa kuendelea na elimu ya sekondari. Lakini inashangaza pia maana kiwango hicho hicho (na hata zaidi) ndicho kilitumika na Baraza kuchagua watoto hao.
 
Watakaofeli, wanawarudisha nyumbani. Tayari Mbeya wamerudishwa nyumbani baadhi ya watoto, na wazazi wameandika hasara kwa vitu walivyokwisha -vinunua. Huu ni utapeli wa juu wa serikali, na mpango huu umefanywa kimya kimya. kila mkoa una tarehe yake ya kufanya mtihani huo. Mkoa wa Mwanza walimaliza last week huko mkoa wa Kagera wameanza mtihani jumatatu hii.
 
Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali ya JK imelazimika kuweka Mtihani wa aina yake kwa Sekondari zote za serikali kwa wanafunzi wa Kidato cha I kama Qualifying Test baada ya kutokuamini matokeo ya wanafunzi hao. Hii ni kashfa kubwa kwa maana mbili. Moja, wanafunzi hao wamefanya Mtihani wa Taifa- kwa kutumia fedha za umma; wakasahihishwa mtihani huo - kwa kutumia fedha za umma; matokeo yakatangazwa - kwa kutumia fedha za umma; Selection ikafanyika - kwa kutumia fedha za umma; wanafunzi na wazazi wakajiandaa kujiunga na sekondari, vifaa vikanunuliwa, madawati na karo vikalipwa kwa kutumia gharama kubwa. Leo hii, shule zote za sekondari zimeagizwa kufanyisha QT kwa watoto hao na wale wataoshindwa mtihani huo, watarudishwa majumbani. Hapo hasara inarudi tena kwa upande wa mtoto na wazazi. Huu ni uharibifu wa rasilimali fedha na muda.

Pili, ni kashfa kwa sababu, sekondari za yeboyebo (kata) zimesababisha hali hii maana, sasa kila mtoto aliyefika darasa la saba anaamini kuwa atajiunga na sekondari bila kujali amefaulu au la. Kipimo cha kupima uwezo halisi wa mtoto hakipo kama ilivyokuwa zamani na mitihani ya darasa la saba imerahishwa ili shule za kata zisipate aibu ya kukosa watoto. Kurahisishwa kwa mtihani kunafanywa kwa makusudi na serikali ili kupima indicator ya number of enrollment na siyo quality ya elimu inayopatikana. Hii ni aibu kwa serikali.

Wadau, hii Serikali ya zima moto inatupeleka wapi? Naomba kuwasilisha!!

Sioni kama ni tatizo kwa sababu nadhani nia ni nzuri tu ya kuwajengea wanafunzi hao morari ya kujisomea
 
Watakaofeli watafanjwaje?

Nadhani Serikali mpaka ifikie uamuzi huo inajua hakutakuwa na adhari kwa pande zote. Hili halihitaji siasa kwa sababu serikali ina wataalamu wake ambao kwa namna moja au nyingine watakuwa wameshirikishwa.
 
Watakuwa ma hausigeli na mahausi boi, tena wakipata kazi chadema wameukata!
Tusiingize siasa katika hili badala yake tuipongeze serikali kwa uwajibikaji wake wa karibu katika suala zima la elimu kuhakikisha elimu itolewayo nchini inakuwa bora.
 
Kuna tatizo gani hapo, hizo ndizo juhudi za Serikali kupunguza wale walioiba mtihani, unapaswa kuipongeza Serikali kwa hilo. Aidha, ni onyo kwa wale wenye tabia ya wizi wa mitihani katika miaka ijayo maana sasa watasoma kwa bidii. Tusipende kupinga kila kitu hata kile chenye manufaa.
 
big up serikali hasa wizara ya elimu.....! nawapa pole mabingwa wa kuogopa mitihani na wataalamu wa kichakachua, mnaona jinsi serikali ilivyojipanga sasa mnatafuta pa kutokea mitandaoni
 
Tuwapongeze kitu gani? kwa nini tusijiulize imekuwaje mtoto anamaliza darasa la saba hajui kusoma wala kuandika huo umakini wa serikali upo wapi? hadi kunakuwa na udanganyifu? haiwezekani mwalimu afundishe zaidi wa watoto 100 darasani huku wakitimua vumbi darasani wengine chini ya miti ndo wanaposomea ukategemea watajua wote kusoma na kuandika huku walimu wanalilia maslahi yao huu ubabaishaji hadi lini wananchi tunatakiwa kuiuliza serikali kwa nini hivi ?na sio kuipongeza yani tupongeze kwa kuwarudisha watoto nyumbani miaka saba hawajui kusoma na kuandika ni aibu kwa serikali na wazazi wao yani hadi kufikia hatua hii mzazi hajui maendeleo ya mwanaye hebu watanzania tuwe makini tuache kupigiana makofi kusiko stahili.changamoto kwa serikali mgomo wa walimu hauna kikomo
 
  • Thanks
Reactions: EMT
big up serikali hasa wizara ya elimu.....! nawapa pole mabingwa wa kuogopa mitihani na wataalamu wa kichakachua, mnaona jinsi serikali ilivyojipanga sasa mnatafuta pa kutokea mitandaoni

nadhani wangekuwa wamejipanha isingefikia hatua mbaya kama hii.tafakari
 
big up serikali hasa wizara ya elimu.....! nawapa pole mabingwa wa kuogopa mitihani na wataalamu wa kichakachua, mnaona jinsi serikali ilivyojipanga sasa mnatafuta pa kutokea mitandaoni

kujipanga gani huku nadhani wangekua wamejipanga yasingetokea haya yote tafakari
 
Kuna tatizo gani hapo, hizo ndizo juhudi za Serikali kupunguza wale walioiba mtihani, unapaswa kuipongeza Serikali kwa hilo. Aidha, ni onyo kwa wale wenye tabia ya wizi wa mitihani katika miaka ijayo maana sasa watasoma kwa bidii. Tusipende kupinga kila kitu hata kile chenye manufaa.

hii ni sawawa na kumpigia makofi nyani akiwa shambani anakula mahindi
 
Umefika wakati sasa tuachane na huo mfumo wa elimu wa kikoloni wa kuchuja wanafunzi ili kupata wachache unaowataka. Tuifanye elimu ya sekondali kuwa ya lazima kwa kila mtoto na itolewe bure na serikali. Kuishia darasa la Saba kumepitwa na wakati, hakuna ajira, na hata ujasiliamali wa std 7 nao ni shida. Tutoe elimu kwa lengo la kuelmisha watoto, siyo kwa lengo la kuchagua wachache ili wafanye kazi serikalini baadae.
 
big up serikali hasa wizara ya elimu.....! nawapa pole mabingwa wa kuogopa mitihani na wataalamu wa kichakachua, mnaona jinsi serikali ilivyojipanga sasa mnatafuta pa kutokea mitandaoni

Kuna tatizo gani hapo, hizo ndizo juhudi za Serikali kupunguza wale walioiba mtihani, unapaswa kuipongeza Serikali kwa hilo. Aidha, ni onyo kwa wale wenye tabia ya wizi wa mitihani katika miaka ijayo maana sasa watasoma kwa bidii. Tusipende kupinga kila kitu hata kile chenye manufaa.

Wakuu kuna tatizo hapo. Yaani ni sawa na kuzima moto bila kuangalia chanzo cha moto wenyewe. Lazima utakuwakia tena tuu. Tunafukia kwa juu juu tuu bila kuangalia kiini cha kuibiwa kwa mitihani. Kama watu wameweza kuiba mitihani ya taifa watashindwa kuiba pia hizo qualifying tests?

Hapa serikali imetafuta temporary solution, lakini hizo qualifying test nazo zitabiwa tena kwa sana tuu. Then what would be the next move for the government? Serikali iache kukwepa kutatua tatizo la kuibiwa kwa mitihani kwa kutafuta cover up solution.
 
Mimi sioni tatizo hapa. Mwaka 1969 nilichaguliwa kuingia kidato cha kwanza na tulifanya mtihani mmoja wa Kiingereza. Sikuelewa mantiki yake mpaka tulipopungua darasani. Kwa kweli elimu yetu imekuwa tata. Policy zinabadilika kila baada ya masaa.
 
Back
Top Bottom