Mimi hii naiita ni sinema. Kila kitu kilipangwa na na kuchezwa kwa ajili ya audience ambao ni watanzania. Walijua fika itajagundulika so wanaamua wao kuiongoza waonekane as if ndio wameibua ufisadi.
Kama movie inavyokua they know where this will end ilhali wameshachota fedha zetu. Kama movie za kihindi zilivyo 'stelingi' hauwawi, atashinda tu. Director wa hii movie aliepanga mchezo huu ni system nzima, maana watu wawili au watatu hawawezi cheza movie.
Nashurutika kuamini hata CAG huwa anaparticipate tangu mwanzo wa kuandika hii sinema, what is unfolding now is part of the ongoing script. Kina Ruta hao ni waigizaji tu wanaoonekana kwenye screen. Movie hii haina tofauti yoyote na ile ya Richmond, EPA, IPTL, na Meremeta, nk. Mwisho wake bahati nzuri twaweza kuhisi itakuwaje.
Nia za hizi movie ni kupumbaza tuone wanaibua vitu na kuvifanyia kazi lakini hakuna kitu. Nina hakika kuna scripts nyingi tu zinaendelea kuandikwa na kueditiwa, fraud and more fraud, wakati wao wa screening utafika tu na the same yatatokea.