mchukiaufisadi
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 546
- 193
Ndio maana tuna idara za "Customs", "health", "TFDA", "TBS", "UWT" na zinginezo, kuhakikisha hatuingiziwi vibovu.
Nakuuliza, vitunguu vibovu bandarini vina husiana nini na Igunga?
Author anajaribu kukumbusha tu serikari hivi sasa akili ipo Igunga. Karibu wakuu wa Idara zote macho na akili zao ziko Igunga na kuwaacha wachina na mafisadi uchwara waingize takataka.
Samahani dada yangu FF hivi UWT nao wana nafasi kwenye uingizaji vyakula? ahaaaa ni wanawake wake wa CCM, Igunga vipi UWT hawakwenda? au ndo walioachiwa majukumu ya Bandari?
Soma vizuri post. Asiyejuwa maana haambiwi maana, msitake kutubabaisha kwa maneno. Hata Usalama wa Taifa ni UWT na huko pia kuna wanawake. Igunga UWT wamekwenda au umesahau mlivyomvua hijab mwana mama wa UWT?
Ahsante Nsiande, si i own hiyo label, hiyo label ni ya wateja wangu ambao tunawatengenezea nguo za pamba yenye ubora unaokubalika. Kama hizo nguo ukikuta ni za pamba na zimetengezwa Mauritius, kumbuka ni mimi nnae zisimamia kuanzia kupeleka pamba India ikafumwa mpaka kuifikisha Mauritius na kuhakikisha zinashonwa nguo kutokana na design na ubora autakao mwenye nembo ya "Cotton Club".
Watu wengine wanajaribu kutenganisha yanayotokea kwenye ufisadi na matokeo yake kwa maisha ya wananchi. Kwamba kwa kuagiza au kuruhusu vitunguu saumu tunaua biashara yetu ya ndani sisi wenyewe na kuendelea kuwasukumiza watu kwenye kona ya umaskini wa kudumu.
sasa sie wapenzi wa vitunguu saumu ndio tumekwisha maana hivi lazima vitaingia tu sokoni.... ewe mola tuepushe na haya mabalaa kha!
Huwa sifikiri, jee wewe?
Umekuja na habari nzuri sana para ya kwanza, kama ni ya kweli, halafu para ya mwisho ukamwaga pumba kama kawaida yako. Unanshangaza kwa kuiharibu habari kwa maswali yasiyo na msingi.
Kuagiza biashara za nje hakuuwi biashara ya ndani bali kunasaidia kuikuza. Amma kwa kuweza kuonesha ubora wa bidhaa zetu amma udhaifu wa bidhaa zetu na kuchukua njia mbadala wa amma kuboresha bidhaa zetu amma kuziuza kwa ubora wake unaostahiki, mashindano ya kibiashara ndio njia pekee ya kukuza biashara, uelewa, elimu, viwango na hata "presentation" ya bidhaa. Na ikiwa tutaendelea kuogopa kuleta bidhaa za nje basi tukubali na matokeo ya kuzifunga fikra zetu na ziendelee kuwa pevu kama tunavyofikiri.
Amekula chumvi mwenzio, mwezi wa 8 alisherehekea miaka 30 ya ndoa yake, hapo hata kama aliolewa na ten yrs unadhani sahizi atakuwa na umri gani? Sijui kwa nini hataki kupumzika ale uzee wake kwa raha!..Huyu hakuvuliwa hijab maana haukuwa na hijab. Huyu alivuliwa nguo aka mtandio.
By the way naomba namba yako nikutwangie, siamini kama wewe ni mzee kama wanavyo kusema. Nipe nafasi
Kuna habari za kuaminika sana kuwa kuna kontena la futi 40 (karibu tani 30) na limeingie nchini kwa karibu wiki mbili sasa ambalo limejaa vitunguu saumu ambalo linajaribiwa kuingizwa nchini na kundi la Wachina. Sasa wakaguzi wa pale bandari wakagundua kuwa vitunguu vinaoneshwa (kwenye mifuko yake) kuwa vimeexpire tangu 2009. Sasa jana Wachina wetu walienda TFDA ili kupata kibali cha kuingiza vitunguu hivyo nchini. Lakini ilikuwa vikitoka hapo viende kutiwa moto - chanzo toka bandarini - kinadokeza kuwa hivyo vitunguu vimekomaa kiasi kwamba ukivipasua "unaweza kupata kizunguzungu au kupaliwa".
Sasa Wachina hawako tayari kuingia hasara. Nasikia wametembeza mlungula wa kitu kidogo kuanzia TFDA, Kilimo, TRA na kwa vile sijafuatilia leo tangu hili sakata lianze jana walikuwa waende na TBS. Sasa uwezekano wa vitunguu hivyo kuingizwa sokoni ni mkubwa hasa kama haitawezekana kuvirudisha China. Sasa hivi vimehifadhiwa katika mafriji ya bandari pale na jamaa hawataki ifanyike "manual" inspection wanataka "scanning". Jamaa wametembeza karibu dola 5000 ili kurahisisha utoaji wa vitunguu hivyo; kuanzia TFDA kwenyewe kilimo na TRA.
Sijui ni mazao gani yanalimwa huko Igunga (najaribu kukumbuka kama kuna maeneo ya Tabora wanalima Vitunguu saumu) lakini vyovyote vile ilivyo taifa lnapofikia kuagiza hata vigunguu saumu basi tuna hali mbaya sana. Ndio nimebakia kusema kuwa kuna kashfa nyingine ni za kijinga.
Vitunguu saumu ndivyo hivi vya kupikia pilau na vingine huwa naona ndugu zangu wa Singida wakiweka kwenye wale kuku wao wa kulimia ili wawe laini wakati wanachomwa au ni vingine? Ndivyo hivi ambavyo vinakosa soko kule Karatu na viunga vya jirani au vingine? Ndivyo hivi vinavyouzwa pale katiakoo kwa muuza viungo vya pilau au ni vitunguu saumu vingine? Mwanakijiji huenda kwenye kontena kuna madwa ya kichina na si vitunguu saumu. Siamini fanya utafiti mujarabu utujuze.
Kama kweli tumeagiza vitunguu saumu basi tena nchi yetu si riziki.
Nna uhakika hujawahi kufanya biashara wala huielewi biashara, kuagiza biashara za nje hakuuwi biashara ya ndani bali kunasaidia kuikuza. Amma kwa kuweza kuonesha ubora wa bidhaa zetu amma udhaifu wa bidhaa zetu na kuchukua njia mbadala wa amma kuboresha bidhaa zetu amma kuziuza kwa ubora wake unaostahiki, mashindano ya kibiashara ndio njia pekee ya kukuza biashara, uelewa, elimu, viwango na hata "presentation" ya bidhaa. Na ikiwa tutaendelea kuogopa kuleta bidhaa za nje basi tukubali na matokeo ya kuzifunga fikra zetu na ziendelee kuwa pevu kama tunavyofikiri. Au tukubali kuwa na fikra changa zenye uwezo wa kufikiri mapya kwa kujifunza mapya mengi kutoka kwa wenzetu waliokubali kuwa hakuna fikra pevu utakayoifundisha ikaelewa (try to teach an old dog new tricks). Kuwa na fikra pevu ni ufinyu wa kufikiri.
Leo kweli mtu haswa mwenye fikra za kimaendeleo anakwambia usiagize bidhaa za nje kwani zinauwa biashara yetu ya ndani? Inashangaza sana.
Halafu uhusishe mambo kibao na uagizaji wa vitunguu?
Hivi huwa unatafuta njia za kupakaza kila unapoweza au ndio upevu wa fikra zako umefikia ukomo wa kufikiri?
Watu wengine wanajaribu kutenganisha yanayotokea kwenye ufisadi na matokeo yake kwa maisha ya wananchi. Kwamba kwa kuagiza au kuruhusu vitunguu saumu tunaua biashara yetu ya ndani sisi wenyewe na kuendelea kuwasukumiza watu kwenye kona ya umaskini wa kudumu.
Mie nadhani wako ndio uliolala, Igunga kuna limwa nini inahusiana nini na vitunguu vya bandarini? halafu kuna kosa lipi kuagiza vitunguu saumu kutoka nje? mradi vitengo vya afya viruhusu, sioni uhusiano wa biashara na Igunga na Bandarini. Nadhani mpaka sasa utajuwa ni ubongo wa nani uliokufa. Nakupa pole sana.