Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

..ikulu wakanushe hili haraka, kama walivyokanusha habari ya mshahara wa raisi.

Ikulu wakikanusha itamaanisha kuwa Lowassa ni muongo. Ili kutoa ushahidi zaidi inabidi Lowassa aje na vithibitisho.
 
Ni kweli tuna haki watanzania kulaumu alikuwa wapi kuyasema kama alikuwa akituhurumia watanzania lakini pia tunahaki ya kuhoji kwanini serikali haikuchua hatua ya kumshitaki alipotuhumiwa kama fisadi? Hapo pia akili ya kuambiwa changanya na zako.
 
'nilishauri mkataba huo uvunjwe' Ulishauri kama nani? Jukumu la kushauri serikali juu ya mambo yote ya kisheria ni la mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General)
 

Huu ndio ulikuwa wakati halali wa kujiuzulu kama kweli wewe ujiitakia mazuri nchi hii. Kume ulikuwa hufai, hata urais hutafaa.

Huyu mtu huangalia maslahi hayake zaidi kuliko ya wananchi. Sasa huyu alikuwa waziri mkuu mtendaji au mtendwaji? Maelezo yake hayana mshiko wala hayauziki hata kwa shilingi moja. Viongozi wa bongo ni malaya tu. Maelezo hayana mshiko kabisa.
 

mwaga kwa maana hii chain ndo tuliisubir mda mrefu
 
mgao kala hv uongozi wa juu yy asiwepo kweli?hv jambo aliandae mkuu wa kaya lowasa asijue kweli?hamna kitu hapa
 
alisema lembeli ukitaka kuona nyeti za kuku subiri upepo. sasa nyeti za kuku hizi hapa!
 
Ni kweli tuna haki watanzania kulaumu alikuwa wapi kuyasema kama alikuwa akituhurumia watanzania lakini pia tunahaki ya kuhoji kwanini serikali haikuchua hatua ya kumshitaki alipotuhumiwa kama fisadi? Hapo pia akili ya kuambiwa changanya na zako.

hapo kweli patata
 
Hiki ni kiwango cha juu kabisa cha uchu wa madaraka mm ningemwona wa maana angefanya hivi wakati wa nyerere aone ,ccm imemlea mpaka amekuwa billionea kwann asiwe wazi tu kwamba kinachompeleka ikulu ni kulinda biashara zake na share kubwa alizonazo kwenye makampuni makubwa hapa nchini
 

Aliogopa mamlaka ya juu itambabu sea yeye na familia yake.
 
Kwa hiyo kukaa kwetu gizani kote , kumbe bwana Mkubwa ndo mhusika sio, aiiseee,,,, ndo maana hanaga stress , anacheka tu
 

Acha povu katika masuala ya mikataba mwanasheria Ndo anahusika. Ye alitaka majibu kwa mwanasheria mkuu.
 
Sijasikia jibu lolote zaidi ya kuquote hearsay ya AG na KM ambao anajua fika kuwa hawana forum ya kumjibu au kujitetea.
 
Nahisi harufu ya vita kati ya mamlaka ya juu na mheshimiwa Lowassa. Tunasubiri kama upande wa pili nao utakuwa na la kusema au utapiga kimya kama kawaida yake. Hizi siasa bhana zinafurahisha sana wakati mwingine. Mambo yameanza kuwekwa hadharani.
 
Nani anaweza kununua hii hekaya!

Yaani Waziri Mkuu anatumia maneno ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati yeye ndiye namba tatu katika utawala wa nchi achilia mbali ile dhana ya kusema yeye hakukutana barabarani na Rais Kikwete. kwa maana kwamba, mahusiano yao yalikuwa zaidi ya mahusiano ya kikazi.

Kwa hiyo Mwanasheria Mkuu alivyomwambia, yeye hakuwasiliana na Rais kutaka kufahamu ukweli wake?

Kwa nini hakuliambia bunge hii story baada ya kupewa nafasi ya kutoa ufafanuzi?

Mtu mwenye fikara pana hawezi kununua hekaya hizi.
 
every thing happens for a reason...kukatwa kwake kulikua kwa sababu kabisaaaaaaa,am gonna love this year's compaign,Gods plan is what i call the whole situation
 
Hebu nisaidieni Je nini kitafuata iwapo kesho Nape Moses Nauye NAYE akiamua kuja UKAWA atapokelewaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…