Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

..ikulu wakanushe hili haraka, kama walivyokanusha habari ya mshahara wa raisi.

Ikulu wakikanusha itamaanisha kuwa Lowassa ni muongo. Ili kutoa ushahidi zaidi inabidi Lowassa aje na vithibitisho.
 
Ni kweli tuna haki watanzania kulaumu alikuwa wapi kuyasema kama alikuwa akituhurumia watanzania lakini pia tunahaki ya kuhoji kwanini serikali haikuchua hatua ya kumshitaki alipotuhumiwa kama fisadi? Hapo pia akili ya kuambiwa changanya na zako.
 
'nilishauri mkataba huo uvunjwe' Ulishauri kama nani? Jukumu la kushauri serikali juu ya mambo yote ya kisheria ni la mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General)
 
Lowassa: Nilipeleka documents kuwa kampuni ya Richmond haikuwa halali. Hizo documents nilizipeleka kwa mwanasheria mkuu Johnson Mwanyika. Lakini baada ya siku tano nilipoona mwanasheria mkuu hatekelezi niliamua kuitisha kikao kilichoongozwa na katibu mkuu kiongozi pamoja na makatibu wakuu wahusika akiwemo mwanasheria mkuu. Tuliongea mengi ila mwanasheria mkuu akaomba pumziko la masaa mawili. Alitoka nje kuongea na simu na aliporudi ndani akasema kuwa mamlaka ya juu imeagiza kuwa Richmond ni halali na kila kitu kiendelee kama ilivyokuwa. Mimi Lowassa ningeongea tena nini?

Huu ndio ulikuwa wakati halali wa kujiuzulu kama kweli wewe ujiitakia mazuri nchi hii. Kume ulikuwa hufai, hata urais hutafaa.

Huyu mtu huangalia maslahi hayake zaidi kuliko ya wananchi. Sasa huyu alikuwa waziri mkuu mtendaji au mtendwaji? Maelezo yake hayana mshiko wala hayauziki hata kwa shilingi moja. Viongozi wa bongo ni malaya tu. Maelezo hayana mshiko kabisa.
 
"Nilitaka kuvunja mkataba wa Richmond baada ya kugundua kuna mashaka ya Upatikanaji wake, Alie husika kuingia mkataba aliomba Lisaa limoja na alipo rudi alisema haya nimeambiwa na mamlaka ilio juu ya ofisi ya Waziri Mkuu nisivunje" .

"Mwenye ushahidi aende mahakamani kama huuna ushahidi plz shut up and keep quite.

#Edward Lowasa
#zuiaGoliLaMkono2015

Mkiendelea kuuliza tunamwaga ugali wote.

mwaga kwa maana hii chain ndo tuliisubir mda mrefu
 
mgao kala hv uongozi wa juu yy asiwepo kweli?hv jambo aliandae mkuu wa kaya lowasa asijue kweli?hamna kitu hapa
 
alisema lembeli ukitaka kuona nyeti za kuku subiri upepo. sasa nyeti za kuku hizi hapa!
 
Ni kweli tuna haki watanzania kulaumu alikuwa wapi kuyasema kama alikuwa akituhurumia watanzania lakini pia tunahaki ya kuhoji kwanini serikali haikuchua hatua ya kumshitaki alipotuhumiwa kama fisadi? Hapo pia akili ya kuambiwa changanya na zako.

hapo kweli patata
 
Hiki ni kiwango cha juu kabisa cha uchu wa madaraka mm ningemwona wa maana angefanya hivi wakati wa nyerere aone ,ccm imemlea mpaka amekuwa billionea kwann asiwe wazi tu kwamba kinachompeleka ikulu ni kulinda biashara zake na share kubwa alizonazo kwenye makampuni makubwa hapa nchini
 
Good question.

Angeteuliwa kuwa mgombea wa CCM angetoka na kusifia kila kitu.

Sijui humu ndani kuna mataahira wangapi., lakini siwezi kuwa mmoja wa machizi wanaoweza kuamini dhamira ya Lowassa ni njema, baada ya kukaa kimya kwa miaka 8 kuhusu kitu alichojua ni kosa,au kuhusu ushiriki wake.

lakin kwa kuwa shake before use wako wengi,kuna watu watakunywa hii kool aid bila hata ku-shake well before drinking.

Aliogopa mamlaka ya juu itambabu sea yeye na familia yake.
 
Kwa hiyo kukaa kwetu gizani kote , kumbe bwana Mkubwa ndo mhusika sio, aiiseee,,,, ndo maana hanaga stress , anacheka tu
 
Ndio ujue uongo mwingine ni wakitoto kwan waziri mkuu na mwanasheria mkuu ni nan mwenye kuongea na mamlaka za juu zaid ya mwenzie ?asitufanye watoto wadogo na Kama angepitishwa angesema yote hayo, yeye aseme atatufanyia nn sio kujibu vitu kitoto namna lie alafu Watu mnachekelea

Acha povu katika masuala ya mikataba mwanasheria Ndo anahusika. Ye alitaka majibu kwa mwanasheria mkuu.
 
Sijasikia jibu lolote zaidi ya kuquote hearsay ya AG na KM ambao anajua fika kuwa hawana forum ya kumjibu au kujitetea.
 
Nahisi harufu ya vita kati ya mamlaka ya juu na mheshimiwa Lowassa. Tunasubiri kama upande wa pili nao utakuwa na la kusema au utapiga kimya kama kawaida yake. Hizi siasa bhana zinafurahisha sana wakati mwingine. Mambo yameanza kuwekwa hadharani.
 
Lowassa: Nilipeleka documents kuwa kampuni ya Richmond haikuwa halali. Hizo documents nilizipeleka kwa mwanasheria mkuu Johnson Mwanyika. Lakini baada ya siku tano nilipoona mwanasheria mkuu hatekelezi niliamua kuitisha kikao kilichoongozwa na katibu mkuu kiongozi pamoja na makatibu wakuu wahusika akiwemo mwanasheria mkuu. Tuliongea mengi ila mwanasheria mkuu akaomba pumziko la masaa mawili. Alitoka nje kuongea na simu na aliporudi ndani akasema kuwa mamlaka ya juu imeagiza kuwa Richmond ni halali na kila kitu kiendelee kama ilivyokuwa. Mimi Lowassa ningeongea tena nini?
Nani anaweza kununua hii hekaya!

Yaani Waziri Mkuu anatumia maneno ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati yeye ndiye namba tatu katika utawala wa nchi achilia mbali ile dhana ya kusema yeye hakukutana barabarani na Rais Kikwete. kwa maana kwamba, mahusiano yao yalikuwa zaidi ya mahusiano ya kikazi.

Kwa hiyo Mwanasheria Mkuu alivyomwambia, yeye hakuwasiliana na Rais kutaka kufahamu ukweli wake?

Kwa nini hakuliambia bunge hii story baada ya kupewa nafasi ya kutoa ufafanuzi?

Mtu mwenye fikara pana hawezi kununua hekaya hizi.
 
every thing happens for a reason...kukatwa kwake kulikua kwa sababu kabisaaaaaaa,am gonna love this year's compaign,Gods plan is what i call the whole situation
 
Hebu nisaidieni Je nini kitafuata iwapo kesho Nape Moses Nauye NAYE akiamua kuja UKAWA atapokelewaje
 
Back
Top Bottom