Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Tunajuwa ndio maana tulimwambia mwisho uwazr mkuu. Urais atausikia.

Wewe ni nani? Wenzio wakubwa wenu hawalali wanahangaika usiku mchana kunusuru mambo nchi ina watoka mikononi huku wanaona wewe na keyboard unajifariji
 
Je, wakati fedha za Mkonge kupitia mfanyabiashara aitwaye CHAVDA zinaibiwa Lowassa alikuwa waziri mkuu? Alikuwa malecela!. - Madini ya dhahabu yaliyokamatwa uwanja wa ndege wakati wa Rais Mwinyi yalikuwa ni madini ya Lowassa? - Wakati Akasha wa dawa za kulevya anakamatwa na kutoroshwa aliyehusika ni Lowassa? Waziri Mkuu alikuwa Malecela. - Mrema alipolipua bomu la mwenyekiti wa CCM kuhongwa milioni 900 za minofu ya samaki alikuwa ni Lowassa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye . - Kashfa ya sukari alikuwa ni Lowasa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye. - Kashfa ya Loliondo gate 1992 ya mtoto wa mfalme wa Kuwait alikuwa ni Lowassa? Kinana na Abubakar Mgumia walihusika. - Wanyama hai kutoroshwa nje ya nchi alikuwa Lowassa? Waziri mkuu Pinda. - EPA aliyeidhinisha fedha zichukuliwe alikuwa Lowassa? Mkapa na Mangula wanajua. - NBC Bank kuuzwa alikuwa Lowasa? Mkapa na Sumaye wanahusika. - Kiwira alikuwa Lowassa? Mkapa na Sumaye wanahusika. - Rada na ndege ya rais alikuwa Lowassa? Mkapa, Chenge na Dr. Rashid walihusika. - Mkataba wa Buzwagi alikuwa Lowassa? Karamagi,Kikwete na Mwakapugi walihusika. - Stimulus package ya wakulima wa pamba baada ya Mdororo wa uchumi duniani alikuwa Lowassa? Kigwangala na Kikwete wanajua. - Fedha za Bunge la Katiba zilizobaki baada ya UKAWA kususia Bunge hilo bilioni 3.87 alizichukuwa Lowasa? Sitta, Samia suluhu wanahusika. -Bilioni 250 zilizolipwa wakandarasi hewa wa ujenzi wa barabara alikuwa Lowassa? Magufuri na Tizeba wanahusika. - TTCL Kuuzwa kwa bei ya kutupa kwa Celtel alikuwa ni Lowassa? Mwandosya analo jibu. - Mabehewa mitumba zilizonunuliwa alikuwa ni Lowassa? Mwakyembe anahusika. - Kashfa za pembejeo za wakulima alikuwa ni Lowassa? Wassira na Pinda wanahusika. - Fedha za Gadaffi alikuwa ni Lowassa? Alikuwa ni Membe. - Ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Italia alikuwa ni Lowassa? Kikwete na Mahalu wanahusika. - Escrow tegeta account alikuwa ni Lowassa? Kikwete, Muhongo, Maswi, Albert Marwa wanahusika. - Mradi wa malaria no more alikuwa ni Lowassa? January Makamba mhusika.

umesahau aliyetudanganya eti balali kafa ?
 
Naam, umenena vyema sana.

Lakini nnakuhakikishia Watanzania wengi wamesha mdharau. Wameshajuwa hana akitakacho zaidi ya madaraka na uwezo wa kuongoza kwa sasa hana.

Mimi nimemdharau zaidi Mbowe kwa kubadilika ghafla na kwa haraka zaidi ya kinyonga!

Yaani sikutarajia Chadema kuikosa penati kirahisi hivi.
 
huu ni zaid ya upuuzi kwani Jakaya mrisho Kikwete anaongoza serikali ya kidikteta? Achane kumchafuwa mzee wa watu.
stock-photo-funny-young-man-scared-of-injections-50510104.jpg

kuwa mpole na utulie ili udungwe sindano vizuri.povu halita kusaidia kitu.
 
Hapa kuna visasi ,kwa ngazi ya Waziri Mkuu ,huwezi kukwepa eti ngazi za juu zimeamuru wakati wewe mwenyewe ni sehemu ya hiyo ngazi! Huyu jamaa hafai amuogope Mungu
 
Mtu mwadilifu siku zote husimama katika ukweli na haki.Kama aliona mkataba wa Richmond una matatizo kwa nini hakugoma kusaini? Na hata kujiuzulu kama aliona watu wanataka asaini ili kulinda hadhi yake ya uadilifu na kulinda mali za umma?

Kusema alishinikizwa kusaini alishinikizwaje? Alishikiwa bastola au? Madhara ya kusaini kisheria si anayajua? Aliyesaini ndiye mhusika mwenyewe au hilo halijui.Kwa taratibu za kikazi hakuna kitu kinachoitwa kushinikizwa kusaini.Mtu anayesaini ana uhuru wa kukubali kusaini au kukataa na hata kujiuzulu akiona kutia sahihi huko kutampa matatizo huyo aliyesaini.

Kama aliidhinisha RICHMOND kusikizia kuwa alipata shinikizo toka juu ni uongo na utapeli mkubwa angegoma kusaini na angejiuzulu na akaeleza sababu za kugoma kusaini na kujiuzulu kuwa ni kwa sababu hataki Richmond leo hii angekuwa shujaa wa kimaadili.Kusaini kunaonyesha mzee mzima alikula pesa aache uongo.Zigo la Richmond analo.
 
NILIWAITA MAKATIBU WAKUU kutaka kuvunja mkataba wa Richmond lakini Mwanasheria Mkuu Ndugu Mwanyika aliporudi kutoka nje alisema kuwa nimepokea simu kutoka mamlaka ya juu kuwa mkataba usainiwe. Mwisho wa kunukuu. Sisi kama waumini wa CCM tumefadhaishwa na maneno haya na hivyo tunaomba maneno haya yakanushwe katika vyombo vya habari, magazeti na hata kwenye redio vinginevyo huku mitaani hakukaliki.
 
Hili lilishaisha siku nyingi kwenye mikutano ya chama chake cha zamani alishalalamika walimwachilizia na kumtafutia vijana wawe wanamchafua ila wenyewe watakuja watakupa majibu mkuu
 
Wakati huo hakuwa muadilifu na hakujua madhara ya kukumbatia dhambi, leo hii anajuta ndio maana kaamua kuzaliwa upya, ushirika tena na shetani basi......ya kale yamepita na sasa yamekuwa mapya.
 
NILIWAITA MAKATIBU WAKUU kutaka kuvunja mkataba wa Richmond lakini Mwanasheria Mkuu Ndugu Mwanyika aliporudi kutoka nje alisema kuwa nimepokea simu kutoka mamlaka ya juu kuwa mkataba usainiwe. Mwisho wa kunukuu. Sisi kama waumini wa CCM tumefadhaishwa na maneno haya na hivyo tunaomba maneno haya yakanushwe katika vyombo vya habari, magazeti na hata kwenye redio vinginevyo huku mitaani hakukaliki.

Ili iweje? hakuyasema hayo alipopewa nafasi ya kujieleza bungeni, badala yake akasepa na kutangaza kujiuzulu? leo nani atamwamini mpenda madaraka huyo?
 
Akihojiwa na Tido Mhando TBC aliwahi kusema akipewa nafasi atasign tena Mkataba wa Richmond kwa vile haoni Makosa, Mwakyembe akajibu.. Akamashauri akae kimya sababu alichokifanya anakijua na kama akipewa nafasi akaridia atashughulikiwa tena.
 
Huyu mammvi siyo amewehuka kweli,haya tutamwona anachokitaka jasho litamtoka,
 
NILIWAITA MAKATIBU WAKUU kutaka kuvunja mkataba wa Richmond lakini Mwanasheria Mkuu Ndugu Mwanyika aliporudi kutoka nje alisema kuwa nimepokea simu kutoka mamlaka ya juu kuwa mkataba usainiwe. Mwisho wa kunukuu. Sisi kama waumini wa CCM tumefadhaishwa na maneno haya na hivyo tunaomba maneno haya yakanushwe katika vyombo vya habari, magazeti na hata kwenye redio vinginevyo huku mitaani hakukaliki.

Kama ndio ukweli ukanushwe wa nini...!!??
Acha kutoka povu mkuu..
Au na wewe ulizoea vya bure kwa Ccm ...!!??
Hakuna chochote mtaani kitakachotokea maana hata mwananchi yule mjinga kabisa ameujua ukweli na anamwamini Lowasa so kipt ur mouth off..
 
Lowasa hawezi kukwepa kashifa hii hata akiogamaji ya baarini.

Punguza wasi wasi kwani unauza mirungi...
Ukawa Ikulu taka usitake ..
Kuwa mpole angalia Mchezo dakika 90 tu utaamini kitachotokea..
 
Tulieni dawa iwaingie, maana sindano lazima iwachome na mpate maumivu kidogo. Baadae maumivu yatapoa na mtapona tu.
 
Back
Top Bottom