Je, wakati fedha za Mkonge kupitia mfanyabiashara aitwaye CHAVDA zinaibiwa Lowassa alikuwa waziri mkuu? Alikuwa malecela!. - Madini ya dhahabu yaliyokamatwa uwanja wa ndege wakati wa Rais Mwinyi yalikuwa ni madini ya Lowassa? - Wakati Akasha wa dawa za kulevya anakamatwa na kutoroshwa aliyehusika ni Lowassa? Waziri Mkuu alikuwa Malecela. - Mrema alipolipua bomu la mwenyekiti wa CCM kuhongwa milioni 900 za minofu ya samaki alikuwa ni Lowassa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye . - Kashfa ya sukari alikuwa ni Lowasa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye. - Kashfa ya Loliondo gate 1992 ya mtoto wa mfalme wa Kuwait alikuwa ni Lowassa? Kinana na Abubakar Mgumia walihusika. - Wanyama hai kutoroshwa nje ya nchi alikuwa Lowassa? Waziri mkuu Pinda. - EPA aliyeidhinisha fedha zichukuliwe alikuwa Lowassa? Mkapa na Mangula wanajua. - NBC Bank kuuzwa alikuwa Lowasa? Mkapa na Sumaye wanahusika. - Kiwira alikuwa Lowassa? Mkapa na Sumaye wanahusika. - Rada na ndege ya rais alikuwa Lowassa? Mkapa, Chenge na Dr. Rashid walihusika. - Mkataba wa Buzwagi alikuwa Lowassa? Karamagi,Kikwete na Mwakapugi walihusika. - Stimulus package ya wakulima wa pamba baada ya Mdororo wa uchumi duniani alikuwa Lowassa? Kigwangala na Kikwete wanajua. - Fedha za Bunge la Katiba zilizobaki baada ya UKAWA kususia Bunge hilo bilioni 3.87 alizichukuwa Lowasa? Sitta, Samia suluhu wanahusika. -Bilioni 250 zilizolipwa wakandarasi hewa wa ujenzi wa barabara alikuwa Lowassa? Magufuri na Tizeba wanahusika. - TTCL Kuuzwa kwa bei ya kutupa kwa Celtel alikuwa ni Lowassa? Mwandosya analo jibu. - Mabehewa mitumba zilizonunuliwa alikuwa ni Lowassa? Mwakyembe anahusika. - Kashfa za pembejeo za wakulima alikuwa ni Lowassa? Wassira na Pinda wanahusika. - Fedha za Gadaffi alikuwa ni Lowassa? Alikuwa ni Membe. - Ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Italia alikuwa ni Lowassa? Kikwete na Mahalu wanahusika. - Escrow tegeta account alikuwa ni Lowassa? Kikwete, Muhongo, Maswi, Albert Marwa wanahusika. - Mradi wa malaria no more alikuwa ni Lowassa? January Makamba mhusika.