Swali la kwanini mnamuogopa Lowasa limeshajibiwa jana na hatuhitaji majibu zaidi.
Tunaomba kabla hujaondoka madarakani urudishe pesa zetu zote mlizotuibia na kutuongezea umasikini, ugumu wa maisha, ujinga, vifo vya watanzania wengi na uporaji wa mali za taifa hili kwa maslahi yenu wenyewe na familia zenu.
Mmetudanganya, mmetufanya wajinga, mmeturubuni, mmewaua ndugu zetu, mmeua elimu yetu alafu leo tena msimame majukwaani kusema tuichague tena CCM? Hapana, ONDOKENI TUMEWACHOKA.
Kwa hili lililotokea jana, Rais yeyote mwenye utu, haiba na utashi mwema kwa uongozi na wananchi wake, mwajibikaji na mpenda haki, Mcha Mungu lazima angechukua hatua ya kujiuzuru. ONDOKENI TUMEWACHOKA.
Pesa uchukue wewe na familia yako, mjinufaishe wenyewe, kila mali za taifa mmiliki wenyewe alafu na pesa za madawati ya shule pamoja na Maabara tuchangie sie..... shame on you corrupt government. ONDOKENI TUMEWACHOKA.
Mliuficha ukweli mkidhani hautakuja kutoka, mkawakandamiza wengi na wengine hata kuwaua, kuwatoa meno, kuwapiga na kuwatesa ili tu wasiongelee uovu wenu uliokithiri ndani ya Taifa hili.. ONDOKENI TUMEWACHOKA
Mmeiharibu CCM na kukifanta kuwa chama cha kidugu kupitisha maslahi yenu ili kulinda maslahi yenu. MUDA WENU UMEKWISHA. Mali mlizoiba na mambi mliyotufanyia yanatosha sana na hamna jipya la kutufanyia wanachi.... ONDOKENI TUMEWACHOKA
Mmevigeuza vyombo vya Usalama wa Taifa kuwa vyombi vya kutekeleza maamuzi yenu na kufanya mambo mnayoyataka mkihisi mtakaa milele katika dola, hapana... Udhalimu wenu, uonevu wenu na mambo yote mliyotufanyia watanzania mkihisi muda huu hautafika sasa halitasalia jiwe ambalo halitageuzwa mpaka wote muwe mmeondoka katika mfumo wa kinyonyaji, wizi na uonevu mlioujenga ndani ya nchi hii. ONDOKENI TUMEWACHOKA
Ni muda sasa umefika wa kuwa na Tanzania Mpya, sio Tanzania ile mliotudanganya ni ya KASI MPYA YA WIZI, NGUVU MPYA YA UKANDAMIZAJI WA DEMOKRASIA NA MAONI YA WENGI ila Tanzania yenye uwezo wa kuwanufaisha watanzania wote kulingana na rasilimali ilizojaaliwa.
JEI KEI na Familia yako, Chama Cha Mapinduzi..... ONDOKENI TUMEWACHOKA
Tumechoka!! Tunahitaji Joshua mpya wa kutuvusha kuelekea nchi ya Ahadi.
Tunahitaji kiongozi mpya wa kutufanya tufurahie utajiri wetu.
Ni mimi Fandre baba Cheupe
#SAFARI YA MATUMAINI INAENDELEA
#UKAWA TUMAINI LETU