Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

One of the owners of Richmond is Rostam and he is the best buddy and financier of the Lowassa, so what do you think?

Kumbuka Rostam alikuwa mwekahazina wa ccm na hivyo ccm yote imeoza.Lowasa kakataa kuutumikia mfumo fisadi
 
Wanasubiri kampeni zianze ili kuchukua hatua uku kampeni zikiendelea

Hii ishu ya Edward Lowassa vs kinachoitwa ufisadi wake wa Richmond vs Mamlaka ya juu ambayo ni ofisi ya Rais ambaye tangu wakati huo mpaka leo ni huyu bwana anayeitwa Jakaya Mrisho Kikwete, ni ngumu na ni kaa la moto kwa maCCM!!

Watu tayari wanazo data za uchafu wote wa Ikulu chini ya huyu bwana (ambaye kiuhalisia yeye ndiye fisadi papa) mkononi na sidhani kama watatoka mwaka huu!!

Kama bado hujaelewa basi subiri tu walianzishe!!
 
Maelezo ktk mada na matamko ya Lowasa

1. Amesema kwa wenye ushahidi waende mahakami, na akasema kama kuvunja mkataba uliokuwa chini aliingiliwa na watu wa juu kwakila hatua aliyotaka kuchukua angefanyaje? aliyekuwa juu ya Waziri mkuu ni nani? Anaweza kuwa Shein? Obvously no; anaweza kuwa nani; jaza ndio maana watoto kwa sasa matajiri wa kutupwa

2. Mwakyembe anasema, kuna mengine hayamo ktk andiko la kamati ya bunge kwa sababu kama tungeyaweka hadharani nchi ingepasuka; hapa inadhihirisha tuhuma za lowasa ilikuwa kisingizio maana mkubwa wake alikuwa anajulikana na alijua nini kinaendelea hatua zote ila ilivyokuwa moto ikabidi kutoa kafara an yeye akakubali kikombe hicho; ubaya hakuwaambia mawakala wake akazidi kuwatumia vijana kumchafua lowasa wakiwemo akina nape na akinia makondoa kwa maslahi aonekane alijiuzuru kihalali na wengine wakapandishwa vyeo

Uchaguzi huu sasa tunampa mchawi kulea mtoto wetu kura zetu zote kwa Lowasa
 
hapo nawaza vp kama kwel upo?, na wahusika ni weng nao wakameza bomu kwamba mwaga mboga namwaga ugali?
 
Najiudhuru uwaziri mkuu kulinda serekali yangu na chama changu..Edward lowassa

Ukisoma post za kina miraj na ridhiwani utaona kuna uasama mbele ya lowassa,...

J.K ametumia nguvu zake zote kumtosa Lowassa,,Ila bado nguvu za wananchi..

Lowassa sio fisadi,lowassa ana ogopwa na mafisadi wanao itumia nchii kuvunia matumbo yao..wanataka kuendelea kuwala tu..

Historia ya nchi hii,itamsimulia lowassa kushinda viongozi wengi walio pita kwa ujasiri na uthubutu..

Wanasemaga siasa ni maisha,kama kijana nimejifunza katika maisha,hakuna kinacho weza kusitisha safari yako kama sio wewe mwenyewe.lowassa ametukanwa sana,wakubwa kwa wavijana,ila hajakata tamaa..

lowassa lowassa lowassa,october watanzania wata ishangaza dunia...
 
kitakacho.mponza lowassa kushindwa october ni kuendelea kukaa kimya badala ya kuyasema maovu ya richmond hadharani na waliohusika.
 
kitakacho.mponza lowassa kushindwa october ni kuendelea kukaa kimya badala ya kuyasema maovu ya richmond hadharani na waliohusika.
Tulia bado chakula hakijaiva, kampeni zikianza atatupakulia!
 
tusubir oct,mda mwngne naona kama plan hvi kwamba el awe rais maana friend wako akiona huku hupati anaweza kufanya njia ya kukuwezesha upande wa pili...kimficho kama hakupend hv,yan anakutupia kwa adui aliyekuwa tishio kwenu lakn ukienda ww adui anaridhka ...We unaonaje
 
Uchaguzi wa mwaka huu kama kweli lowasa hajatumwa kuvuruga ukawa basi tutaskia siri nyingi kwenye kampeni ili kuchafuana
 
Najiudhuru uwaziri mkuu kulinda serekali yangu na chama changu..Edward lowassa

Ukisoma post za kina miraj na ridhiwani utaona kuna uasama mbele ya lowassa,...

J.K ametumia nguvu zake zote kumtosa Lowassa,,Ila bado nguvu za wananchi..

Lowassa sio fisadi,lowassa ana ogopwa na mafisadi wanao itumia nchii kuvunia matumbo yao..wanataka kuendelea kuwala tu..

Historia ya nchi hii,itamsimulia lowassa kushinda viongozi wengi walio pita kwa ujasiri na uthubutu..

Wanasemaga siasa ni maisha,kama kijana nimejifunza katika maisha,hakuna kinacho weza kusitisha safari yako kama sio wewe mwenyewe.lowassa ametukanwa sana,wakubwa kwa wavijana,ila hajakata tamaa..

lowassa lowassa lowassa,october watanzania wata ishangaza dunia...

mi naona amemsaidia, unajua isingekuwa hv dr slaa /ukawa wangetumia hoja ya ufsad kumuangusha el...Ni kama cnema hvi
 
Imechapwa 21 July 2010

MADAI mapya ya Edward Lowassa, yule waziri mkuu aliyejiuzulu, kwamba hata kama angekuwa madarakani angeendelea kushirikiana na kampuni ya Richmond, yameibua mapya.

Akizungumza na kituo cha Televisheni cha TBC1 Ijumaa iliyopita, Lowassa alisema hajutii “uamuzi wa kuipa kazi Richmond.” Anasema hata kama angerudi leo madarakani, bado angeendelea na mpango huo uliozaa kashfa iliyommomonyoa kisiasa. Lowassa alijiuzulu wadhifa wake, Februari 2007 baada ya kutuhumiwa kufanya upendeleo wa kuipa kazi kampuni ya Richmond Development Company (LLC) kutoka Marekani.

Kampuni hiyo ambayo ilikuja kuthibitika kuwa haikuwa na sifa wala uwezo wa kifedha na kitaaluma, ilipewa jukumu la kuzalisha megawati 100 za umeme wa dharura. Ilishindwa. Wakati Lowassa akijitapa kwamba uamuzi wake ulikuwa sahihi, taarifa kutoka ndani ya serikali na Kamati Teule ya Bunge, zinasema Lowassa alitumia madaraka yake vibaya kwa kuagiza kufutwa kwa zabuni ya kufua umeme ambayo tayari ilipewa kampuni ya CDC Glogbeleq kutoka Canada.

Uamuzi wa Lowassa wa kufuta zabuni ya CDC ndio ulisababisha taifa kutumbukia katika giza na hatimaye kuingizwa kwa kampuni isiyokuwa na hadhi, sifa wala uwezo wa kufanya kazi iliyoomba â€" Richmond.

Uchunguzi unaonyesha kwamba tarehe 11 Januari 2006, serikali iliteua kampuni ya CDC kuingiza nchini mitambo ya kuzalisha umeme yenye uwezo wa kuzalisha megawati 74. Mitambo ya kampuni hiyo ilikuwa na vipengele vifuatavyo:

Kwanza, ikiwa mkataba wa ukodishaji utakuwa wa miaka mitano, serikali itatakiwa kulipa dola za Marekani 3.2 kwa kWh moja ya umeme itakayotumia.

Pili, iwapo mkataba wa ukodishaji utakuwa wa miaka mitatu, serikali italazimika kujikamua na kulipa kiasi cha dola 5.3 kwa kWh moja ya umeme. Mkataba kati ya serikali na CDC ulikuwa na unafuu mkubwa kwa kuwa kilikuwapo kipengele kinachoelekeza kuwa mara baada ya mkataba wa ukodishaji kumalizika, mitambo iliyokodishwa inakuwa mali ya serikali.

Kwa mujibu wa mawasiliano ambayo gazeti hili linayo, baina ya TANESCO, serikali na kampuni ya CDC, mitambo ya kampuni hiyo ilitarajiwa kuwasili nchini Aprili 2006.

Kampuni ya CDC Glogbeleq ni kampuni tanzu ya kampuni inayofua umeme kwa kutumia gesi ya Songas.
Hadi sasa, hakuna anayefahamu kilichosababisha Lowassa kuingilia mchakato wa zabuni ulioiteua kampuni hiyo ya kimataifa na inayosifika kimaadili, uwezo wa kiuchumi na kiutaalam; na badala yake kuipa kazi hiyo Richmond.
Uchunguzi wa MwanaHALISI unaonyesha kwamba tarehe 20 Februari 2006, Lowassa kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha aliagiza bodi ya zabuni ya Tanesco kuanza mchakato upya.

Mchakato huo ulioibua Richmond kutoka kusikojulikana, ulisimamiwa kwa nguvu zote na Lowassa mwenyewe. Tangazo la serikali la kuitisha zabuni mpya lilitolewa 23 Februari 2006, huku zabuni zikipangwa kufunguliwa 6 Machi 2006 na tathimini kwa wazabuni ikiwa tarehe 7 na 8, Machi 2006. Hata hivyo, kabla Lowassa hajatekeleza mpango wake wa kuipa kazi Richmond, hapo tarehe 22 Februari 2006, mamlaka ya manunuzi ya umma (PPRA) iliandika barua mbili kwa Tanesco.

Barua zote mbili â€" ile yenye Kumb. Na. PPRA/Tanesco/41/16 ya tarehe 23 Februari 2006 na nyingine yenye Kumb. Na. PPRA/Tanesco/47/18 â€" zilikuwa zikitaka kusitishwa kwa zoezi la zabuni zilizozaa Richmond kwa kuwa ilikuwa kinyume cha sheria. Aidha, PPRA ilitaka Tanesco kutafuta moja kwa moja mitambo kutoka kwa watengezaji kwa maelezo kuwa, katika mazingira yaliyopo nchini na kutokana na zabuni kwenda kinyume cha taratibu, zoezi hilo likiendelea litaingiza wazabuni feki.

Lakini katika hali isiyotarajiwa, serikali iligoma kutekeleza maagizo ya PPRA na badala yake ilijibu kwa kile kinachoitwa, “Tumepokea ushauri wenu, lakini uamuzi wa mwisho ni wetu.” Ni katika mkakati huo, serikali iliagiza Tanesco kufungua tenda iliyowekewa masharti ya vigezo 29. Kati ya makampuni tisa yaliyoomba, hakuna hata moja iliyofanikiwa kupenya. Kampuni ya Richmond ilionekana kuwa na mapungufu 17.

Baada ya vigezo hivyo kuonekana vimeshindwa kuibeba kampuni ya Lowassa, ofisi ya waziri mkuu, kupitia katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Arthur Mwakapugi, ilipunguza vigezo hivyo kutoka 29 hadi 16.

Katika mchujo huo, kampuni tano ziliteuliwa ikiwamo Richmond ambayo, hata hivyo, tayari ilikuwa ya mwisho katika mchujo wa awali.

Katika eneo hilo, wazabuni ambao angalau walionekana afadhali walikuwa wanne, yakiwemo makampuni kutoka Italia, Ujerumani, Gapco ya Tanzania na Richmond “ya Marekani.”
“Hata pale Tanesco ilipofanya tathimini ya kina, bado Richmond ilikutwa na mapungufu13 katika vigezo vilivyowekwa,” taarifa zinaeleza.

Kama hiyo haitoshi, nyaraka zinaonyesha tarehe 1 Aprili 2006, serikali kupitia waziri Msabaha ilikataa mapenedekezo ya Bodi ya Zabuni ya Tanesco iliyosisitiza kwamba “hakuna mzabuni mwenye sifa miongoni mwa wazabuni walioomba.” Msabaha alifika mbali zaidi. Huku akijua kuwa ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma kuingilia mchakato wa zabuni, barua yake inayodaiwa kuandikwa kwa maelekezo ya Lowassa, yenye Kumb. Na. CBD/88/286/01, iliagiza kuvunjwa kwa Bodi ya Zabuni ya Tanesco.

Barua hiyo ilitumwa kwa mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya Tanesco. Vilevile, Dk. Msabaha alindika barua nyingine tarehe 12 Aprili 2006 ambayo ilimtaja moja kwa moja Lowassa. Barua hiyo yenye Kumb. Na. CBD/88/286/01, inasema “…suala hili limeshughulikiwa na waziri mkuu baada ya kuunda kamati ya wataalamu ya watu watatu, katibu mkuu wa hazina, katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini na mwanasheria mkuu wa serikali.”

Barua hiyo ilieleza pia, “Nia ni kuliondoa suala hili mikononi mwa Tanesco na isije tena picha ya kuendelea na suala hilo, maana huko ni kukiuka maagizo ya waziri mkuu.”

Kujitumbukiza kwa Lowassa katika mchakato wa zabuni ulianza kuonekena tarehe 10 Februari 2006, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la Mawaziri ulioongozwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, serikali iliamuru wizara ya nishati na madini kuwasiliana na CDC kwa mambo mawili.

Kwanza, kuiomba kampuni hiyo kuuza mitambo yake moja kwa moja badala ya kuikodisha.

Pili, kama ombi la kutaka serikali kuinunua litakataliwa na CDC, basi mitambo itakayoagizwa ikodishwe katika kipindi kile tu cha ukame na kwamba baada ya ukame kumalizika mitambo hiyo irejeshwe kwa CDC.
Hata hivyo, kinyume na maagizo ya Baraza la Mawaziri, taarifa zinaonyesha mara baada ya mkutano huo, Lowassa alimuagiza aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya nishati, Mwakapugi kuvunja mkataba.

Katika kile kilichoelezwa kuwa ni kutekeleza maelekezo ya Lowassa, tarehe 10 Februari 2006, mara baada ya kikao cha baraza la mawaziri kumalizika, Mwakapugi aliandikia barua Kumb. Na. CBD286/297/01 kwenda CDC.
Barua ya Mwakapugi inasema, “Licha ya maendeleo mazuri mliyoyafanya katika mradi huu, serikali imeamua kufuta ukodishaji wa mitambo, badala yake itaipatia Tanesco fedha za kununua, kufunga na kuzindua mitambo yake na ya aina hiyohiyo.”



Inaarifiwa kwamba Mwakapugi alieleza Kamati za Nidhamu zilizokuwa zinasikiliza utetezi wa watuhumiwa wakuu wa Richmond, jinsi alivyokuwa tarishi wa Lowassa katika kuipa kazi Richmond. Inaelezwa kwamba katika vikao hivyo, Mwakapugi alitoa hadi vimemo vya Lowassa vilivyokuwa vikimtaka kuvunja mkataba na kuipa kazi kampuni aliyotaka Lowassa, pamoja na kwamba alijua haikuwa na sifa kwa kila hali.

“Mle ndani ya Kamati za Nidhamu kulifumuka mambo mengi. Kuna wakati watu waliumbua wakubwa. Kwa mfano, Mwakapugi alitoa hadi vimemo vilivyokuwa vinaonyesha jinsi Lowassa alivyomshinikiza kuipa kazi Richmond, pamoja na kwamba alijua kuwa haikuwa na sifa ya kupewa kazi iliyoomba,” zinaeleza taarifa zisizopingika.

Hoja ya kupindisha maamuzi ya Baraza la Mawaziri ambapo Lowassa aliagiza kuvunjwa kwa mkataba, ilitawala mjadala wakati wa mahojiano yaliyodumu kwa siku nne kati ya Kamati Teule ya Bunge na Dk. Msabaha aliyekuwa waziri wa nishati na katibu wake Mwakapugi.

Kwa mujibu wa Hansard ya Bunge, Kamati ilitaka maelezo katika maeneo yafuatayo kutoka kwa Dk. Msahaba na Mwakapugi: Kwanza, iwapo kulikuwa na kikao kingine cha Baraza la mawaziri kilichofanyika tarehe 10 Februari 2010 na kubatilisha maamuzi ya kwanza.

Pili, kama hakukuwa na kikao kingine cha baraza la mawaziri, kwa nini wizara ya nishati na madini ilipeleka ujumbe tofauti CDC kinyume cha maagizo ya baraza la mawaziri?

Tatu, kwa nini barua ya wizara kwenda CDC ilipelekwa hata kabla ya kampuni hiyo kujibu maombi ya serikali ya kutaka kubadilisha mkataba?

Nne, Kamati ya Bunge iliuliza: Je, maamuzi kama haya yaliyochukuliwa siku nne baada ya mgawo wa umeme kuanza, huku serikali ikiwa haina kampuni mabadala, yalikuwa sahihi au yalilenga kunufaisha kikundi fulani cha watu ndani ya serikali?

Si Msabaha wala Mwakapungi aliyeweza kujibu kwa ufasaha maswali yaliyoulizwa na Kamati.

Wakati hayo yakiwa ndani ya serikali, Kamati Teule ya Bunge iling’amua kuwa kumwita na kumhoji Lowassa kungevuruga ushahidi na kukwamisha kazi za Kamati.

Aidha, ilihofia mamlaka ya rais kuingilia kati. “Unajua, Kamati Ndogo ya Bunge, haikuwa na mamlaka ya kuhukumu waziri mkuu. Kazi ya kuhukumu au kumwajibisha, ilibaki mikononi mwa Bunge. Hilo ndilo lililomuidhinisha na ambalo linaweza kumfukuza kazi,” ameeleza mjumbe mmoja wa Kamati Teule.

Kwa mujibu wa mamlaka za Bunge, kuita na kuhoji waziri mkuu kungehitaji kibali cha Spika ambaye naye angelazimika kupata ridhaa ya rais wa Jamhuri.

Wengi wanakiri kuwa hekima iliongoza Kamati Teule. Badala ya kumhoji Lowassa ilipendekeza kwake kujitetea mbele ya Bunge na juu ya masuala yaliyomgusa na Bunge lingeamua baada ya kusikiliza maelezo yake,” kimeeleza chanzo kingine cha habari.

Kwa kuzingatia utendaji wa Rais Kikwete na majukumu aliyonayo, kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kuchelewa kutoa idhini ya kumhoji Lowassa. Vilevile huenda rais angenyamaza ili asionekane mbaya na kazi mzima ya kamati ingekwama, ameeleza mmoja wa wajumbe wa Kamati alipoulizwa juu ya kiini cha Lowassa kudai kuwa bado anashikilia Richmond.

Majigambo ya Lowassa yameonekana kwa wachunguzi wa siasa za CCM kuwa njia ya kujikosha kwa kuendelea kung’ang’ania kuwa alikuwa sahihi kutoa mkataba kwa kampuni iliyofeli kutenda wajibu wake


Chanzo: Mwanahalisi
 
Lowassa aibua mapya

Na Saed Kubenea - Imechapwa 21 July 2010

Huwa nnawashangaa watu kama nyinyi mnao angaika kuleta makablasha meng yaliyopitwa na wakati mitandaoni wakati huyo mtu mnae angaika kumchafua amejaa uchafu mpka kwenye damu yake yan hata huo uchafu mnaojitahd kumwongezea hauna nafas pakuuweka ndio maana watu wenye akili timamu huwa tuna wapuuza na vihabar vyenu uchwala mnahaika mitandaoni wakati raisi kashapatikana na wahusika wakuu wanafahamu hilo ila wanafanya siri ili kuwapumbaza wananch wa Tanzania pamoja na nchi za magharibi na vibaraka wao.

ACHENI KULALA WATANZANIA AMKENI SERIKALI INA SIRI KALI AMBAYO WACHACHE WANAO BAHATIKA NDIO WANAOIFAHAMU"

NB:
Acheni kushabikia mambo musio yafahamu undani wake.
 
Kinana: Lowassa safi, Nyalandu anazurura



"Mfano ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye anafanya kazi ya kuzunguka nchi nzima na maeneo mengine wakati mizunguko yake haisaidii kuondoa matatizo ya wananchi." Kinana

Kwa ufupi


  • Katibu huyo wa CCM amwelezea kuwa ni mtu shupavu na mchapakazi
  • Waziri ajibu kuwa analijua tatizo la wananchi, litatuliwa wiki mbili zijazo

By Habel Chidawali, Mwananchi Kondoa/Monduli. Jana ilikuwa siku ya hisia tofauti kwa watu wawili wanaotajwa kwenye kinyang'anyiro cha urais, Edward Lowassa na Lazaro Nyalandu baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kumsifu mmojawao na kumponda mwingine.

Akiwa Kondoa, Kinana alitumia muda mwingi kujibu kilio cha wananchi wanaosumbuliwa na askari wa wanyamapori kwa kumponda Waziri Nyalandu kuwa anazurura bila kushughulikia matatizo ya wananchi, lakini saa chache baada ya kuwasili Monduli alimsifu Lowassa kuwa ni kiongozi shupavu.

Tayari Nyalandu ameshatangaza nia ya kugombea urais, wakati Lowassa, mmoja wa wanachama wa CCM wanaotajwa sana kwenye kinyang'anyiro hicho, hajatangaza uamuzi wake lakini anatumikia adhabu ya chama chake kilichomfungia kujihusisha na harakati za uongozi pamoja na makada wengine watano.

Baada ya msafara wa Kinana kuwasili Monduli na kupokewa na viongozi wa chama hicho wa eneo, katibu huyo wa CCM, Kinana alipata nafasi ya kuzungumza machache kabla ya kuanza safari ya kukagua shughuli mbalimbali.

"Hatuna shaka na Monduli kwa kuwa yupo kiongozi shupavu, ndugu yetu Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa (Halmashauri Kuu ya CCM) Nec," alisema Kinana akiwaelezea wananchi waliokuwapo eneo hilo.

"Wa Monduli mna kiongozi shupavu na mchapakazi. Hongera Bwana Lowassa."

Baadaye, Lowassa aliwakaribisha akisema: "Mmefanya kazi kubwa sana ya kukijenga chama chetu. Nawashukuru sana, karibuni."

Naye katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: "Nafurahi kuwa katika jimbo la mzee wangu, rafiki yangu Edward Lowassa. Mapokezi mazuri, bila shaka Arusha mmeamka."

Kinana amekuwa akitumia sehemu kubwa ya ziara yake kushuhutumu viongozi wa Serikali na hasa mawaziri kwa kushindwa kuwatatulia wananchi matatizo yao na ilifikia wakati aliwataja mawaziri wanne aliowaita kuwa ni mizigo, tofauti na alivyofanya kwa waziri mkuu huyo wa zamani.

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne na anajulikana kama mtu aliye tayari kufanya uamuzi mgumu. Alilazimika kujiuzulu wadhifa huo mwaka 2008 baada ya kuibuka kwa kashfa ya Richmond.

Kinana alikuwa mtu tofauti wakati akijibu kero za wananchi mkoani Singida, ambako alimtaja moja kwa moja Waziri Nyalandu kuwa hashughulikii matatizo ya wananchi na badala yake amekuwa akizunguka bila msaada wowote.

Kinana alisema hayo juzi katika Kijiji cha Ikengwa, Kata ya Kinyasi wilayani Kondoa baada ya wananchi wa kijiji hicho kumchongea Nyalandu kwa Kinana kwamba wizara yake inawaua na kuwaumiza bila ya hatia, hivyo wamechoka.

Wananchi hao walisema mateso wanayoyapata kutoka kwa askari wa wanyamapori katika Pori la Mkungunero ni makubwa ambayo yanalenga kuondoa uhai wa watu.

Katibu wa CCM wa Kata ya Inyasi, Jusberi Jumanne aliyesoma risala ya malalamiko hayo, alisema wanaishi ndani ya kijiji chao na kufanya shughuli zao za kilimo, lakini kila wakati wanachomewa nyumba, mazao yao kufyekwa na hata kuwasababishia ulemavu na vifo.

"Mheshimiwa katibu mkuu, hapa ni kijiji halali kilichosajiliwa 1974 na kupewa hati 398, lakini hifadhi hiyo ilikuja kuweka mipaka yao mwaka 2006, jambo hili sisi tunaona ni uonevu ambao tunafanyiwa bila ya kushirikishwa na kuambiwa tuhame kwa nguvu na hatujui mahali pa kwenda," alisema.

Akijibu hoja hiyo Kinana alionekana kukerwa na namna maisha ya watu wa maeneo hayo yasivyoshughulikiwa ili nao waishi kama Watanzania wengine.

"Ni jambo la aibu kwa Waziri wa Maliasili na Utalii kusikia migogoro lakini yeye akawa kimya,"alisema Kinana.

"Nyalandu awaeleza Watanzania kama kuna mahali amefanikiwa kumaliza kabisa migogoro walau 10 kwani amekuwa ni bingwa wa maneno na matembezi."

Kinana alisema ni lazima Nyalandu abebe msalaba huo kwani roho za binadamu zina thamani… ni heri roho ya binadamu kuliko mnyama ingawa alizuia wanyama wasiuawe.

"Hawa mawaziri lazima waje, na nina wasihi waje haraka, yaani Waziri wa Maliasili na Utalii na mwenzake wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi," alisema.

"Mfano ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye anafanya kazi ya kuzunguka nchi nzima na maeneo mengine wakati mizunguko yake haisaidii kuondoa matatizo ya wananchi."

Kinana alitaka kamatakamata ya wananchi isimamishwe kwanza hadi ufumbuzi kuhusu mipaka ya pori hilo itakapoangaliwa upya. Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, Waziri Nyalandu alisema anakubaliana na alichosema Kinana, lakini akataka watu wajjue kuwa mgogoro huo ni wa muda mrefu.

"Mgogoro huo ni wa siku nyingi, hivyo busara inahitajika sana kulinda watu, mali zao na maliasili. Niliunda kamati ambayo yumo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na Manyara, Ma-RAS (maofisa utawala wa mikoa) wao na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambayo imefanya uchunguzi pamoja na kuongea na wananchi," alisema.

"Kamati inatarajiwa kumaliza kazi wiki hii na itanikabidhi kwa kuwa mimi ndiye niliyeiunda. Nimepanga kwamba ndani ya hizi wiki mbili za Bunge, mimi na Waziri wa Ardhi tutatangaza suluhisho la tatizo hili. Tutaenda pamoja Mkungunero kuongea na wananchi."

Katika mkutano huo, Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Zabein Mhita alisema kuwa katika kata hiyo na maeneo mengine kumekuwa na kelele zinazotishia amani na tayari kwa baadhi ya watu wameshapoteza maisha.

Walimkabidhi Kinana maganda ya risasi pamoja na rundo la mabaki ya nguo zilizochomwa moto na askari wa wanyamapori.
 
mbona mnaahangaika jamani mara ooh mtt wake anamiliki nyumba mbele mara ooh sijui nn na nn ....mtakonda bure mafuriko hayazuiliki kwa kiganja
 
jk+lowassa[1].jpg
JK: Lowasa jembe


Kwa ufupi


  • Mnaweza kuchafuana leo, kesho mkapata mgombea mwenye nundu nyingi na mabandeji kila mahala, halafu mkapata shida kumnadi.

By Waandishi Wetu Dodoma/Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amemwagia sifa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hatua ambayo inaweza kutafsiri mengi katika medani ya siasa nchini.

Akizungumza na wabunge wa CCM kwenye Ukumbi wa White House Dodoma juzi, Rais Kikwete ambaye pia mwenyekiti wa chama hicho, alisema nguvu za Lowassa pekee zinatosha kushinda uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani Kata ya Makuyuni kilichoko wilayani Monduli.

Kata ya Makuyuni iko wilayani Monduli, ambako Lowassa amekuwa mbunge wake tangu mwaka 1995.

Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa Makuyuni, baada ya kuwa ametoa ruksa kwa makada wa chama hicho wanaotaka urais kuanza kujipitisha pitisha miongoni mwa wanachama wa chama hicho. Lowassa anatajwa kuwa miongoni mwa wanaCCM wanaotaka kumrithi Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

"Sina tatizo na pale Makuyuni, najua muscles (misuli) za Mzee Lowassa zinatosha kutupa ushindi; au vipi mzee?" alidokeza mmoja wa wabunge wa CCM akimnukuu Rais Kikwete.

Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Makuyuni unaotarajiwa kufanyika Juni 16, mwaka huu, utakuwa wa ushindani mkali kati ya CCM na Chadema ambao historia yao kisiasa mkoani Arusha ni ya uhasama.

Katika uchaguzi huo, unaofanyika baada ya kifo cha Abdillah Warsama (CCM), chama hicho kitatetea nafasi yake kwa kumsimamisha Godluck Lerunya na Chadema ni Japhet Sironga.

Mbali na Kata ya Makuyuni, uchaguzi wa udiwani mkoani Arusha utafanyika pia katika Kata za Kaloleni, Themi, Kimandolu na Elerai, kutokana na waliokuwa madiwani wa kata hizo (Chadema), kufukuzwa na chama chao.

"Mnaweza kuchafuana leo, kesho mkapata mgombea mwenye nundu nyingi na mabandeji kila mahala, halafu mkapata shida kumnadi," alisema.

Siyo mara ya kwanza kwa Kikwete kumsifia Lowassa kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka jana huko Longido wakati akikabidhi ng'ombe.

Pia aliwahi kumsifia wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 wakati Kikwete alipomwelezea Lowassa kama Mbunge makini na kuwaomba watu wa Monduli kumchagua tena.

Hata hivyo, alipoulizwa kama baada ya kuruhusiwa kuanza kujipitisha kwa wanaCCM kama anataka kuwania urais, Lowassa alijibu kupitia watu wake wa karibuni kuwa asingependa kuzungumzia suala hilo hasa baada ya Rais kutoa kauli hiyo.



Kutangaza nia ruksa

Rais Kikwete aliwaeleza wabunge hao kuwa si kosa kwa watu kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwamo urais mwaka 2015.

"Wabunge na mawaziri wenye nia ya kutangaza nia ya kugombea urais wawe huru, kwani hiyo ni haki yao, isipokuwa wafanye kwa wema bila kukivuruga chama na kuwagawa wanaCCM katika makundi. Sioni tatizo watu kujipitisha. Sisi sote hapa tulijipitisha. Lakini tufanye hivyo kistaarabu bila kuvurugana."

Aliwaagiza wabunge wa chama hicho kwenda majimboni mwao kusikiliza kero za wananchi badala ya kusubiri wakati wa uchaguzi.



Membe

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye naye anatajwa kuwa miongoni mwa wagombea amewataka waandishi waache kuandika kila siku habari za urais na badala yake waandike mambo ya maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kukutana na mabalozi wa nchi zinazoendelea kuhusu Mkutano wa Smart Partnership, unaotarajiwa kufanyika nchini, Membe alisema ni vizuri yakaandikwa mambo ya maendeleo na si kila wakati kuandika mambo ya urais.

"Mkutano kama huu nchi kama Kenya watauripoti vizuri na kwa undani hivyo mfanye hivyo si kila kitu urais 2015," alisema Membe. Mkutano huo utaanza Mei 28, hadi Juni Mosi na utajadili jinsi gani sayansi na teknolojia vinaweza kutumika kuzikwamua kiuchumi.

Imeandikwa na Kizitto Noya, Habel Chidawali na Boniface Meena.
 
Back
Top Bottom