Hii Nchi Kuna mambo yanatia hasira, yaani kweli muda mchache ulopita wananchi walikua wanahangaika na upatikanaji wa Sukari Kuna baadhi ya maeneo kilo ilifikia 10,000/=
Wenye viwanda wakapewa ruhusa ya kuingiza Sukari wakagoma, Serikali (waziri)ikapambana kwakutumia wafanya biashara mpaka Sasa Kuna unafuu kiasi.
Bado Kuna mtu (Mbunge) analalamika na kukusudia kwenda mahakamani kwakua utaratibu wa uagizaji haukufuatwa ivi inaingia akilini kweli!
Ayo yote Mbunge anayafanya kwa manufaa ya nani.
Yaani ameshasahau wakati akiwa waziri alikua akipima samaki wa ziwa Victoria kwa rula na kuchomea watu Nyavu, Mbona tuna sahau haraka?