Kichwa cha habari hakina uhusiano kabisa na kilichoandikwa ndani.Tujifunze uandishi mzuri sio ilimradi tu.
Hii inaonyesha namna kusambaza umeme vijijini inavyopaswa kuwa kipaumbele Cha kupambana na uharibifu wa mazingira. Umeme unachochea Kasi ya maendeleo ya kiuchumi, kielimu, kiafya, kijamii na kimazingira pia. Tuache kutumia hela kwenye sherehe, safari na misamaha ili tumalize kwanza kero za maji, umeme, elimu, na afya ambazo zimewaganda wanyonge kama fulana kwa miaka 60 Sasa hata baada ya Uhuru.
Miaka 60 bro ni mingi sana kwa watu kukosa umeme na maji. Miti mingi sana imepotea kwa kosa hili.
Tumeambiwa Kuna Kodi kwenye mafuta na miamala ya simu ili kumaliza shida hizi kwa Kasi, lakini sioni idadi ya vijiji vinavyopata umeme ikiongezeka kwa kasi, badala yake tunaona Kasi ya safari TU.
Tungesifiwa na kupigiwa makofi mengi sana na dunia nzima kwenye mikutano kama hii kama kiongozi wetu angesimama na kusema Tanzania katika kupambana na uharibifu wa mazingira Tanzania imefanya yafuatayo:
1. Imesambaza umeme vijiji vyote (100%) ili kuepusha miti kukatwa kwaajili ya kupata nishati.
2. Inajenga bwawa la umeme wa kutumia maji (hydro power) huko Rufiji na kusimika mitambo ya kuvfua umeme wa upepo huko singinda.
3. inasambaza maji nchi nzima ili kuepusha watu kuhamahama kutafuta maji ya malisho na majumbani.
4. Nimeshusha bei za umeme na saluji ili kupunguza idadi ya watu wanaojenga nyumba za miti.
5. Nimesambaza gesi yetu itumike majumbani, mashuleni, magerezani na majeshini badala ya kutumia mkaa na Kuni kupikia.
6. Tubabadilisha magari yooote madogo yatumie gesi badala ya mafuta ya diseli na petroli.
7. Tumepiga marufuku matumizi ya vifungaahio vya plastic nchi nzima.
8. Tumeshusha bei ya umeme na gesi ya kupikia ili kuepusha matumizi ya Kuni na mkaa.
9. Tumewapatia pembejeo za kilimo na ufugaji wananchi ili kuepuka kilimo na ufugaji wa kuhamahama.
10. Tumepanda miti hekta kadhaa kurudishia zile zilizoharibiwa na wananchi waliokuwa wakikata Kuni, mkaa, mijengo, kilimo na ufugaji wa kuhamahama.
Hotuba zetu kwenye mikutano zingekuwa kama hivi watu wote wangeduaa na kupiga makofi hadi mikono Yao ipate malengelenge. Lakini unaposema tunapanda miti mingi wakati huohuo wananchi wanakata miti mingi zaidi kuliko uliyopata kwaajili ya kupata mkaa, Kuni, jengo, kilimo na ufugaji wa kuhamahama na mwanga wa kumulikia watu wanakushangaa kwelikweli. Utadhani umeupiga mwingi lakini wanakucheka TU.
Unapanda miti 3 lakini hapohapo wananchi wamekata miti 33 kwa kuni, kuchoma mkaa, kujenga nyumba zao na kutafuta mashamba.