Kasi ya kupeleka umeme vijijini imepungua sana, kulikoni?

Kwani mkutano mmoja kama huu unatugharimu sh. ngapi? Labda tuanzie hapo. Hela hizo zingetosha kupanda miti mingapi inayoweza kunyonya gesi chafu?

Ndugu zangu we have to think globally and act locally, na sio to think locally and and act globally.
Correct
 
Makini sana brother
 
Kila nchi iupige mwingi hukohuko nyumbani kwake katika uihifadhi mazingira kabla ya kulaumu wengine. Sisi tunashindwa hata kuwapangia maeneo wamachinga wanaochafua mazingira. Tunapanda miti michache halafu watu wetu wanakata miti zaidi kutaka kuni, mkaa, na mijengo ya nyumba.
 
Ndiyo tatizo la viongozi wengi wa Africa
 

Tusishangae sababu kubwa ni kwamba baada ya kusambaza umeme kwa kasi umeme ulikuwa unapungu sana na kulianza migao!. Hivyo chinichini wanapunguza kasi ya usambazaji ili wapate muda wa kuongeza uzalishaji wa umeme. Umeme tulionao hautoshi!. P, note hii point nafikiri hii ndiyo sababu Pascal Mayalla
 
Mkuu Kamundu , umeniacha juani, ndio sababu ya nini?!.

P

Sababu ya kupunguza kasi ya usambazaji wa umeme vijijini. Yaani nafikiri serikali ilifanya usambazaji kwa kasi kuliko uzalishaji. Kilichotokea ni upungufu wa umeme na kuanza kwa mgao wa umeme kwa sehemu nyingine. Theory yangu ni kwamba kasi ya usambazaji umeme vijijini kupungua ni makusudi kuipa serikali muda wa kuongeza uzalishaji wa umeme kwa ujumla. Wakiendelea kusambaza kwa kasi umeme utaendelea kupungua kama capacity bado ni ndogo. Hii ni theory tu lakini sina uhakika
 
Kwahiyo wamesitisha pia tozo za umeme kwenye mafuta na miamala kwaajili ya umeme vijijini? Mbona hakuna feedback kwa wadau kuhusu sababu yako hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…