Serikali ya Awamu ya 5 inajitahidi sana kufanya miradi mikubwa ya kimkakati ndani ya muda mfupi kwa gharama kubwa.
Miradi hii inatosha sana kuiuza Serikali na CCM kwa wananchi kama wawakilishi wake wangekuwa wanamsaidia vizuri Rais kuitangaza na kuifafanua kwa wananchi
Miongoni mwa miradi hiyo, ni mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambayo inapita Morogoro. Fursa zake ni nyingi kwa wakazi wa mji huo uliopo katikati ya Dar es Salaam na Dodoma. Katikati ni kutamu
Cha ajabu, Mfanyabiashara Abdulazizi Abood ambaye ni Mbunge anayefahamika zaidi hapo Morogoro, ameshindwa kumsaidia Rais katika eneo hili.
Kwa maslahi ya chama na wananchi, Mbunge huyu ilibidi awe kinara wa kuzungumza bungeni kuhusu mradi huo ili wakazi wa jimbo lake lineemeke na fursa zilizopo. Kufanya hivyo kungekuwa na faida nyingi kwake, chama na kiongozi wake mkuu, Rais Magufuli.
Badala yake, mfanyabiashara huyu amekuwa bubu bungeni na jimboni. Wenzake wanahangaika, yeye hata wananchi wake hakutani nao. Hii inaleta taswira kuwa ni kiongozi mbinafsi na anautumia Ubunge au siasa kulinda maslahi ya biashara zake, sio kuhudumia wananchi.
Haya mambo kwa bahati mbaya hayaendani na falsafa za Magufuli. Yeye ashasema hataki mambo ya business as usual. Kasi yake inataka kila mmoja afanye anachofanya kwa maslahi ya wananchi kwanza.
Yapo madai kwamba, Abood amegeuka kuwa mfadhili wa viongozi wa chama na sio mbunge wa kupeleka matatizo ya wananchi Bungeni. Pia amekuwa akitoa misaada ya kilaghai pale linapozuka jambo jimboni.
Kama hayo ni kweli, ajiandae kustaafu siasa na jina lake kukatwa kwenye kura za maoni mwaka huu. Mzee Magufuli hatamuacha salama.