Unayafahamu majukumu na kazi za Mbunge lakini? Sidhani kama kigezo cha kuwa tajiri na kuajiri kama kipo. Nikupe tu pole, maana lolote linaweza kutokea.
Uombee tu siku hiyo ya uteuzi wa mgombea, Mwenyekiti aamke vizuri! au kati ya hao watia nia wa hilo Jimbo la Moro Mjini, asiwepo Mgombea mwenye shahada ya Uzamili au PhD! Akiwepo/wakiwepo, hakika jina la huyo Abood wako litakatwa na Mwenyekiti muda utakapowadia.
Hii awamu matajiri hasa wale wenye rangi kama ya huyo Abood, watapumulia mashine kwenye kinyang'anyiro cha ubunge maana Magufuli anawaogopa kama ukoma! kutokana na changamoto alizopitia kwenye uchaguzi uliopita.