Kasi ya ugonjwa wa kisukari yaongezeka nchini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Dk. Seif Rashidi


Serikali imesema ugonjwa wa kisukari umeenea kwa kati ya asilimia 0 hadi 20 katika wilaya 50 za Tanzania Bara.

Takwimu hizo zilitolewa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashidi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mgogoni, Kombo Khamis Kombo (CUF).

Mbunge huyo alitaka kujua kama serikali imefanya utafiti wa ugonjwa wa kisukari ambao unapoteza maisha ya wananchi wengi.

Pia, alihoji kama serikali imetoa elimu gani kwa wananchi ili kuepuka magonjwa nyemelezi yanayosababishwa na ugonjwa huo.

Dk. Rashidi alisema tafiti zilizofanyika miaka ya 1986/87 na baadaye mwaka 1996/97 katika mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mara na Mwanza, zilionyesha kuwa ugonjwa wa kisukari ulikuwa umeenea kwa asilimia moja vijijini na asilimia tatu jijini Dar es Salaam.

Alisema mwaka 2005, idadi hiyo ilikuwa imefikia asilimia tano kwa wakazi wa Dar es Salaam.

“Utafiti wa viashiria vya magonjwa yasiyoambuzika kwa nchi nzima umeonyesha kuwa ugonjwa wa kisukari umeenea kati ya asilimia 0 hadi 20 katika wilaya 50 za Tanzania Bara,” alisema.

Aidha, alisema matokeo ya utafiti huo yatasaidia kubuni mbinu za kudhibiti vichochezi vinavyosababisha ongezeko la ugonjwa huo na magonjwa yasiyoambuzikiza nchini.

Kuhusu kutoa elimu, alisema serikali inafahamu kuwa elimu ni kiungo muhimu katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu magonjwa mbalimbali.

“Elimu juu ya ugonjwa wa kisukari na elimu ya afya hutolewa kwenye hospitali mbalimbali na vituo vya kutolea huduma za afya nchini,” alisema




CHANZO: NIPASHE

 
Mfumo wa maisha tuishio, nao unachangia sana huu ugonjwa... @ MziziMkavu nasikia ukiwa na huu ugonjwa nguvu za kibaba huisha?
 
Last edited by a moderator:
Mfumo wa maisha tuishio, nao unachangia sana huu ugonjwa... @ MziziMkavu nasikia ukiwa na huu ugonjwa nguvu za kibaba huisha?
Mkuu manoah Ukiwa na ugonjwa wa kisukari unaishiwa nguvu za kiume itabidi unione mimi nikupe Dawa za kurudisha heshima yako ya kitandani. Ama sivyo Mtalimbo wako utalala doro.

Upungufu wa nguvu za kiume husababishwa na magonjwa ya moyo, kisukari, mafuta mengi mwilini (high cholesterol), uvutaji sigara, matumizi ya madawa ya kulevya, matatizo katika uhusiano, mawasiliano duni na mwenza wako, matatizo ya kisaikolojia, msongo wa mawazo, wasiwasi (anxiety),unywaji pombe,upungufu wa homoni aina ya testerone, kuongezeka uzito au uzito uliopitiliza, tabia ya kujichua kwa muda mrefu kupiga Punyeto (masturbation)
 
Last edited by a moderator:
Mfumo wa maisha tuishio, nao unachangia sana huu ugonjwa... @ MziziMkavu nasikia ukiwa na huu ugonjwa nguvu za kibaba huisha?
Mkuu manoah Ukiwa na ugonjwa wa kisukari unaishiwa nguvu za kiume itabidi unione mimi nikupe Dawa za kurudisha heshima yako ya kitandani. Ama sivyo Mtalimbo wako utalala doro.

Upungufu wa nguvu za kiume husababishwa na magonjwa ya moyo, kisukari, mafuta mengi mwilini (high cholesterol), uvutaji sigara, matumizi ya madawa ya kulevya, matatizo katika uhusiano, mawasiliano duni na mwenza wako, matatizo ya kisaikolojia, msongo wa mawazo, wasiwasi (anxiety),unywaji pombe,upungufu wa homoni aina ya testerone, kuongezeka uzito au uzito uliopitiliza, tabia ya kujichua kwa muda mrefu kupiga Punyeto (masturbation)
 
Last edited by a moderator:
duh! hili ni janga kubwa! je kwa wale mabinti wenye tatizo hili suala la kuzaa kwao likoje?
 
mh hii ni bad news nadhani inakuja na milo mibovu na ongezeko la obesity
 
Japokuwa kwa kiasi fulani takwimu hizo zinaweza kuwa zimekuzwa na ukweli kwamba watu wengi sasa wana ufahamu na wanakwenda kupima Kisukari, na pia vipimo vimekuwa vinapatikana sehemu mbali mbali...basi takwimu lazima zipande. Hata hivyo, huo ndio ukweli wenyewe..kuwa maisha tunayoishi sasa yanatuongezea hatari za kupata tatizo hili, tubadilikeni jamani..tujali tunachokula, na tuwe na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara.

Lingine ni watoto wetu...siku hizi yaani idadi ya watoto wenye vitambi ni kubwa hasa ukienda kwenye shule hizi za Saint nini sijui..watoto wa kike kwa wa kiume wamefura mafuta hatari, na wazazi wanachukulia kama jambo la kawaida tu, na wengine wanaona ni sifa kuwa watoto eti ndio wana afya...si kweli, si afya ile! Tunawaexpose watoto kwenye life style hatarishi tangu umri mdogo, ndio hawa wanakuja kuishia kuwa na kisukari na high blood pressure katika umri mdogo..and its not their fault, ni fault yetu sisi kama wazazi kuwabambikiza maisha hatarishi watoto wanakuja athirika baadae!
 
Basi nimekwisha sasa hayo yote nahisi yana ninyemelea.

 
Maji hukinga na kuponya ugonjwa wa kisukari:

Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.

kuna aina kuu mbili za kisukari:

  • Kisukari aina ya kwanza, ambapo Insulini inakuwa tegemezi (insulin-dependent); hapa kongosho halitengenezi kabisa insulini au linaitengeneza kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba mgonjwa analazimika kuchomwa sindano ya insulini au kutumia pampu za insulini.
  • Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo Insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.

Aina ya kwanza ya kisukari inaweza kutokea kwa watu kuanzia utotoni mpaka kwa watu wa umri wa miaka 30. Aina hii ya kisukari hushambulia kwa haraka sana, kwa kawaida ndani ya majuma mpaka miezi kadhaa. Kwakuwa kongosho halifanyi kazi vizuri, usawa wa damu sukari lazima upewe uangalizi wa karibu. Watu wenye kisukari aina hii ya kwanza pia huwa na uzito pungufu (underweight).

Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanya mazoezi au sababu za kurithi (genetics). Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunashuhudia hata watoto wadogo wakipatwa na aina hii ya kisukari. Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).

Baadhi ya dalili kuu za kisukari ni:

  • Kiu iliyozidi
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kupatwa na ganzi kwenye miguu na mikono
  • Kujisikia mchovu
  • Kutoona vizuri
  • Kuongezeka njaa
  • Kushindwa kuhimili tendo la ndoa

Ikiwa daktari atakuona una dalili za kuwa na kisukari, ata kutaka ufanye jaribio la kuiandaa glukozi katika usawa wake wa chini kabisa kwenye damu (fasting plasma glucose test – fpgt), kwa sababu hiyo, atakutaka ubaki bila kula kitu chochote kwa muda usiopungua masaa nane kabla ya kukupima, ambapo kwa kawaida huwa ni asubuhi ili kupata uwezekano wa damu sukari kuwa katika usawa wake wa chini kabisa.

Kisha atachukua damu toka kwenye mkono na kuipima na kulinganisha matokeo na uwiano ufuatao:

  • Chini ya 99 mg/dl ni kawaida
  • 100 – 125 mg/dl ni hatua za mwanzo za kisukari
  • Zaidi ya 126 mg/dl ni kisukari.

Kisukari ambacho hakikudhibitiwa kinaweza kusababisha mwili kulazimika kuanza kuchoma mafuta ili kuzarisha nishati/nguvu (diabetic ketoacidosis), hii kwa kawaida hutokea kwa watu wenye kisukari cha aina ya kwanza ambapo glukozi inaweza kuingia kwenye seli bila insulini.

Kitendo cha mafuta kutumika kuzarisha nishati huzarisha taka nyingi za asidi zilijulikanazo kwa kitaalamu kama 'Ketones'.
Taka hizi (Diabetic ketoacidosis – DKA) hujijenga kwenye mzunguko wa damu na kusababisha pumzi fupi, mauzauza na kutapika na mwishowe kukuwekea koma na hata kusababisha kifo.

DKA haijitokezi sana siku hizi ahsante kwa insulini na vifaa rahisi kutumia kufuatilia damu sukari.

Wakati damu sukari inapokuwa nyingi na damu inapokuwa imetulia, nene na hafifu (hyperosmolar syndrome), husababisha kukojoa mara nyingi ili kuilazimisha sukari iliyozidi kutoka nje. Ikitokea hivyo, utapatwa na upungufu mkubwa wa maji na unaweza kushikwa na mikakamao ya miguu, mapigo ya moyo kwenda mbio, mauzauza, msukosuko, au hata kuelekea kwenye koma. Hii huwatokea watu wenye kisukari aina ya pili ambao hawafuatilii kujuwa kiasi cha damu sukari yao mwilini.

Moja kati ya matatizo makubwa ya kisukari ni kitendo cha kushuka kwa kiasi kikubwa cha damu sukari mwilini (hypoglycemia), hii hutokea wakati damu sukari inazarishwa kidogo kutokana na kutumia kiasi kingi cha insulini au kukaa muda mrefu bila kula chochote na huku ukiwa umetumia insulini au ulinusa harufu ya chakula fulani.

Zifuatazo ni dalili za kushuka kwa damu sukari mwilini:

  • Kichwa kuuma
  • Mauzauza
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio
  • Kutokwa na jasho jingi
  • Kuona vitu viwili katika kimoja.
  • Ikiwa damu sukari itashuka kufikia usawa wa 50 – 70 mg/dl, unaweza kujisikia kuwa na hali zifuatazo:
  • Kuishiwa nguvu
  • Kusinzia na kizunguzungu
  • Kuona nukta nukta kabla ya macho yako
  • Mwili unaweza kuwa kama uliopooza.

Wakati damu sukari imeshuka kufikia 30 – 45 mg/dl, unaweza kwenda kwenye koma (deep sleep) na kufa ikiwa hautapewa sukari ya haraka kama inayopatikana kwenye juisi ya chungwa (ambayo huitwa muokoaji kwenye uwanja wa madawa), sukari halisi au peremende ya sukari ili kupandisha kiwango cha damu sukari mwilini.

Namna moja ambayo kisukari kinaweza kujipenyeza taratibu kwenye miili ya watu, ni pale insulini inapofanya ukaidi bila wao kujua, ukaidi huu wa insulini ukitokea, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kupatwa na kisukari wakati fulani katika safari yako ya kuishi.
Ukaidi wa insulini (insulin resistance) ni wakati ambapo mwili unazarisha insulini lakini hauitumii ipasavyo.

Insulini ni homoni inayotengenezwa na kongosho ili kuusaidia mwili kuitumia glukozi kwa ajili ya kuzarisha nishati. Glukozi ni aina ya sukari ambayo ni chanzo kikuu cha nishati ya mwili.

Mfumo wa umeng'enyaji wa chakula, hukimeng'enya chakula na kuwa glukozi ambayo kisha husafiri kwenye mkondo wa damu mwili mzima. Glukozi inapokuwa kwenye damu huitwa damu glukozi, pia hujulikana kama damu sukari. Wakati damu sukari inapopanda juu baada ya kula, kongosho huitoa insulini ili kuziwezesha seli za mwili wako kuitumia glukozi.

Mtu anapokuwa katika hali ya ukaidi wa insulini, mishipa, mafuta na Ini lake vinakuwa haviitiki vema kwa insulini, kwa sababu hii, mwili wake utaihitaji insulini zaidi ili kuiwezesha glukozi kuziingia seli.

Kongosho litajaribu kukidhi ongezeko la uhitaji huo wa insulini kwa kuizarisha insulini nyingi zaidi. Hatimaye kongosho nalo halitaweza kuendelea kumudu kuzarisha kiasi hicho kingi cha insulini. Insulini na Glukozi iliyozidi, vitajijenga ndani ya mkondo wa damu vikiandaa ngazi kuelekea kisukari.

Katika kitabu cha dr.Batmanghelidj kiitwacho ‘Your Bodies Many Cries For Water' anasema ikiwa mwili una kiasi kidogo cha maji na chumvi, ubongo utakuwa unajiendesha kwa karibu ya aslilimia 100 kwa kutumia sukari.

Ubongo pia utapandisha juu kiwango cha sukari kwenye damu ili kuuwezesha kufanya kazi zake vizuri. Cha kushangaza ni kuwa, mwili unaihitaji insulini ili kuuwezesha kuitumia sukari kama chanzo cha nishati, lakini kamwe ubongo hauihitaji insulini ili kuupelekea mahitaji yake ya nishati.

Katika kisukari, ubongo unajipa moyo wenyewe kama vile daktari ampavyo moyo muathirika wa kisukari kwa kutumia dripu zenye sukari na chumvi (intravenous fluid treatment).

Watu wengi wenye kisukari huwa hawaelewi ni kwanini wanakuwa na damu sukari nyingi wakati waamkapo asubuhi ikiwa hawakula kitu chochote kabla ya kwenda kulala. Sababu ni kuwa, usiku unapokuwa umelala, mwili hufanya kazi kwa bidii kujiripea wenyewe, katika kufanya hivyo, mwili hutumia sukari. Kwakuwa haukula chochote kabla ya kwenda kulala, mwili lazima ujile wenyewe (cannibalize off itself) ili kuliwezesha Ini kutengeneza sukari kwa ajili ya nishati.

Ubongo, ambao ni kituo kikuu cha udhibiti wa kazi zote za mwili, utagunduwa kuwa hakuna kiasi cha kutosha cha sukari kwenye damu kwa ajili ya matumizi yake, na kwa sababu hiyo utaliamuru ini kutoa mara mbili mpaka tatu ya kiasi cha sukari ikiwa damu itaihitaji. Hii ndiyo sababu ya kupanda kwa kiwango cha sukari asubuhi kama hukula chochote kabla ya kwenda kulala.

Inashauriwa kwa watu wenye kisukari kula gramu 25 mpaka 30 za maharage machanga ya kijani kibichi au njegere (green beans), siagi halisi na chumvi dakika 15 kabla ya kwenda kulala, hii itasaidia kushusha damu sukari waamkapo asubuhi. Maharage haya yana kiasi kidogo cha wanga (carbs), na kiasi kingi cha protini, magnesiamu na asidi amino iitwayo ‘tryptophan' ili kuubeba mwili usiku mzima.

Katika kuepuka sukari, baadhi ya watu wenye kisukari huamua kutumia viongeza sukari visivyo vya asili (artificial sweeteners). Unapoweka sukari ya kutengenezwa ulimini, ulimi utauambia ubongo kuwa sukari inakaribia kuja, ubongo utaliambia Ini liache kuendelea kutengeneza sukari bali liihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye na lijiandae kuishughurikia sukari iliyopo njiani kuja.
Ubongo upo makini sana (very smart), baada ya muda utagundua kuwa hakuna sukari iliyoliwa bali ulilaghaiwa. Dakika hii mzunguko wa damu unakuwa katika udharura wa uhitaji wa sukari.

Fikiri:
Kila siku unaenda dukani kununua sembe kilo moja. Siku moja unafika dukani mwenye duka anakuambia sembe limebaki kilo tatu na hajuwi lini atapata mzigo mwingine. utafanya nini?. Utafanya kila uwezalo uzichukuwe hizo kilo tatu zilizopo kama tahadhari kesho usishinde bila kula.

Ndicho kinachotokea mwilini. Ubongo ukishagunduwa kuwa iliyoliwa haikuwa sukari na ulishaliamuru Ini kupumzika kuitengeneza sukari kwenye mzunguko, utaliamuru Ini kuipatia damu mara mbili mpaka tatu ya kiasi cha sukari zaidi ya inavyohitajika!. Sasa unapoenda kupima kiasi cha damu sukari, unajikuta huelewi nini cha kufanya kwa sababu kipo juu mno. Na sasa lazima uchomwe insulini ili kuishusha damu sukari.

Dr.Batman, anasema; ‘kwa sehemu kubwa, kisukari ni matokeo ya kukosa maji, chumvi, magnesiamu, asidi amino (tryptophan) ipatikanayo kwenye mayai, maharage, vyakula jamii ya karanga na jibini, vitamini B6, zinki na mazoezi'.
Unapokuwa katika upungufu wa maji (haunywi ya kutosha) na unakula vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, ‘automatikali' ubongo utapandisha kiwango cha sukari kwenye damu yako.

Jinsi ya kutumia maji kujitibu kisukari
 
Hili ni janga la Taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua za dharuara, vinginevyo Taifa litakula HASARA. Kama alivyosema Mkuu RIWA, watoto wetu siku hizi wanazidi kufura. Hakuna mazoezi hakuna mlo kamili. Wakitoka mashuleni wanafikia kwenye T.V na Internet. Nawaonea huruma kwa kweli. ile system ya zamani kwamba mtoto/watoto ndio watakaowazika wazazi wao imeanza kuingia walakini. Siku hizi wazazi ndio wanaozika watoto wao. Hii ni kasheshe. Nchi inahitaji health care policy haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…