GE2025 Kasimu Matimbwa amejitokeza rasmi kuomba ridhaa kuwania ubunge wa Jimbo la Morogoro Kusini

GE2025 Kasimu Matimbwa amejitokeza rasmi kuomba ridhaa kuwania ubunge wa Jimbo la Morogoro Kusini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kasimu Matimbwa, mtaalamu wa maji na mchambuzi wa miamba (Hydrogeologist), amejitokeza rasmi kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Morogoro Kusini katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akiwa na umri wa miaka 33, Matimbwa ni miongoni mwa wagombea vijana waliojitokeza kuwania nafasi hiyo. Amekuwa na uzoefu mkubwa katika utafiti wa maji chini ya ardhi na uchimbaji wa visima maeneo mbalimbali nchini.

Amechukua fomu hiyo katika ofisi za CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini, na kukabidhiwa na Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Michael Charles Bundala.
1751286474505.jpeg
 
Back
Top Bottom