Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Misamiati:
Baraza: Wilaya
Wadi - Kata
Mkoa wa Kaskazini Unguja ni mmoja kati ta mikoa 31 ya Tanzania ambayo unapatikana Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja huko Visiwani Zanzibar.
Kulingana na Sensa ya mwaka 2022, mkoa huu una jumla ya wakazi 257,290 kati ya hao wanaume ni 126,341 na wanawake ni 130,949 huku kaya zikiwa takriban 54, 810. Mkoa wa Kaskazini Unguja una jumla ya Majimbo 8, Baraza (Wilaya) 8 na Wadi (Kata) 10.
Majimbo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja;
- Nungwi
- Kijini
- Mkwajuni
- Chaani
- Tumbatu
- Donge
- Mahonda
- Bumbwini
Katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, ushindi ulitawaliwa zaidi na chama cha CCM katika majimbo mbalimbali. Katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, CCM kilishinda kwa zaidi ya asilimia 90% ya kura katika majimbo mengi kama Bumbwini, Mkwajuni, Chaani, Donge, Kijini, na Mahonda, ikiendelea kuwa na nguvu kubwa katika siasa za mkoa huo.
ACT-Wazalendo pia ilipata ushindi katika majimbo kadhaa kama Nungwi na Tumbatu, ikiweka alama muhimu kwa zaidi ya asilimia 79% ya kura kwenye baadhi ya majimbo. Hivyo, CCM kiliibuka na ushindi mkubwa, kikidhibiti sehemu kubwa ya mkoa, huku ACT-Wazalendo ikijitokeza kama mpinzani mkuu kwenye maeneo machache.
Aidha kuna vitendo vya kiukwaji wa haki za binadamu viripotiwa katika mkoa huo wakati wa Uchaguzi wa mwaka 20. Mtandao wa Human Rights Watch iliripoti kuwa Serikali ilipiga marufuku wanahabari kuchukua picha za majeshi ya ulinzi yalipokuwa yakiingia kwenye vituo vya kupigia kura.
Polisi waliwakamata na kuwashikilia wanahabari watatu waliokuwa wakiripoti juu ya maandamano ya upinzani. Wanahabari hao walizuiliwa kwa takriban saa moja mnamo Oktoba 29, katika jiji la Zanzibar, Unguja.
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Januari
Februari