SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Pamoja na wazo jema la ujenzi wa uwanja wa KMC Complex, naomba nijikite kutoa kasoro kadhaa nilizoziona katika mradi huu.
Kasoro zangu zitajikita katika maeneo yafuatayo:
1. Design
2. Gharama za matumizi
3. Ufinyu wa nafasi
SEHEMU YA 1: DESIGN
Ukiangalia design ya ujenzi wa uwanja huo umekaa zaidi kama uwanja wa mazoezi kuliko uwanja wa mashindano. Hapa nitatolea mfano uzio mrefu uliojengwa kutenganisha sehemu ya kuchezea na mashabiki.
Ule uzio unaondoa ladha ya kuangalia mechi maana unalazimika kuangalia mpira kupitia kwenye zile nyavu. Hii hitilafu niliiona pia uwanja mpya wa Amaan ingawa level zinazoathirika kwenye uwanja ule ni chache za chini.
Kama ilishindikana kuweka majukwaa yaliyo juu maana ingehitaji kuweka platform ya cement, ilitakiwa kuwa na uzio mfupi halafu watumiaji wa uwanja watakiwe kuweka wahudumu kuzunguka uwanja kudhibiti mashabiki. Hii ingesaidia kuepuka hii adha.
Kasoro nyingine katika design ni kushindwa kuweka viti vya plastiki vya mtu mmoja mmoja na kuamua kuweka mabenchi. Pamoja na kwamba mabenchi yanadumu zaidi ila hii imekuja na changamoto zake.
Kwanza ni kushindwa kucontrol uingiaji wa mashabiki maana hata kama unaweza kukadiria watu watakaaje kwenye mabenchi, waswahili tunajua tunavyoweza kujibana. Hii inaondoa comfortability na burudani uliyoilipia na kuifuata.
Tungefanya mambo kisomi, tungeweka viti vya plastiki halafu hii gharama ingewekwa katika malipo ya matumizi ya uwanja. Yaani, unasema kwa mfano kila kiti kimegharimu 50,000 kukiweka. Basi katika bei za tiketi, kuna shilingi 500 inawekwa kama rejesho la gharama za kuweka kila viti. Utaona haifiki mwaka gharama za hivyo viti inakuwa imesharudi na viti standard vinaweza kukaa si chini ya miaka 5 kabla ya kuanza kuchakaa na kuharibika.
Sehemu ya 2 na 3 zinafuata...