Kassim Majaliwa: Atamaliza, tutamuongezea miaka mitano mingine kwa utamaduni wa chama cha Mapinduzi

Kassim Majaliwa: Atamaliza, tutamuongezea miaka mitano mingine kwa utamaduni wa chama cha Mapinduzi

Anajua na yeye bata la uwaziri mkuu kwa miaka 10 zaidi .

Hapo anajiongelea
Hahaha, ni kweli mzee! Watu wanajua kujiposition, maana hajui akiingia mtu mpya atakuja na mikato ipi!! Hataki kimtokee kilichowatokea akina Bashiru, Polepole, Kalemani, Dotto James na wengineo...!
 
Huyu mwalimu hesabu zinampiga chenga, Samia hata akipata awamu mbili bado atakuwa rais kwa miaka 9 na miezi kadhaa.

Na kwa mwenendo wake huu wa kurudisha majambazi na wanamtandao wapiga dili serikalini, niwawashangaa 'wazalendo' wetu uchwara kama wataruhusu aendelee past 2025.
Nimachounga mkono kuwa aendelee ni kikundi hiki kinachojipanga dhidi yake ambacho sina imani nacho hata kidogo. Hivyo naunga mkono hoja ya PM 100% Mama aendelee.
 
Nimachounga mkono kuwa aendelee ni kikundi hiki kinachojipanga dhidi yake ambacho sina imani nacho hata kidogo. Hivyo naunga mkono hoja ya PM 100% Mama aendelee.
Sidhani Kama atakuwa Pm Tena labda uslamu Umbebe
 
Hata akiwa rais after 2025 election, Hawezi kuwa rais kwa miaka 10, Maximum atakaa miaka 9 tu

Kassim Majaliwa asitake kujipendekeza kwa Samia
 
Hata akiwa rais after 2025 election, Hawezi kuwa rais kwa miaka 10, Maximum atakaa miaka 9 tu

Kassim Majaliwa asitake kujipendekeza kwa Samia
We sema kwa utaratibu anatakiwa akae miaka 9 sio uongee kama vile maamuzi ni ya kwako. Inaweza pigwa U-turn usiamini kinachotokea, na jeshi likishakuwa upande wake hakuna wa kuleta fonyo fonyo.
 
Huyu naye anaogopa kutumbuliwa
sio anaogopa kutumbuliwa. Anampaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili Mama ajipweteke kuona anakubalika. Ila dakika za mwisho watamgeuka vibaya bibi wa watu mpaka asijue kilichomkuta. Mama hajui tu ila maadui zake wakubwa ni hao hao wanaosadikika kuwa wasaidizi wake.
 
Majaliwa anataka Kutuambia Iwe isiwe lazima Samia awe Rais Wa Nchi Kwa Miaka 10 ijayo?

===========

Kassim Majaliwa: Nataka kuwahakikishia tena, Serikali yenu iko makini na maam yetu kwenye eneo hili anaendelea kutenda haki. Leo miezi sita tu, ana miaka mitano tutamjumlishia miaka mitano mingine, bado ana nafasi ya kufanya sana. Hii miaka mitano anayokwanda nayo, sasa hivi bado tunafahamishana fahamishana tu lazima kila mtu ajue filosofi ya mama ni nini!

Atamaliza, tutamuongezea miaka mitano mingine

View attachment 1954361

Luka 12:16-21​

Kisha akawaambia mfano: “Kulikuwa na tajiri mmoja ambaye shamba lake lilizaa mavuno mengi. Tajiri huyo akafikiri moyoni mwake: ‘Nitafanyaje nami sina mahali pa kuhifadhia mavuno yangu? Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu na kujenga kubwa zaidi, nami nitahifadhi humo mavuno yangu yote na mali yangu. Hapo nitaweza kuiambia roho yangu: Sasa unayo akiba ya matumizi kwa miaka na miaka. Ponda mali, kula, kunywa na kufurahi.’ Lakini Mungu akamwambia: ‘Mpumbavu wewe; leo usiku roho yako itachukuliwa. Na vitu vile vyote ulivyojirundikia vitakuwa vya nani?’” Yesu akamaliza kwa kusema, “Ndivyo ilivyo kwa mtu anayejirundikia mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu.”
 
Kwahizi kauli za kila siku ni kama wanapigana vijembe wenyewe CCM, kuna kitu kinaendelea ndani ya CCM maana hii haiwahusu wapinzani Mama kikatiba ana haki ya kugombania kiti tena hakuna shida. Ndani ya CCM kuna shida na tamaduni za CCM mambo yao huwa hawaweki hadharani lakini safari hii mbio za mwaka 2025 zimeanza 2021. Kwanini CCM haifanyi yake kama kuna watu wanaleta chokochoko wasishughulikiwe ndani ya Chama kwenye vikao vyao badala ya kupiga kelele huku nje.
 
Itakuwa CCM kumeanza kufukuta,
Da Sami waachie zigo lao haaaaooooh.
 
Back
Top Bottom