#COVID19 Kassim Majaliwa: Hakuna mtu aliyelazimishwa kuchanja chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Kassim Majaliwa: Hakuna mtu aliyelazimishwa kuchanja chanjo ya UVIKO-19

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
WAZIRI MKUU WA TANZANIA, NDUGU. KASSIM MAJALIWA: HAKUNA MTU ALIYELAZIMISHWA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO 19.
Awataka wananchi wapuuze upotoshwaji unaoendelea mitandaoni

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haijamlazimisha na wala haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19, hivyo amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

"Hakuna aliyelazimishwa kuchanja chanjo hiyo na wala hakuna mahali palipoandikwa kwamba lazima wananchi wachanjwe. Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 27, 2021) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nandagala ambapo amewasisitiza waendelee kuchukua tahadhari na kujikinga na UVIKO 19.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imeleta chanjo hiyo ili kutoa fursa kwa Watanzania watakaohitaji kuchanjwa kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 waweze kuipata kwa ukaribu na urahisi zaidi na si vinginevyo.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewasisitiza Watanzania waendeleze tabia ya kunawa mikono mara kwa mara na maji safi yanayotiririka na sabuni, watumie vitakasa mikono pamoja na kuvaa barakoa zilizothibitishwa na mamlaka husika.

Mbali na maelekezo hayo, Pia Waziri Mkuu amesema ni vema kwa sasa wananchi wakajiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima na inapolazimu basi wazingatie kukaa umbali wa mita moja au zaidi kutoka mtu mmoja hadi mwingine lengo likiwa ni kujikinga na UVIKO 19.

Mheshimiwa Majaliwa amesema wananchi wanatakiwa wafanye mazoezi ya mara kwa mara kulingana na afya zao pamoja na mazingira yanayowazunguka, pia amewasihi wazingatie lishe bora.

E6_VUyBX0AA4Get.jpg
 
Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi katika janga hili kulitokomeza hapa nchini na duniani kote.
 
Hao wananchi aliokuwa anazungumza nao walikusanyika au hawakukusanyika?

Mikusanyiko isiyo ya lazima imekatazwa,yeye kwa nini kawakusanya hao wana Nandagala?

Hii sio "uchochezi wa maambukizi"!?
 
Back
Top Bottom