Pre GE2025 Kassim Majaliwa: Tujiulize kwanini matukio ya uuaji na utekaji yanatokea karibu na uchaguzi

Pre GE2025 Kassim Majaliwa: Tujiulize kwanini matukio ya uuaji na utekaji yanatokea karibu na uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania badala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji, ni vema wakajiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.

Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumatatu Septemba 16, 2024 katika Baraza la Maulid lililofanyika kitaifa mkoani Geita.

Majaliwa amesema tangu awamu ya tatu, nne, tano na sasa awamu ya sita, matukio ya aina hiyo yamekuwa yakitokea hususan kipindi cha kukaribia uchaguzi na kwamba jamii inapaswa kujitafakari na kujiuliza kwanini matukio hayo hutokea kwenye kipindi kama hicho.

“Rais alitoa karipio juu ya yanayotokea, matukio haya yanatokea kila kipindi fulani, lazima tujiulize kwanini yanajitokeza hasa inapokaribia uchaguzi. Nani anafanya, ni rahisi kusema polisi, ni muhimu tukatafakari kwanini wakati huu na nani anafanya” amesema Majaliwa.

Majaliwa amesema Jeshi la Polisi pekee haliwezi kulilinda Taifa, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda usalama wa nchi na kusema Serikali itaendelea kuhamasisha wanachi kulilinda Taifa na kuifanya nchi kuwa imara kwa kutambua viashiria vya matukio yanayovunja amani na utulivu.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa majibu ya matukio ya kupotea na utekaji watu yanaendelea Nchini

Serikali ambaye hata viongozi hawajui kazi zao na wajibu wao. Je huyu chawa ana mlalamikia nani
 
Alitekwa na nani,na kwa nini atekwe yeye tu!?

..Mzee Ally Kibao alitia nia kugombea ubunge jimbo la Handeni kwa tiketi ya Cuf.

..siku ya kurudisha fomu akatekwa, akaja kupatikana akiwa amepigwa, na mchakato wa kurudisha fomu umepita.

..serikali huwa haifanyi uchunguzi kwa matukio yanayohusu wapinzani. Waliomteka wakati huo bado hawajakamatwa.
 
Nchi ya hovyo sana hii, Jeshi la polisi linaweza kufanya kazi yake na serikali inalisifia ikifika kwenye kupiga wananchi wasio na hatia.

Ila inapokuja kwenye majukumu yao halisi ya kulinda usalama wa raia, inaonekana jeshi hilo hilo haliwezi kufanya hivyo peke yake.

Kwa tafsiri ya haraka jeshi la polisi Tanzania ni weak au linatumika vibaya na serikali.
 
Tujiulize akina nani?!! Yaani kauli anatoa yeye kama raia au waziri mkuu?!! No wonder he is to most inefficient primers this country has ever had
 
Back
Top Bottom