Kassim Majaliwa: Ujenzi Bwawa la Nyerere unaendelea kwa kasi

Nipo huku Ila kwa jinsi ujenzi unavyoendelea ingawa Mimi si mhandisi Ila ngoma bado mbichi, ningetupia kapicha Ila naogopa kujiingiza matatizoni
Atleast Geza Ulole huwa anakuwa na data za mambo haya..

Kaka leta taarifa na picha pia.
 
Nilimsikiliza Muhongo dalali wa gesi yetu na moja kati ya watu walioigawa gesi yetu bure akiuponda huu mradi nikasema ndio maana tupo nyuma kimaendeleo kama tuliongozwa na watu wa namna ile
Muhongo fala sana yule jamaa
 
Wazari mkuu tunamuamini sanaa, karudishiwa nafasi yake kwa sababu kaaminiwa. kudanganya kifo hayo mambo yapo katika jamii zetu.
kuna watu wengi ,wazazi , mabibi mababu watoto wao wamefariki hawajaambiwa wala kupewa taarifa ya kifo.
 
Wazari mkuu tunamuamini sanaa, karudishiwa nafasi yake kwa sababu kaaminiwa. kudanganya kifo hayo mambo yapo katika jamii zetu.
kuna watu wengi ,wazazi , mabibi mababu watoto wao wamefariki hawajaambiwa wala kupewa taarifa ya kifo.
Kabisa
 
Ni ngumu sana wewe kuaminika kwa sasa maana ni muongo uliyekubuhu. PM hata useme saiz kumekucha lazma nihakiki. Yaani huwenda hata bwawa labda halipo limesombwa na mafuriko yalizidi kipimo ila ww unatuzuga ujenz unaendelea. Za kuambiwa na Majaliwa changanya na zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 

JPM ametuachia matahira,akili za mashabiki wake zimejaa mavi.
 
Kwa uongo aliotoa huyu mzee angekua nchi nyingine angekua hana kazi ila Tanzania kuna watu wanamuona mtu mwenye hekima mchapakazi.
Mzee ovyo tu amejaa ego na anatumia dini kudanganya watanzania.
 
Mtajinyonga
 
wewe ni nani hasa ambae unaongelea watanzania wote? kwaninin usijiongelee wewe binafsi ? nani kakuambia watanzania turiridhika ?
enzi za kujitoa akili zimeisha anza kutumia ubongo sasa.
 
Serikali ya Tanzania itaendelea kugharimia ujenzi wa mradi wa Bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere, ili uweze kukamilika kwa wakati, yaani Juni 2022.

ULIMWENGU

Tanzania: Mradi wa Umeme wa Mto Rufiji Kukamilika kwa Wakati 2022

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa fedha za kugharamia ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115), ili ukamilike kwa wakati. Ameyasema hayo Jumamosi Aprili 10, 2021 baada ya kukagua mwenendo wa mradi huo unaotarajiwa kukamilika Juni 2022. Ubora na wakati ni muhimu

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, -Rufiji.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa fedha za kugharamia ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115), ili ukamilike kwa wakati. Ameyasema hayo Jumamosi Aprili 10, 2021 baada ya kukagua mwenendo wa mradi huo unaotarajiwa kukamilika Juni 2022. Amesema kuwa Serikali itahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili. Waziri Mkuu amesema amefarijika kuona kazi nzuri yenye viwango na ubora wa hali ya juu inayofanywa na Kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy Electric zote kutoka nchini Misri chini ya usimamizi wa TANESCO, TANROADS na Wizara ya Nishati.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kukamilika kwa mradi huo kutawawezesha Watanzania kupata umeme mwingi na wa gharama nafuu ambao utasambazwa nchini kote na ziada kuuzwa nje ya nchi ili kulipatia Taifa fedha za kigeni. Waziri Mkuu amesema bwawa hilo linatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 ambazo zikijumlishwa na megawati 1,500 zinazozalishwa na vyanzo mbalimbali nchini hivi sasa zitaifanya Tanzania kuwa na umeme utakaotosheleza mahitaji yake na ziada kuuzwa kwa majirani. ”Lengo la kuanzisha mradi huu ni moja ya juhudi za Serikali za kupunguza gharama za umeme kwa wananchi kwa sababu uzalishaji wake ni wa gharama nafuu ukilinganisha na vyanzo vingine. Uniti moja ya umeme unaozalishwa kwa kutumia maji inagharimu shilingi 36 hadi shilingi 50 huku umeme unaotumia vyanzo vya mafuta uniti moja inazalishwa kwa gharama ya shilingi 440 hadi shilingi 600.”

Amesema faida nyingine ya ujenzi wa mradi huo ni pamoja na kuzalisha ajira kwa Watanzania mbalimbali wanaoshiriki katika kuujenga na kutoa huduma mbalimbali kama wauzaji wa vifaa vya ujenzi, mafuta, vyakula na huduma nyingine zinazohitajika kwenye mradi huo. Waziri Mkuu amesema tayari TANESCO imeshatangaza zabuni ya ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme kutoka kwenye chanzo cha mradi huo hadi Chalinze mkoani Pwani na ukifika Chalinze njia moja itakwenda Dar es Salaam na nyingine Dodoma ili kuwezesha umeme huo kusambazwa nchi nzima. Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Nishati ifuatilie changamoto zote zinazoweza kukwamisha ujenzi wa mradi huo ili kuzipatia ufumbuzi na ihakikishe unakamilika kwa wakati. Pia amewataka wananchi wanaozunguka mradi huo kutoa ushirikiano kwa wajenzi kwa kuwahakikishia usalama wao, mali zao na vifaa vinavyotumika katika ujenzi huo.

Mapema, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameishukuru Serikali kwa kuwa wakati wote tangu kuanza kwa mradi huo hadi sasa imeendelea kutoa fedha za kugharamia mradi huo kwa wakati na tayari imeshatoa zaidi ya shilingi trilioni mbili. Hadi kukamilika mradi huo utagharimu shilingi trilioni 6.5. Mradi huo ambao unajengwa kwa fedha za ndani upo katika eneo la Selous linalotajwa kuwa moja ya maeneo ya urithi wa dunia, ambapo Tanzania inakusudia kupata umeme wa kutosha kupitia mradi huo. Ingawa mataifa ya kigeni yalionya kuhusu uharibifu wa mazingira katika eneo hilo.

Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa mradi huu alisema kwa msisitizo kwamba, Tanzania ni taifa huru lenye uwezo wa kujiamulia mambo yake hata kama mambo hayo yatawachukiza wengine: "Natambua kuwa pamekuwepo na maneno, kuwa mradi huu utaharibu mazingira lakini kiukweli mradi huu unayajenga mazingira. Upinzani huo ulianza mara tu tulipotangaza kuanza kutekeleza mradi huu mwezi Juni 2017. Hata hivyo kwa kuwa nchi yetu ni huru na sio maskini, narudia nchi yetu huru na wala siyo maskini kama baadhi ya watu wanavyodhani. Tuliamua ni lazima tuutekeleze mradi huu, sisi hakuna mtu wa kutufundisha katika suala hili Tanzania. Tanzania ni kinara katika kuhifadhi mazingira", alisema Rais Magufuli wakati akizindua mradi huo, sasa apumzike kwenye usingizi wa amani!

My take:Hii nchi tunaishi kwa kudanganywa tu sijui kwanini PM hupenda kusema uwongo kila mara!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…