Kassim Majaliwa: Wanaorekodi Matukio ya Ukatili na kuyarusha Mtandaoni waache

Kassim Majaliwa: Wanaorekodi Matukio ya Ukatili na kuyarusha Mtandaoni waache

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo, Februari 2, 2023 kwenye Mkutano wa 10, Kikao cha 3



WAZIRI MKUU: WANAOREKODI MATUKIO NA KUYARUSHA MITANDAONI WAACHE
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema “Nitoe wito kwa jamii hasa wale wanaonasa matukio na kuyarusha kwenye mitandao kutofanya hivyo kwa kuwa yanajenga chuki na taswira hasi kwa walimu wote badala ya wahusika wachache

Ameongeza “Matukio yanapojitokeza taarifa zitumwe kwa mamlaka husika ili hatua zichukuliwe badala ya kuleta taaruki kwa jamii. Naomba nieleweke kuwa lengo si kuficha taarifa bali kuzuia taharuki na uhasama, hii pia si kwa Walimu tu bali kwa vyombo vyote.”

KUHUSU SUALA LA KUPUNGUZA AU KUONDOA VIBOKO SHULENI
Waziri Mkuu ushauri wa kupunguza adhabu ya viboko kutoka nne kuwa kimoja amesema kwa kuwa suala hilo ni muongozo na kanuni kutoka Wizara ya Elimu, suala hilo litaangaliwa
Akijibu swali Bungeni amesema “Serikali ipo tayari kusikiliza maoni ya Wadau, watahusishwa, tutaangalia mwenendo wa nidhamu, wakati ukiruhusu kupunguza kiboko kuwa kimoja au kuondoa kabisa litaangaliwa.”

SPIKA WA BUNGE: WANAOTOA TAARIFA ZA UKATILI WALINDWE
Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema isingekuwa rahisi kufahamu matukio hasi yanayoripotiwa mitandaoni kama watu wasingerekodi na kuyasambaza

Amesema “Tunataka kupata taarifa nzuri na mbaya ili tuchukue hatua, mtoa taarifa ikiwa hajakosea sheria zetu namna ya kuzituma kwa mamlaka basi alindwe ili tuendelee kuzipata hizo taarifa, kama haitakuwa hivyo hatutaweza kuzipata hizo na matokeo yake ukatili utaendelea.”

Ameongeza “Matukio ya ukatili yanatokea sehemu nyingi Duniani, kama hakuna ushahidi watu watasema tofauti, mtoa taarifa akichukuliwa hatua watu wataacha kuchukua hayo matukio na watoto wataathirika. Tuwatie moyo watoa taarifa lakini wazifikishe pale panapotakiwa.”
 
Afisa Elimu manispaa ya Kinondoni alisema kama Siyo mitandao ya Kijamii na ITV kuripoti tukio la Msichana wa Darasa la saba kucharazwa fimbo 6 Kinyume cha kanuni basi Serikali isingepata taarifa kwani Mwalimu mkuu na uongozi wa shule walificha!
 
Back
Top Bottom