Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu mara kampeni za uchaguzi mkuu zitakapofunguliwa ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.
Akizungumza katika ibada ya siku kuu Eid Al Adha Jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema kuwa ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu.
“Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi” amesema Majaliwa
Waziri Mkuu pia amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha mazuri yenye lengo la kujenga jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa Taifa.
Akielezea kuhusu hayati Benjamini Mkapa ,amesema kuwa waislamu watamkumbuka kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha waislamu kwa kutoa majengo ya Serikali na kukabidhi kwa waislamu na hivyo kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho kilichopo mjini Morogoro.
Ippmedia.com