Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,128
- 1,896
CCM-tanzania yawaahidi wanakigoma na Watanzania kuwarejeshea tena kipenzi chao Mama Samian Suluhu Hassan 2025 Kwani ndani ya mwaka mmoja tu amefanya maajabu mengi,
===
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hana masihara na jambo linalobusu maendeleo ya wananchi.
Amesema kuthibitisha hilo, katika kipindi chake kifupi ameweka histori ya kuwa kiongozi wa kwanza kufikisha umeme wa gridi mkoani Kigoma jambo ambalo halikuwa limefanyika katika kipindi cha zaidi ya miaka 60 ya uhuru nchi.
Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2022, mjini Kasulu mkoani Kigoma, baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimia wananchi akiwa katika msafara wa Rais Samia ambaye yuko ziarani mkoani humo.
"Ndugu Mwenyekiti (Rais Samia) ukitaka kujua raha angalia wana Kasulu leo wanavyoonesha mbwembwe, eti wanawasha taa mchana...baada ya miaka 60 ya uhuru wa nchi hii Rais Samia amefanya maajabu makubwa, Rais Samia hana mbambamba katika kuleta maendeleo ya Watanzania," amesema.
Amesema kinachofanywa na Ras Samia na serikali yake ni kutekeleza ahadi ya CCM ya kuwaletea maendeleo wananchi.
"Dawa ya deni ni kulipa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichukua dhamana ya deni kwa Watanzania na wana Kasulu na wana Kigoma mwaka 2020. Ndugu Mwenyekiti kwa hali tuliyoiona leo tumeshuhudia namna ambavyo mkilipa deni hili kupitia Ibara ya 80 pale ulipokwenda ukaweka jiwe la msingi la kuzindua shule ya kisasa kabisa, lakini tumeshuhudia namna ambavyo mnalipa deni hili kupitia uimarishaji na uboreshaji wa nishati ya umeme, Ibara ya 63 ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi inavyotekelezwa kwa ufanisi mkubwa," amesema.
===