ISMAIL MKIMBIZI
Senior Member
- Jan 13, 2013
- 192
- 23
Ni diwani wa viti maalumu CUF Kasulu, anaitwa Ester Obed Kasyome ni hawala aka nyumba ndogo ya diwani wa Kata ya Ruhita CCM, Bw. Kabujanja. Pichani ni mtu wa pili kutoka kushoto akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Kasulu Benjamini Chalukula (CCM). PICHA hiyo ni jana katika kupokea mwenge wa uhuru mapema asubuhi kijiji cha Mvugwe wilayani Kasulu. Hapo yupo na madiwani wenzake wa CCM akiwa mwenye furaha bila kujali wenzake wa upinzani walioalikwa kuhudhuria walikataa.
Mama huyo historia yake ni mbaya sana katika harakati za mageuzi Kasulu kwa kuwa pamoja na upinzani kushinda viti vingi zaidi ya CCM kwa ubunge na udiwani wilayani Kasulu, habari za kuaminika ni yeye aliyeibeba CCM kwa rushwa aliyopewa akauangusha upinzani na Halmashauri ikaingia mikononi mwa walio wachache (CCM). Naamini hawezi akawa kiongozi mzuri katika UKAWA Kasulu wala hakubaliki na ni jembe la CCM kudhoofisha upinzani.
Najiuliza maswali mengi, kwa uhusiano huo (ambao ni dhahili ni kama mke na mume) alionao yeye diwani wa CUF na Bw. Kabujanja diwani CCM, siri za UKAWA Kasulu zitatunzwa? Mitaani wapo pamoja shambani wanakwenda wote, hapo kwenye picha Mvugwe wapo pamoja hatatuuza UKAWA kwa CCM? Na kwa kuwa alituuza siku za nyuma na ni uhakika na ushahidi tunao kwa nini CUF isimchukulie hatua za kinidhamu? Nashauri afutwe uanachama CUF aende akajiunge na mumewe CCM.
Alichotufanyia wanamageuzi Kasulu hatutakisahau, dhambi aliyotenda itamtafuna yeye na familia yake na mwisho wa siku kitaeleweka mpaka kaburini. Watu aina hii ambao huwa hawaeleweki huku wapo kule wapo ni sumu mbaya sana miongoni mwa wanamageuzi. Tumeona Lushoto mtu anajaza fomu kurudisha anakula kona harafu anazingishia alitekwa nyara kumbe alikula rushwa na alikuwa hana uchungu na CHADEMA. Mtu huyu hatufai Kasulu kabisaa CUF Mkoa au Taifa kama kweli mna nia ya dhati kwa muungano huu wa kuja kuweka mgombea mmoja tuungane mkono TAFAKARINI KWA KASYOME KISHA CHUKUENI HATUA.
Uzi ujao nitaingia jamvini na taarifa kuhusu jinsi ambavyo amekuwa akishiriki, michango na harambee mbalimbali za kuiimarisha CCM na jumuiya zake. Kasulu kwa sisi wazawa tunaoijua ni shuka ndogo ukinyosha miguu unang'atwa na mbu, usije ukafanya jambo la USALITI ukadhani itakuwa siri lazima mwisho wa siku uumbuke na itakukosti. Inaniuma sana watu tupo kwenye msiba wa watanzania maoni yetu kukataliwa kuunda katiba mpya harafu ninaona mtu ambaye ameaminiwa kupewa vyeo kibao CUF Kasulu mdau mwenzetu katika UKAWA anakwenda kucheza HALAIKI, disco wakinywa pombe na kushangila pamoja na muuaji (CCM) aliyemuua marehemu. Nakushauri Ester Kasyome mwisho wako umefika tumechoka usaliti kajiunge na CCM kabla hatujakufukuza ukaondoka kwa aibu, nenda mfuate mumeo Kabujanja acha tufanye mabadiliko.
Mwenge wa Uhuru, umekesha uwanja wa Umoja Kasulu mjini na asubuhi hii umeondoka kwenda wilayani Buhigwe.
UKAWA KASULU TUNASEMA TANGANYIKA HURU, ZANZIBAR HURU NI MSINGI WA UIMARA WA MUUNGANO NA MAENDELEO ENDELEVU.