Wapendwa, nina tatizo ambalo mwanzoni lilikuwa dogo lakini sasa naweza kusema limekuwa sugu. Niliwahi kufanya sexual intercourse ambayo result yake ni kuumia na kujeruhiwa kwa kojoleo. Yaan nimeambukizwa ugonjwa kaswende. Nimefanya jitihada sana kuhakikisha napona bila mafanikia. Nimetumia vidonge na hata sindano lakini hazijanisaidia. Tatizo linapoa tu then linaanza kuleta madhara. Linaniletea uchovu na hata kojoleo halina raha yoyote. Nawaomba wataalam wa hapa wanivumbulie njia muafaka ya kunisaidia ikiwa ni pamoja na tiba kwa anayejua. Changieni sasa