KERO Kata ya Ilemi maeneo ya Juhudi, Ilemi Mapelele na Janga kuna matukio mengi ya uhalifu

KERO Kata ya Ilemi maeneo ya Juhudi, Ilemi Mapelele na Janga kuna matukio mengi ya uhalifu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Matukio ya uhalifu katika maeneo ya Juhudi, Ilemi Mapelele na eneo linaloitwa Janga Video, Kata ya Ilemi, Mbeya Mjini, Kumekuwa na matukio ya watu kupigwa nondo, kukatwa kwa mapanga na kuporwa mali zao kama fedha na simu.

Kwa hali hii, tunaomba Jeshi la Polisi liongeze ulinzi katika maeneo hayo, hususani nyakati za alfajiri kuanzia saa moja kasoro na kuanzia saa moja usiku, kwa kuwa muda huo matukio haya yanaonekana kuwa mengi.

Changamoto nyingine ni kwamba baadhi ya vijana wanaodaiwa kujihusisha na uhalifu wanapokamatwa, baada ya siku kadhaa tunaendelea kuwaona tena mitaani. Hali hii inawafanya wananchi kuishi kwa hofu na kuhisi kutokuwa salama katika maeneo yao.

Naomba suala hili lifuatiliwe na hatua zichukuliwe ili kuimarisha usalama katika maeneo hayo.

Tamko la Viongozi ~ Diwani wa Ilemi, Baraka Zambi: Vijana wote ambao wapo tayari kuacha uhalifu, ofisi ya Kata ipo tayari kuwapokea
 
Kama Wezi mnawachekea chekea kwa nini wasiwe wanawapiga mapanga?😎 Mnashindwa kuwaadhibu kisa tu mtoto wa mtaani kwenu sasa acha waendelee kuwaibiaa🫪
 
Back
Top Bottom