Kataeni Katiba Pendekezwa: Jukwaa la Wakristo Tanzania

Rapture Man

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Posts
439
Reaction score
145
Maaskofu Jukwaa la Wakristo: Kataeni Katiba. Dar es Salaam. (Source: Gazeti la Mwananchi) 👉Jukwaa la Wakristo Tanzania limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa 👉kupiga kura ya “hapana”.Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana na kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha mgawanyiko.“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu,” linasema tamko hilo la kurasa nne.Taarifa hiyo imekuja siku moja tu baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutangaza kuwa muswada wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi uliokuwa umeondolewa kwenye mkutano uliopita wa Bunge kwa ajili ya mashauriano zaidi, utawasilishwa katika vikao vya chombo hicho vinavyoanza Jumanne ijayo baada ya kufikiwa kwa maridhiano baina ya viongozi mbalimbali wa dini.Pia tamko hilo limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuiagiza Hazina itoe fedha kwa Tume ya Uchaguzi (Nec) kwa kadri inavyohitaji ili kuiwezesha kukamilisha mchakato wa Kura ya Maoni.Viongozi wa Jukwaa la Wakristo walikutana Machi 10, mwaka huu kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi.Katiba inayopendekezwaTaarifa hiyo ya maneno 712 inasema: “Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe.👉“Pia haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali kama muundo wa Serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya rais na uwiano wa mihimili ya dola.“Ikumbukwe Katiba Inayopendekezwa ilipitishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa ahadi ya Serikali kuipa dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi. 👉Inashangaza kuwa hata Serikali inatoa rushwa ili kufikia malengo yake. Kwa hali kama hii, Kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa,” ilisema sehemu ya tamko hilo.Mahakama ya Kadhi: Kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, taarifa hiyo inasema, “Suala la uanzishwaji wa Mahakama hii nchini kama tulivyotoa maoni yetu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (Januari 16, 2015); barua yetu kwa Waziri Mkuu na matamko mbalimbali yaliyokwisha kutolewa kuhusu jambo hili; Mahakama ya Kadhi inakiuka misingi ya Taifa hili kuwa na Serikali isiyokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia wake kwa misingi ya dini.” Inaeleza kuwa mjadala unaoendelea unavunja Katiba ya Jamhuri Ibara ya 19 kwa kuendelea kujadili suala hilo katika Ilani za vyama vya Siasa, majukwaa ya kisiasa na bungeni na kusisitiza kuwa suala hilo limeligawa Taifa, Serikali, Bunge, Mahakama na wananchi.“Mahakama ya Kadhi imekuwa ikiendelea kutumiwa na wanasiasa kama mtaji wao wa kujipatia madaraka kwa gharama za kuleta chuki za kidini.“Kwa dhamiri safi, Jukwaa linatamka wazi kuwa mjadala unaoendelea kati ya Serikali na vikundi vya kidini kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kikatiba na kisheria ufungwe na badala yake ziachiwe taasisi husika za kidini kuamua juu ya masuala hayo bila kuihusisha Serikali wala waumini wa dini nyingine,” inasema taarifa hiyo. Hali ya usalama: Kuhusu hali ya usalama nchini Jukwaa hilo limeeleza kusikitishwa na viashiria pevu vya ugaidi vilivyoanza kujitokeza nchini kwa takribani miaka mitano iliyopita na kwamba kumekuwa na vitendo vinavyoashiria kuchipuka kwa ugaidi nchini. Maaskofu hao wameyataja matukio kama vile uvamizi wa vituo vya polisi, kuporwa silaha na mauaji ya polisi, mafunzo ya kareti katika nyumba za ibada, mafunzo ya itikadi kali za kidini kwa watoto, tukio la Amboni Tanga, mauaji ya viongozi wa dini, uchomaji wa nyumba za Ibada na kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini.“Jukwaa linasikitishwa na mwendelezo wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino) na ukatili unaosababisha ulemavu wa kudumu wa maalbino katika nchi yetu. Hali hii inatishia utulivu, amani na umoja wa kitaifa tuliokuwa nao kama Taifa la mfano barani Afrika,” inaeleza taarifa hiyo. Jukwaa hilo limewataka wananchi kuacha tabia ya kuua albino na kusisitiza kuwa kukosekana kwa uwajibikaji wa viongozi wa Serikali na kuongezeka kwa wigo wa kipato kati ya walionacho na wasionacho kunachangia ongezeko la vitendo hivyo viovu.👉“Mbona tembo na ng’ombe wakiuawa operesheni maalumu zinafanyika na viongozi wanawajibika, kwa nini maalbino wakiuawa viongozi hawawajibiki,” inahoji sehemu ya taarifa hiyo.👉“Kwa kuwa chama tawala na Serikali wameshindwa kusimamia misingi iliyolea taifa kama serikali isiyo ya kidini na taifa lenye amani; umoja na utulivu; Jukwaa linawaelekeza waumini wote na wenye mapenzi mema 👉wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao kufanya maamuzi yanayolitanguliza Taifa badala ya kutanguliza mazoea, mapokeo, itikadi na ushabiki wa chama fulani cha Siasa.”
 
Nawashukuru sana Maaskofu waliotia saini waraka unaowataka waumini wao wajiandikishe kwa wingi ili kushiriki kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa. Hili ni jambo la kiungwana sana na kuleta amani katika Taifa, kwa hili nawapongeza sana. Naomba hata madhehebu yasiyo ya Kikristo kuiga mfano huu na kuwahimiza waumini wao wajitokeze kwa wingi ili kujiandikisha na kushiriki katika kura ya maoni. Jambo la pili nawashukuru viongozi hawa muhimu sana katika taifa ni kuwasisitiza kuisoma na kuilewa Katiba Inayopendekezwa. Ninaamini wakishaisoma watafanya uamzi sahihi na sio wa shinikizo. 1. Kuhusu miiko na maadili ya viongozi na watumishi wa Umma, Katiba Inayopendekezwa imeanisha vizuri sana katika SURA YA NNE: MAADILI NA MIIKO YA UONGOZI NA UTUMISHI WA UMMA,
SEHEMU YA KWANZA inaongelea MAADILI YA UONGOZI NA UTUMISHI WA UMMA
na SEHEMU YA PILI:
MIIKO YA UONGOZI WA UMMA. Kwa hiyo ndugu muumini ukisoma hapo utaelewa vizuri jinsi miiko na maadili ya viongozi wa umma yalivyoelezwa. 2. Kuhusu Mahakama ya Kadhi. Jamani tuache ushabiki, Mahakama ya Kadhi haipo kwenye Katiba Inayopendekezwa. Hapa tusichanganye hoja. Hii itafanya waumini wetu watuone kama tunawadanganya. 3. Muundo wa Serikali umeelezwa vizuri na hauna mkorogano, hebu chukua muda usome mwenyewe na uelewe ili uipigie kura ya ndio katiba ambayoi imajali makundi yote. Viongozi wa Dini tunaambiwa tuheshimu na kutii mamlaka kwa maana mamlaka zote zote kwa Mungu. Warumi 13 inasema Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. [SUP]2 [/SUP]Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. [SUP]3 [/SUP]Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. [SUP]4 [/SUP]Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. [SUP]5 [/SUP]Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri. 4. Kuikataa Katiba Inayopendekezwa ni kukataa kumtii Kristo tunayemhubiri. Nizidi kuwashukuru kwa hamasa ya kuwataka waumini wenu waisome kwa makini Katiba Inayopendekezwa na kufanya maamuzi sahihi.
 
Lakini hawa akina pinda, membe lowasa na wengineo si tunawaonaga makanisani huku?! ebu waambilieni huko wakija kusali, waache huu unafiki wa undumila kuwili.
 
Sina uhakika kama haya umeyaandika kwa kunukuu Biblia kwa weledi au ni kwa matakwa yako binafsi! lakini ngoja nikukumbushe kwamba Mwana wa Adamu alikuja kuwakomboa watu kutoka kwenye makucha ya ibirisi shetani, na si kwamba alipokuja hapa duniani alikuwa anapambana na shetani moja kwa moja bali alikuwa anapambana na shetani aliyejificha kwenye miili na akili za watawala wa nyakati hizo, watawala ambao ndio tulio nao nyakati hizi.

Lakini hakuwapinga kwamba sio viongozi na si kwamba hakutambua kuwa uongozi/ mamlaka waliyokuwa nayo yalitoka kwa Mungu, alijua kwa sababu alikuwepo wakati Mungu anagawa hayo mamlaka kwa watawala hao. Lakini Mwana wa Adamu asingeweza kuvumilia unyanyasaji na ukihukaji mkubwa wa mapenzi ya Mungu uliokuwa unafanywa na watawala hao ambao walishakuwa shirika na shetani na kuyatenda yasiyompendeza Mungu.

Hira na ghiliba zao za kutotaka kuondoka madarakani (katiba pendekezwa) ndio zilipelekea kumsurubisha Mwana wa Adamu wakidhani huyu kampeini zake zimekuwa kali na hivyo hofu ya kuondolewa madarakani ikawapata mpaka wakabuni mashitaka ya uongo na hatmaye kutoa hukumu isiyo haki dhidi yake, na kweli Mwana wa Adamu akahangikwa msalabani.

Upofu wa madaraka hayo waliyopewa na Mungu uliwafikisha mahala pa kutomtambua Mwana wa Mungu hata pale alipowaambia kuwa utawala wake si wa dunia hii, hata pale alipowatendea miujiza bado hawakuona kwa sababu walihemkwa na uchu wa madaraka na nadhani albino hawakuwepo nyaka hizo wangekufa sana ili kumuondoa Mwana wa Adamu aliyekuwa anaonekana tishio kwao.

Nifupishe tu ndugu yangu kwamba ni kweli Biblia inasema hivyo kwamba mamlaka zinatoka juu, lakini pia shetani naye alitoka juu hukohuko hivyo anazo mbinu nyingi za kuwaingia wanadamu walio mamlakani na kuwafanya kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu, na kwa maana hiyo kubatirisha uhusiano wa mamlaka hayo na mbingu.
 
Kura ya maoni haiwezekani tena.taratibu hazitakamilika labda sheria ibadilishwe.siku 60 za elimu hazipatikani na siku 30 za kampeni pia.
 
Wakinapinda wamewahonga maaskofu na wachungaji uchwara, wakaawapeleka kutalii kwenye mbuga za wanyama. Waliitisha Kikao feki cha maridhiano ya Viongozi wa dini wakawatumia maaskofu na wachungaji feki waliowahonga ili kupata colum ya kutosha kwa upande wa Wakristo.
 
HAPANA ! HAPANA ! HAPANA !

...Dar es Salaam. Jukwaa la Wakristo Tanzania limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa kupiga kura ya “hapana”.

Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana na kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha mgawanyiko.

“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu,” linasema tamko hilo la kurasa nne.

Taarifa hiyo imekuja siku moja tu baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutangaza kuwa muswada wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi uliokuwa umeondolewa kwenye mkutano uliopita wa Bunge kwa ajili ya mashauriano zaidi, utawasilishwa katika vikao vya chombo hicho vinavyoanza Jumanne ijayo baada ya kufikiwa kwa maridhiano baina ya viongozi mbalimbali wa dini.

Pia tamko hilo limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuiagiza Hazina itoe fedha kwa Tume ya Uchaguzi (Nec) kwa kadri inavyohitaji ili kuiwezesha kukamilisha mchakato wa Kura ya Maoni.

Viongozi wa Jukwaa la Wakristo walikutana Machi 10, mwaka huu kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi.

Katiba inayopendekezwa

Taarifa hiyo ya maneno 712 inasema: “Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe.

“Pia haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali kama muundo wa Serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya rais na uwiano wa mihimili ya dola.

“Ikumbukwe Katiba Inayopendekezwa ilipitishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa ahadi ya Serikali kuipa dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi. Inashangaza kuwa hata Serikali inatoa rushwa ili kufikia malengo yake. Kwa hali kama hii, Kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa,” ilisema sehemu ya tamko hilo.

Mahakama ya Kadhi

Kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, taarifa hiyo inasema, “Suala la uanzishwaji wa Mahakama hii nchini kama tulivyotoa maoni yetu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (Januari 16, 2015); barua yetu kwa Waziri Mkuu na matamko mbalimbali yaliyokwisha kutolewa kuhusu jambo hili; Mahakama ya Kadhi inakiuka misingi ya Taifa hili kuwa na Serikali isiyokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia wake kwa misingi ya dini.”
Inaeleza kuwa mjadala unaoendelea unavunja Katiba ya Jamhuri Ibara ya 19 kwa kuendelea kujadili suala hilo katika Ilani za vyama vya Siasa, majukwaa ya kisiasa na bungeni na kusisitiza kuwa suala hilo limeligawa Taifa, Serikali, Bunge, Mahakama na wananchi.

“Mahakama ya Kadhi imekuwa ikiendelea kutumiwa na wanasiasa kama mtaji wao wa kujipatia madaraka kwa gharama za kuleta chuki za kidini.

“Kwa dhamiri safi, Jukwaa linatamka wazi kuwa mjadala unaoendelea kati ya Serikali na vikundi vya kidini kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kikatiba na kisheria ufungwe na badala yake ziachiwe taasisi husika za kidini kuamua juu ya masuala hayo bila kuihusisha Serikali wala waumini wa dini nyingine,” inasema taarifa hiyo.

Hali ya usalama

Kuhusu hali ya usalama nchini Jukwaa hilo limeeleza kusikitishwa na viashiria pevu vya ugaidi vilivyoanza kujitokeza nchini kwa takribani miaka mitano iliyopita na kwamba kumekuwa na vitendo vinavyoashiria kuchipuka kwa ugaidi nchini.

Maaskofu hao wameyataja matukio kama vile uvamizi wa vituo vya polisi, kuporwa silaha na mauaji ya polisi, mafunzo ya kareti katika nyumba za ibada, mafunzo ya itikadi kali za kidini kwa watoto, tukio la Amboni Tanga, mauaji ya viongozi wa dini, uchomaji wa nyumba za Ibada na kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini.

“Jukwaa linasikitishwa na mwendelezo wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino) na ukatili unaosababisha ulemavu wa kudumu wa maalbino katika nchi yetu. Hali hii inatishia utulivu, amani na umoja wa kitaifa tuliokuwa nao kama Taifa la mfano barani Afrika,” inaeleza taarifa hiyo.

Jukwaa hilo limewataka wananchi kuacha tabia ya kuua albino na kusisitiza kuwa kukosekana kwa uwajibikaji wa viongozi wa Serikali na kuongezeka kwa wigo wa kipato kati ya walionacho na wasionacho kunachangia ongezeko la vitendo hivyo viovu.

“Mbona tembo na ng’ombe wakiuawa operesheni maalumu zinafanyika na viongozi wanawajibika, kwa nini maalbino wakiuawa viongozi hawawajibiki,” inahoji sehemu ya taarifa hiyo.

“Kwa kuwa chama tawala na Serikali wameshindwa kusimamia misingi iliyolea taifa kama serikali isiyo ya kidini na taifa lenye amani; umoja na utulivu; Jukwaa linawaelekeza waumini wote na wenye mapenzi mema wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao kufanya maamuzi yanayolitanguliza Taifa badala ya kutanguliza mazoea, mapokeo, itikadi na ushabiki wa chama fulani cha Siasa.”
 
Viongozi wa dini nawaombeni msikimbilie kutoa kasoro ambazo hazipo eti imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu mara mchakato umeendeshwa kwa hila na ubabe!! La hasha, hizo hoja hazina ukweli wowote, nyie tuna waamini sana na hata vitabu vya dini vinawataka Viongozi wa Dini kuheshimu na kutii mamlaka kwa maana mamlaka zote ni za Mungu. Mkisoma kitabu cha Warumi 13, kinasema kuwa "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala, kwa maana hakuna Mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na Serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu". Ushauri wangu isomeni Katiba hiyo ili mujionee ukweli wa mambo mazuri yaliyomo ndani ya Katiba hiyo. Asanteni!
 
Asante viongozi wangu wa dini.Hata kwny majumba ya ibada waambieni watu wajiandikishe kwa wingi na wakapige HAPANA.Mtahukumiwa mkikaa kimya na kuacha kondoo wakapotea.
Ni muda wa kuweka wazi na kutofumbia uozo uliopo ktk ka-taifa haka.
 
Jukwaa la Wakristo Tanzania madai yenu kuhusu suala la ulinzi na usalama nawashauri muipate Katiba Inayopendekezwa na muisome kwa makini Katiba hiyo katika SURA YA 17 mtapata majibu mazuri ya wasiwasi wenu kuhusu usalama wa nchi.

Kuhusu suala la Muundo wa Serikali, wajameni SURA YA 7 ya Katiba Inayopendekezwa imeeleza wazi wazi juu ya Muundo wa Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 73.

Kuhusu masuala ya mauaji ya watu wenye ualbino, nadhani kila siku mnasikia wahusika wanavyokamatwa haswa waganga wa jadi pamoja na wauaji, lakini pia kuna kesi mbalimbali zinaendelea na nyingine zimeshatolewa hukumu kali.

Kuhusu kuwataka waumini wenu wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu mlizozitaja hapo mmechemsha, kwasababu msidhani kuwa waumini wote watafanya hivyo, nina amini wapo waumini wenye busara na wenye uelewa juu ya ukweli wa mambo mazuri yaliyoelezwa ndani ya Katiba Inayopendekezwa ambao hawatapoteza haki yao ya kufanya hivyo mlivyopanga.

Lakini pia hivi hamuoni kuwa mtakuwa mmemkosea Mwenyezi Mungu kwa kuwashinikiza waumini wenu waipinge Katiba hiyo? Kwani hata Biblia yenyewe inasema "ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu", sasa udikteta huo mnaowafanyia waumini mmeupata wapi? Dini mnaiingiza na siasa tena jamani? Tanzania ni nchi isiyokuwa na dini, kuweni makini msije mkaulizwa na Muumba wenu je kwanini mliwanyima haki waumini wenu katika Mamlaka ya Dunia. Kuweni mfano wa mbele katika kuelimisha waumini badala ya kuwashinikiza waikatae. Huo sio uungwana kabisaaaaa!.
 
Maaskofu Jukwaa la Wakristo: Kataeni Katiba. Dar es Salaam. (Source: Gazeti la Mwananchi) 👉Jukwaa la Wakristo Tanzania limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa 👉kupiga kura ya “hapana”.Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana na kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha mgawanyiko.“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu,” linasema tamko hilo la kurasa nne.Taarifa hiyo imekuja siku moja tu baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutangaza kuwa muswada wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi uliokuwa umeondolewa kwenye mkutano uliopita wa Bunge kwa ajili ya mashauriano zaidi, utawasilishwa katika vikao vya chombo hicho vinavyoanza Jumanne ijayo baada ya kufikiwa kwa maridhiano baina ya viongozi mbalimbali wa dini.Pia tamko hilo limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuiagiza Hazina itoe fedha kwa Tume ya Uchaguzi (Nec) kwa kadri inavyohitaji ili kuiwezesha kukamilisha mchakato wa Kura ya Maoni.Viongozi wa Jukwaa la Wakristo walikutana Machi 10, mwaka huu kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi.Katiba inayopendekezwaTaarifa hiyo ya maneno 712 inasema: “Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe.👉“Pia haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali kama muundo wa Serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya rais na uwiano wa mihimili ya dola.“Ikumbukwe Katiba Inayopendekezwa ilipitishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa ahadi ya Serikali kuipa dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi. 👉Inashangaza kuwa hata Serikali inatoa rushwa ili kufikia malengo yake. Kwa hali kama hii, Kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa,” ilisema sehemu ya tamko hilo.Mahakama ya Kadhi: Kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, taarifa hiyo inasema, “Suala la uanzishwaji wa Mahakama hii nchini kama tulivyotoa maoni yetu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (Januari 16, 2015); barua yetu kwa Waziri Mkuu na matamko mbalimbali yaliyokwisha kutolewa kuhusu jambo hili; Mahakama ya Kadhi inakiuka misingi ya Taifa hili kuwa na Serikali isiyokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia wake kwa misingi ya dini.” Inaeleza kuwa mjadala unaoendelea unavunja Katiba ya Jamhuri Ibara ya 19 kwa kuendelea kujadili suala hilo katika Ilani za vyama vya Siasa, majukwaa ya kisiasa na bungeni na kusisitiza kuwa suala hilo limeligawa Taifa, Serikali, Bunge, Mahakama na wananchi.“Mahakama ya Kadhi imekuwa ikiendelea kutumiwa na wanasiasa kama mtaji wao wa kujipatia madaraka kwa gharama za kuleta chuki za kidini.“Kwa dhamiri safi, Jukwaa linatamka wazi kuwa mjadala unaoendelea kati ya Serikali na vikundi vya kidini kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kikatiba na kisheria ufungwe na badala yake ziachiwe taasisi husika za kidini kuamua juu ya masuala hayo bila kuihusisha Serikali wala waumini wa dini nyingine,” inasema taarifa hiyo. Hali ya usalama: Kuhusu hali ya usalama nchini Jukwaa hilo limeeleza kusikitishwa na viashiria pevu vya ugaidi vilivyoanza kujitokeza nchini kwa takribani miaka mitano iliyopita na kwamba kumekuwa na vitendo vinavyoashiria kuchipuka kwa ugaidi nchini. Maaskofu hao wameyataja matukio kama vile uvamizi wa vituo vya polisi, kuporwa silaha na mauaji ya polisi, mafunzo ya kareti katika nyumba za ibada, mafunzo ya itikadi kali za kidini kwa watoto, tukio la Amboni Tanga, mauaji ya viongozi wa dini, uchomaji wa nyumba za Ibada na kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini.“Jukwaa linasikitishwa na mwendelezo wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino) na ukatili unaosababisha ulemavu wa kudumu wa maalbino katika nchi yetu. Hali hii inatishia utulivu, amani na umoja wa kitaifa tuliokuwa nao kama Taifa la mfano barani Afrika,” inaeleza taarifa hiyo. Jukwaa hilo limewataka wananchi kuacha tabia ya kuua albino na kusisitiza kuwa kukosekana kwa uwajibikaji wa viongozi wa Serikali na kuongezeka kwa wigo wa kipato kati ya walionacho na wasionacho kunachangia ongezeko la vitendo hivyo viovu.👉“Mbona tembo na ng’ombe wakiuawa operesheni maalumu zinafanyika na viongozi wanawajibika, kwa nini maalbino wakiuawa viongozi hawawajibiki,” inahoji sehemu ya taarifa hiyo.👉“Kwa kuwa chama tawala na Serikali wameshindwa kusimamia misingi iliyolea taifa kama serikali isiyo ya kidini na taifa lenye amani; umoja na utulivu; Jukwaa linawaelekeza waumini wote na wenye mapenzi mema 👉wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao kufanya maamuzi yanayolitanguliza Taifa badala ya kutanguliza mazoea, mapokeo, itikadi na ushabiki wa chama fulani cha Siasa.”

Hivyo, ikitokea na waislam nao wakaunda jukwaa Lao na wakapanda juu na wakatoa walaka unaosema " Waislamu jiandikisheni kwa wingi ili mkapige kura ya ndio ya kuikubali katiba iliyopendekezwa kwa kuwa ni nzuri na inatambua mahakama ya kadhi". Hivi nini kitatokea! Tunakwenda wapi jamani!
 
Mm nadhani huo muswaada unootaka kupelekwa bungeni wa mahakama ya kadhi ubadilishwe badala ya muswada kadhi uwe muswada wa kutuuwa waislam wote wa tz nadhani wenzetu wakiristo ndio wataridhika.
 
Viongozi wa dini nawaombeni msikimbilie kutoa kasoro ambazo hazipo eti imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu mara mchakato umeendeshwa kwa hila na ubabe!! La hasha, hizo hoja hazina ukweli wowote, nyie tuna waamini sana na hata vitabu vya dini vinawataka Viongozi wa Dini kuheshimu na kutii mamlaka kwa maana mamlaka zote ni za Mungu. Mkisoma kitabu cha Warumi 13, kinasema kuwa "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala, kwa maana hakuna Mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na Serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu". Ushauri wangu isomeni Katiba hiyo ili mujionee ukweli wa mambo mazuri yaliyomo ndani ya Katiba hiyo. Asanteni!

Sote tuliona jinsi ilivyopatikana,,,, kuisoma ni kupoteza mda,,,,
 
Naamini hata wewe unaeipinga haki zako zimewekwa katika Katiba hiyo hiyo unayoipinga, sasa ukiipinga hao viongozi wa dini ndo watakupatia hizo haki zako? tumia akili
 
...lakini ngoja nikukumbushe kwamba Mwana wa Adamu alikuja kuwakomboa watu kutoka kwenye makucha ya ibilisi shetani, na si kwamba alipokuja hapa duniani alikuwa anapambana na shetani moja kwa moja bali alikuwa anapambana na shetani aliyejificha kwenye miili na akili za watawala wa nyakati hizo, watawala ambao ndio tulio nao nyakati hizi.

Lakini hakuwapinga kwamba sio viongozi na si kwamba hakutambua kuwa uongozi/ mamlaka waliyokuwa nayo yalitoka kwa Mungu, alijua kwa sababu alikuwepo wakati Mungu anagawa hayo mamlaka kwa watawala hao. Lakini Mwana wa Adamu asingeweza kuvumilia unyanyasaji na ukihukaji mkubwa wa mapenzi ya Mungu uliokuwa unafanywa na watawala hao ambao walishakuwa shirika na shetani na kuyatenda yasiyompendeza Mungu.

Hila na ghiliba zao za kutotaka kuondoka madarakani (katiba pendekezwa) ndio zilipelekea kumsurubisha Mwana wa Adamu wakidhani huyu kampeini zake zimekuwa kali na hivyo hofu ya kuondolewa madarakani ikawapata mpaka wakabuni mashitaka ya uongo na hatmaye kutoa hukumu isiyo haki dhidi yake...

Upofu wa madaraka hayo waliyopewa na Mungu uliwafikisha mahala pa kutomtambua Mwana wa Mungu...

Nifupishe tu ndugu yangu kwamba ni kweli Biblia inasema hivyo kwamba mamlaka zinatoka juu, lakini pia shetani naye alitoka juu hukohuko hivyo anazo mbinu nyingi za kuwaingia wanadamu walio mamlakani na kuwafanya kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu, na kwa maana hiyo kubatilisha uhusiano wa mamlaka hayo na mbingu.
Safi sana Mulama. Umetoa majibu na ufafanuzi muafaka. You know well the context of your bible!
 
Ukitaka kujua kama katiba inayopenekezwa ni bora au sio bora isome ukiwa unailinganisha na rasimu ya Warioba hapo ndo utaelewa vizuri ..maana hii katiba imeandikwa kiujanja ujanja sana ukiisoma yenyewe peke yake unaweza ukajikuta unashawishika kuikubali.
 
Back
Top Bottom