Katambi alipoka majukumu ya baraza la usalama ya kutangaza hali ya hatari

Katambi alipoka majukumu ya baraza la usalama ya kutangaza hali ya hatari

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Unaandaa AFCON na unajua kutakuwa na wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali, halafu unatangaza nchi yako sio salama kuna magaidi.

Katambi, hukujua kutangaza Tanzania sio salama ni kuigharimu nchi kunaathiri uwekezaji, hujui kutangaza mmekamata magaidi 100 ni kuathiri utalii.

Sijui nani kawashitua, kwa hiki kipindi kifupi tayari mmeichafua nchi, mmelitia hasara taifa, ili tu kuikomoa Chadema na Heche na kumfurahisha mtu, mtatumia gharama kubwa kuisafisha.

Nchi hii inaendeshwa na vilaza sana.

IMG_20260730_074536.jpg
 
Unaandaa AFCON na unajua kutakuwa na wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali, halafu unawatangazia nchi yako ina magaidi sio salama.

Katambi, hukujua kutangaza Tanzania sio salama kungeathiri uwekezaji, jeshi la polisi kutangaza limekamata magaidi 300 halijui ni kuathiri utalii.

Sijui nani kawashitua, ila hasara mliyoisababisha kwa taifa kwa hiki kipindi kifupi ili kuwakomoa Chadema na kumfurahisha mtu, itachukua muda mrefu ku recover.

Nchi hii inaendeshwa na vilaza sana.
Gentleman,
magenge ya kigaidi na washukiwa wote wa ugaidi kote nchini wataendelea kusakwa kokote pale walipo na kutiwa nguvuni bila kujali hizo porojo zako 🐒
 
Ni aibu Katambi ataondoka kwenye hii wizara nda utakua mwisho wake kisiasa hii wizara haitaki siasa kutokana za zama tulizopo hiyo wizara inatakiwa kuongozwa na mwasheria nguli anaweza kusimamia usalama wa ndani police kutenda HAKI. ukileta uchawa utachomoka mapema kwenye hii wizara inaitaji mwenye akili na busara hii wizara sio wakina Katambi sijui kwanini walimtoa Chawene
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Leo wanalialia Tanzania hakuna ugaidi huku bado wanaendelea kukamata watu kwa kesi za ugaidi na vyombo vya habari vinaandika "watu kadhaa wakamatwa kwa kesi za ugaidi" hii nchi kweli inahitaji uponyaji 😁
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMAG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
 
Itawagharimu sana inabidi watafute PR wa kutangaza Tanzania haina magaidi Misime peke yake hatoshi.
Wajinga sana hawa jamaa, Kombo Waziri wa Mambi ya nje anatumia mabilioni huko ughaibuni kusafisha uchafu wa 29.10,2025 huku nyuma huyu mwenye meno kama anakula kinyesi na mapolisi wake wanaitangazia dunia kuwa Tanzania kuna ugaidi, hakika huu ni utawala uliofitinika na anguko lake ni dhahiri halipo mbali.
GhfJRpEacAEgTRK.jpeg
 
Gentleman,
magenge ya kigaidi na washukiwa wote wa ugaidi kote nchini wataendelea kusakwa kokote pale walipo na kutiwa nguvuni bila kujali hizo porojo zako 🐒
Pamoja na porojo zako mkumbushe mama zimebaki siku 9.

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.
 
Pamoja na porojo zako kumbushe mama zimebaki siku 9.

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.
hiyo nonsense ikusumbue wewe na wafuata mkumbo wenzako gentleman na itapendeza zaidi 🐒
 
Ni aibu Katambi ataondoka kwenye hii wizara nda utakua mwisho wake kisiasa hii wizara haitaki siasa kutokana za zama tulizopo hiyo wizara inatakiwa kuongozwa na mwasheria nguli anaweza kusimamia usalama wa ndani police kutenda HAKI. ukileta uchawa utachomoka mapema kwenye hii wizara inaitaji mwenye akili na busara hii wizara sio wakina Katambi sijui kwanini walimtoa Chawene
Sijui alikuwa anawaza Nini...Kamharibia hata Mama, kipindi ambacho ni very vulnerable yeye anachochea Kuni, pengine bado yupo upinzani ndiyo sababu anafanya haya
 
Back
Top Bottom