Katambi: Kufikia Aprili 2026 watuhumiwa 49,469 wa makosa ya kiuhamiaji walikamatwa

Katambi: Kufikia Aprili 2026 watuhumiwa 49,469 wa makosa ya kiuhamiaji walikamatwa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, Bungeni Dodoma leo Mei 25, 2026 akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ameeleza kuwa operesheni, doria, na misako ya kimkakati iliyofanywa na Idara ya Uhamiaji imesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti uingiaji holela wa wageni nchini ambapo hadi Aprili 2026 jumla ya watuhumiwa 49,469 walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo wahamiaji haramu 34,099 wamefukuzwa na kuondolewa nchini.

Waziri Katambi, ametoa wito kwa Watanzania nchi nzima kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Idara ya Uhamiaji kwa kuwafichua wageni wote wanaoishi kwenye makazi na maeneo yao kinyume na sheria, kanuni, na taratibu za nchi.

 
Back
Top Bottom