Katambi: Maandamano ni haki lakini sharti Polisi wapewe taarifa

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
"Kuzingatia maelezo ambayo ni msingi wa kikatiba na sheria, msimamo wa kisheria nchini ni kwamba haki ya kufanya mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba lakini utekelezaji wake unaweza kuwekwa chini ya masharti ya sheria inayolenga kulinda usalama, utulivu wa umma na haki za wengine. Kifungu cha 43 kimeka msisitizo kuwa waandaaji lazima wawasilishe taarifa ya maandishi saa 48 kabla ya tukio," amesema Katambi.

Waziri amefafanua kuwa baada ya taarifa hiyo kuwasilishwa, waandaaji wanaweza kuendelea na maandalizi, isipokuwa tu pale Kamanda wa Polisi wa Wilaya au Mkoa atakapotoa amri ya kusitisha baada ya kubaini kuwa mkusanyiko huo unaweza kuvunja amani, kuhatarisha usalama, au kutumika kwa madhumuni yasiyo halali.
 
Wajuzi wa sheria wako humu vifungu vya sheria vimekamilika kweli?
 
🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…