Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametoa ufafafnuzi kuhusu kanuni za Usalama Barabarani za mwaka 2014 zilizorekebishwa mwaka 2025 ambapo amesema kinachofanyika ni majaribio ya namna mfumo huo utakavyoweza kutumika ili kudhibiti madereva wasiotii sheria na kanuni za usalama barabarani.
Waziri Katambi ameto ufafanuzi huo leo Septemba 19, 2026 ambapo amewatoa hofu madereva kwamba mfumo huo bado haujaanza kutekelezwa rasmi hivyo hakuna haja ya dereva yoyote ambae leseni yake imeondolewa alama kutokana na kosa aliloandikiwa tozo kuwa na wasiwasi.
Kwa mujibu wa taarifa yake, amesema Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi anayo mamlaka ya kutunga kanuni kuhusu masuala yanayohusu Usalama Barabarani kwa ajili ya kupunguza wimbi la ajali za Barabarani zinazotokana na sababu mbalimbali ikiwemo makosa ya kibinadamu yanayosababishwa na watumiaji wa Vyombo vya usafiri na Usafirishaji.