DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Mkoani Shinyanga na Naibu Waziri, Ofisi ya waziri Mkuu (Kazi, Vijana na watu wenye ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi amesema ndani ya miaka minne ya Uongozi wa serikali ya awamu ya sita mapinduzi makubwa yamefanyika kwenye uwezeshaji wananchi kiuchumi, suala ambalo limefanikisha kuondoa omba omba waliokuwa wakionekana kwenye maeneo mbalimbali ya Miji nchini.
Katambi ameyasema hayo leo Jumamosi Oktoba 11, 2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa wananchi wa Shinyanga Mjini kwenye Viwanja vya Kambarage, wakati wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimshukuru pia Mgombea huyo kwa wema na uungwana wake kwa Watanzania.
Ameeleza mafanikio hayo kuwa yametokana na uanzishwaji wa mfuko maalumu wa watu wenye ulemavu ambapo zaidi ya Bilioni 2 zimeingia kwenye Akaunti zao kama ruzuku ya kuwasaidia sambamba na Mikopo.
Aidha Katambi pia amezungumzia mapinduzi yaliyofanyika katika kuimarisha mifuko ya pensheni pamoja na mfuko wa usalama na afya mahali pa kazi OSHA, akisema mfuko huo sasa umekuwa wa mfano kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati sambamba na mikopo mingine kwa Vijana na wanawake.
"Leo vijana wanapata mikopo ya zaidi ya Bilioni 160, tunakushukuru sana Vijana na hakika wewe ni rafiki na Kipenzi cha Vijana na kupitia mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi, Mhe. Mgombea Urais umetoa zaidi ya Shilingi Trilioni 4 ambazo zimenufaisha wananchi zaidi ya Milioni 24 wakiwemo Vijana, wanawake na Makundi mbalimbali. Tunakushukuru sana umeupiga mwingi." Amesisitiza Mhe. Katambi.
Kiongozi huyo pia amemshukuru Dkt. Samia kwa mabadiliko makubwa ya sera ya Maendeleo ya Vijana ili iendane na matakwa na matamanio ya leo kwaajili ya kuendelea kunufaisha zaidi Vijana na kuwaendeleza kiuchumi.