Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi amezitaka Jumuiya za kiraia nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha umoja, mshikamano na kulinda amani.
Wito huo ameutoa wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 70 ya Usajili wa Jumuiya za Kiraia katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Katambi amesisitiza kuwa,Taifa letu lina historia nzuri katika kulinda amani na utulivu wa nchi, hivyo ni vizuri kuendelea kuilinda historia hiyo kwa kuepuka kuingia kwenye vurugu na machafuko yanayoweza kusababisha kupoteza amani.