Katavi: Barabara iliyofungwa kutokana na athari za mafuriko kuanza kutumika

Katavi: Barabara iliyofungwa kutokana na athari za mafuriko kuanza kutumika

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Katavi, Mhandisi Martin Mwakabende ameifungua barabara hiyo baada ya kufanyiwa ukaguzi na ukarabati wa Daraja la Stalike kuelekea Mkoani Rukwa.

Barabara hiyo ilifungwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko baada ya kujaa maji yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Aidha, Mhandisi Mwakabende amesema Serikali kupitia Rais wa Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni moja kukarabati barabara zote zilizoharibiwa na mafuriko.

Hali ilivyokuwa awali - Katavi: Barabara imefungwa baada ya mafuriko kukwamisha Abiria
 
Back
Top Bottom