DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1,172,824,000/= ambapo mchanganuo wake ni kama ifuatavyo:
Vikundi vya Wanawake (107), Tshs. Milioni 529,765,000/=
Vikundi vya Vijana (97), Tshs. Milioni 603,843,000/=
Vikundi vya Watu wenye Ulemavu (16), Tshs Milioni 39,216,000/=
Aidha, mikopo hii imetolewa kwa kila Kata kwa vikundi vyenye sifa zilizobainishwa kwenye muongozo wa utoaji wa mikopo ya 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri wa Mwaka 2024, ambapo katika Kata ya Ikola jumla ya vikundi (15) vimenufaika na kiasi cha shilingi Milioni 69,000,000/= kwa mchanganuo ufuatao:
Vikundi vya Wanawake (6), Tshs. Milioni 29,000,000/=
Vikundi vya Vijana (8), Tshs. Milioni 39,000,000/=
Vikundi vya Watu wenye Ulemavu (1), Tshs Milioni 1,000,000/=
Kwa awamu hii Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 251,268,048.95/= ambayo ni Bakaa ya asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25, Hivyo basi Mkurugenzi Mtendaji anavikaribisha vikundi vyote kutuma maombi yao kwaajili ya kupatiwa mkopo, ambapo sifa zifuatazo zitazingatiwa:
Kiwe kikundi aidha cha Wanawake, Vijana au cha Watu wenye ulemavu kilichotambuliwa, kusajiliwa na kupewa cheti cha utambuzi cha Halmashauri.
Kiwe kinajishughulisha na ujasiriamali mdogo au mkubwa au kiwe kinatarajia kuanzisha shughuli za ujasiriamali.
Kikundi kiwe na akaunti ya Benki iliyofunguliwa kwa jina la Kikundi.
NB: Kipaumbele kitakuwa kwa vikundi ambavyo viliwahi kuomba mkopo na kukosa kutokana na mapungufu yaliyobainishwa na kamati.
Mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ni Septemba 10, 2025 saa 9:30 Alasiri.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini H/W Tanganyika.