LGE2024 Katavi: Jeshi la Polisi lawaasa Waandishi wa Habari kuepuka kuandika habari za kichochezi kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa

LGE2024 Katavi: Jeshi la Polisi lawaasa Waandishi wa Habari kuepuka kuandika habari za kichochezi kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Lungo hilo la kuwanyamazisha waandishi wa habari kipindi hiki cha uchaguzi. Habari za Uchochezi ni zipi?

=====
1732527648056.png


Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanya kikao kazi na Waandishi wa Habari na kuwataka kujiepusha kuandika, kuripoti habari za uchochezi hususani kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 Nchini.

1732527677258.png

Hayo yamejiri wakati wa kikao kilichofanyika Novemba 24, 2024 katika ukumbi wa mkutano Polisi Katavi ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani amesema kuwa Polisi Mkoa wa Katavi imejipanga vyema kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya utulivu na amani.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

1732527704883.png

Aidha, amewasisitisa waandishi wa Habari kuendelea kuwa wazalendo na kutumia kalamu zao vizuri kwa kuwajulisha wananchi kuhusu haki na wajibu wa mpiga kura na jinsi mchakato mzima wa uchaguzi unavyoenda.
 
Back
Top Bottom