Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wanajukwaa!
Habari iwafike kutoka CHADEMA. Baadhi ya makada wa chama hicho wamendelea kuonyesha upande katika kuelekea uchaguzi wa CHADEMA taifa ambao utafanyika mwaka 2025.
Inavyoenyesha Mbowe ni kama time yake ya kuachia ngazi wengi wanatamani kumuona Lissu kwenye nafasi ya Uenyekiti wa chama!
====================
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi, Deus Josephat, ameonesha wazi msimamo wake wa kumtaka Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, Freeman Mbowe
kumwachia nafasi Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu , ili aweze kugombea nafasi ya uenyekiti wa Taifa.
Soma Pia:
"Kama Mbowe aliridhia Lissu kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2020, sasa leo anashindwaje kuongoza chama ambacho kina kanda zake kumi?" amesema Deus.
Katibu huyo amesisitiza kuwa wote, Mbowe na Lissu, wana historia ya kukipigania chama na wamepitia changamoto nyingi katika siasa za upinzani nchini. Hata hivyo, amesisitiza kuwa mazingira ya sasa ya kisiasa nchini yanahitaji kiongozi mwenye sifa kama za Lissu.
"Mimi ninaamini kwa sasa tulipofikia kama nchi na siasa zake zilivyo, zinamuhitaji sana mtu kama Lissu atekeleze pale ambapo Mwenyekiti Mbowe aliachia," amesema.

- Ratiba Kamili Ya Uchaguzi Wa CHADEMA Taifa
- Tundu Lissu achukua rasmi Fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA
- Mbowe: Familia yangu imeniambia niachane na siasa