Katavi kuna ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia kwa 12.5%

Katavi kuna ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia kwa 12.5%

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamanda wa Polisi Mkoa, ACP Ali Makame amesema ongezeko hilo ni kuanzia Januari hadi Septemba 2022 ambapo kulikuwa na matukio 270 ya ukatili kulinganisha na 240 yaliyotokea mwaka 2021.

Ametaja sababu zinazoongeza matukio hayo ni pamoja na tatizo la Afya ya Akili na kupungua kwa utoaji elimu juu ya madhara ya ukatili na unyayasaji wa kijinsia kwa jamii.

Ili kudhibiti matukio hayo, ACP Makame amesema Jeshi la Polisi limeweka mikakati ya kuongeza kasi ya kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na kupitia njia nyinginezo ikiwemo mikutano ya hadhara.

=======================

Matukio 270 ya vitendo vya ukatili na unyayasaji wa kijinsia yameripotiwa mkoani Katavi, ukilinganisha na makosa 240 yaliyoripotiwa kwa kipindi kama hicho mwaka 2021. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ali Makame, amesema makosa hayo yameripotiwa ndani ya miezi tisa kuanzia Januari hadi Septemba 2022.

“Kuna ongezeko la makosa 30 ya ukatili na unyayasaji wa kijinsia, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 12.5,” alisema. Amesema sababu ya matukio kuongezeka ni kupungua kwa utoaji elimu juu ya madhara ya ukatili na unyayasaji wa kijinsia kwa jamii.

Ili kudhibiti matukio hayo, ACP Makame amesema Jeshi la Polisi mkoani humo, limeweka mikakati ya kuongeza kasi ya kutoa elimu, ambayo inaendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari na kupitia njia mbalimbali, ikiwemo mikutano ya hadhara.

Ametoa wito kwa asasi zote, viongozi wa dini na wa serikali na jamii kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, kwa kutoa elimu ya madhara ya vitendo hivyo, ili kutengeneza jamii yenye amani.

HABARI LEO
 
Back
Top Bottom