Katavi: Mbaroni kwa kukamatwa na meno ya tembo yenye thamani ya milioni 247

Katavi: Mbaroni kwa kukamatwa na meno ya tembo yenye thamani ya milioni 247

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Polisi Mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hiifadhi ya Taifa ya Katavi, wamewakamata watu wanne kwa tuhuma za kukutwa na vipande 13 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 247.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Katavi, Ali Hamad Makame, alisema hayo mkoani hapa mwishoni mwa wiki alipozungumza nа waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa hao katika maeneo mawili tofauti.

Akizungumzia tukio la kwanza, Kamanda Makame alieleza watuhumiwa watatu Alex Ruben (45), Masele Kasema (36) na Nkamba Ntemula (45), walikamatwa kwa tuhuma za kukutwa na vipande saba vya meno ya tembo.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa Mtaa wa Ikulu, Kata ya Kawajense, Manispaa va Mpanda, wakiwa wameyahifadhi meno hayo ndani ya nyumba kwa kuyauza. Makame alibainisha watuhumiwa walikamatwa kutokana na Jeshi la Polisi na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kupata taarifa za watu hao kujihusisha na masuala ya ujangili.

Kuhusu, tukio la pili, Kamanda Makame alisema walifanikiwa kumkamata Michael Kisiba kwa tuhuma za kukutwa na vipande 11 vya meno ya tembo ambavyo ni sawa na tembo sita. Alisema mtuhumiwa huvo alikamatwa na meno hayo eneo la Kata ya Usevya, kutokana na msako mkali uliofanywa wa kuwasaka wanaojihusisha ujangili.

Alieleza Kisiba alikamatwa na meno hayo aliyokuwa ameyahifadhi ndani ya mfuko wa sandarusi na kuyaficha katika kichaka. Kwa upande wake, Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Kamishna Msaidizi Maneno Peter, alisema idadi ya meno wanayodaiwa kukamatwa navyo watuhumiwa ni sawa na tembo saba wenye thamani ya sh. 247,590,000.

Peter aliwataka na vitendo vya wanaojihusisha ujangili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi na nje ya hifadhi kutambua maeneo hayo siyo salama kwao. Mhifadhi huyo aliwaonya watakaojihusisha na masuala ya ujangili watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, hivyo ni vema wakajihusisha na biashara halali ikiwemo kilimo.

Alisema kukamatwa kwa meno hayo ni juhudi wanazozifanya za kuzuia ujangili, kabla ya kutekelezwa.​
 
Back
Top Bottom