JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tatizo hilo limebainika wakati shirika lisilo la kiserikali la Marie Stopes lilipofika katika Kijiji cha Mapili, Kata ya Ilela Mkoani Katavi na kuzungumza na kundi la wazee wa kimila, viongozi wa dini, viongozi wa kijiji kwa njia ya mdahalo ambapo wamesema utandawazi ni moja ya saba.
Moja ya Mila iliyotajwa kuwa sababu ni ile ya Wasichana wakifikisha umri wa miaka 13 kuruhusiwa kuolewa, hivyo wale ambao hawajapata wenza wanaanza kishiriki ngono.
Imeelezwa ndoa za utotoni zimekuwa zikiendelea chini ya viongozi wa Kimila na kupewa baraka na baadhi ya viongozi bila tatizo lolote.
Wamesema vijana wengi wakike na wakiume hawawasikilizi wazazi wao kama ilivyokuwa zamani wakati wao wanakua mtoto wakike ilikuwa hawezi kushiriki tendo la ndoa pale anapozuiliwa.
"Kweli hili tatizo lipo kwenye kijiji chetu na ni kubwa na mtoto wakike akipata mimba sisi wazazi wakike tunatukanwa sana na baba zao tunaambiwa wewe ndio umesababisha umeshindwa kumlea mtoto katika misingi wakati mwingine hadi unapigwa wewe na mtoto wako.
"Hilo ni kwa wenyeji na wakazi wa eneo hili la Mapili lakini kuna wahamiaji wa kabila la wasukuma wawo wanakamila fulani ambako kanawaruhusu wao kushiriki ndoa za utotoni ambapo watu wazima wanadiriki kuoa watotot wadogo tena kwa makubaliano tu mazuri," amesema Katawa John.
Naye kiongozi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mapili Kefasi Lutandika amesema wao kama viongozi wa dini wanaelekezwa umri sahihi wa kufungisha ndoa ambao hata serikali inautambua na kama wapo wanaofanya hivyo nikinyume hata na maandiko ya Mungu.
Akitoa takwimu za mimba za utotoni Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Finner Soka amesema kwa mwaka wa fedha 2021/22 kuna mimba za utotoni 3,574 ndani ya halmashauri hiyo.
Soka amesema katika Kijiji cha Mapili pekee kilichopo Kata ya Ilela kuna mimba zaidi ya 400 na kata nzima ya Ilela inaonyesha kuna mimba zaidi ya 700 ambapo takwimu hizo amesema ni kwa wale waliojifungulia katika vituo vyao vya afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, Theresia Irafay amekana kuwepo kwa takwimu hizo huku akidai wanaendelea kupiga vita ukatili na mimba za utotoni.
"Mimi siwezi kukubaliana na hilo kwamba katika kijiji hiki wapo 400 hapana hizo data itabidi tuziangalie vizuri kwanza, lakini tumeimarisha kamati za vijiji, kata na wilaya kuhakikisha zinafanya majukumu yake ya kupiga vita ukatili na mimba za utotoni," alisema Irafay.
Hata hivyo, mshauri wa maswala ya kijinsia, vijana na makundi maalumu kutoka shirika lisilo la kiserikali la Marie Stopes Magdalena Thomas, amesema wamefanya mijadala hiyo mikoa mengine minne na Katavi ni mkoa ambao wameurudia mara ya pili kutokana na changamoto kubwa ya ndoa za utotoni.
Source: IPP