Katavi: Mume amuua mkewe, mwanaye kisa ugomvi wa gunia 60 za mpunga

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu wanne waliokiri kufanya mauaji katika matukio tofauti, akiwamo mmoja aliyemuua mke na mwanawe na kuitupa miili yao kwenye pori la Kalilankulukulu wilayani Tanganyika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Machi 15, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema kuwa Dutu Danga (30) ambaye ni mume wa marehemu alifanya mauaji hayo kwa kushirikiana na Yussuph Muge (32).

Amesema Machi 8, 2022 Polisi walipokea taarifa za kutoweka kwa mama na mtoto katika mazingira ya kutatanisha.

“Tulifanya upelelezi wa kina Machi 9, 2022 tuliwakamata watuhumiwa akiwamo mume aliyezaa na huyo marehemu, baada ya kuwahoji wote kwa pamoja walikiri kuua na waliwaongoza polisi kuonyesha walipofukia miili,”

“Baada ya kufukua yalipatikana mabaki ya miili ya marehemu na chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia kati ya wanandoa hao kugombania magunia 60 ya mpunga,” amesema

Kamanda Makame amesema kuwa wanandoa hao wakikorofishana walikuwa wanashtakiana kwa ofisa mtendaji wa kijiji hicho na kutozwa faini mara kwa mara hivyo mume aliona njia pekee ya kuondoa tatizo ni kumuua mkewe na mtoto wake.

Mwananchi
 
Sasa mtoto anakosa gani? Halafu najiuliza, hadi wanaenda kuonyesha baada ya mahojiano, huwa ni mahojiano ya aina gani hayo? Au ndio kama ya yule jamaa aliekuwa anapigwa na rungu kubwa kwenye makende?! Aiseee!!!Mi nitataja hata kabla hujanipiga aisee.., acheni tu.., aaagh
 
275619151_637207184176854_1068540942418854584_n.jpg
 
damu ya mtu haipotei bure na NGUMU.
wewe mwenyewe una funguka bila hata kupigwa.
labda uwe mzoefu na masuala ya mauaji ila Kama tukio lako la kwanza lazma utajichanganya tu unapohojiwa

Mapolice wa natumia mwongozo wa Vipigo na sio PGO
 
damu ya mtu haipotei bure na NGUMU.
wewe mwenyewe una funguka bila hata kupigwa.
labda uwe mzoefu na masuala ya mauaji ila Kama tukio lako la kwanza lazma utajichanganya tu unapohojiwa
Hiyo ni imani tu mkuu!!labda kama mtu amefanya kwa bahati mbaya tu, lakini kwa haya mauaji ya kupanga!!ukiona mtuhumiwa amekwenda kuonyesha mahali alipofukia mwili, jua hicho kipondo chake alichopata si cha kawaida!!
Ni sawa sawa na unapoona jambazi sugu amekwenda kuonyesha silaha!!jua alikuwa anaenda kufa, akaona isiwe tabu!!kuna mkoa nilikuwa naishi ni karibu na kituo cha polisi, sasa ikifika usiku kwenye ofisi ya upelelezi, kazi ya kuwahoji ikianza ni kilio tu.
 
Ukishaua na polisi ikakushuku,lazima utaongea tu.Wana mafunzo maalumu ya kukupiga ili uongee...
 
katavi mshavuna mpunga? sambazeni basi bei ipungue
 
Back
Top Bottom