LGE2024 Katavi: Mwenyekiti wa CHADEMA pamoja na timu yake wanadaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mbilinge zinaendelea za kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa. Huku tukiendelea kusikia mambo yanayotokea kwenye vituo vya kujiandikisha.

Leo huko Katavi yalitokea ni haya
==================
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Katavi, Rhoda Kunchela, pamoja na timu yake wanadaiwa kukamatwa na jeshi la polisi katika eneo la Inyonga, jimbo la Kavuu mkoani humo na kushikiliwa katika kituo cha polisi cha stendi ya zamani, Inyonga.

Rhoda na timu yake walikuwa wakihamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la mkazi kwa ajili ya kushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Soma Pia: Special Thread: Hali ya Vituo vya Kujiandikisha kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Picha na Vide
 
Unataka muhalifu asikamatwe akivaa gwanda?
 
Kwa mwendo huu !!

Upinzani 0 -3 CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…