Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Shule ya msingi Ilangu. Iliyopo katika kata ya Ilangu wilayani Tanganyika inakabiliwa na upungufu wa walimu pamoja na vyumba vya madarasa.
Siyajali Odasi ambae ni Makamu Mwenyekiti wa kijiji hicho amesema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya mia tisa (900) iliyopo kijijini kwake ina walimu sita (6) tu,Pamoja na vyumba tisa(9) vya madarasa.
Pamoja na hayo katika kata hiyo kumekuwa na shida kubwa ya Maji kutokana na ukosefu wa visima vya maji kwani vilivyopo ni vichache kulinganisha na idadi ya wakazi wa kijijini hapo na pia vipo mbalimbali na hivyo basi hulazimika kutumia maji ya mito ambayo sio Salama kwa afya maana huchangia maji hayo pamoja na mifugo na hata msimu wa kiangazi maji hayo ya Mito hukauka.
Wakazi wa vijiji katika kata hiyo kulazimika kusafiri umbali wa kilomita 30 kufuata kituo cha afya kilichopo katika makazi ya mishamo,kutokana Na kuwa zahanati Moja iliyopo katika kata hiyo haikidhi huduma muhimu za matibabu.
Pia wakazi wa vijiji hivyo wamekuwa wakikosa huduma muhimu za matangazo ya Radio kutokana na Kuwa Mawimbi ya Radio hayafiki huko.