Katavi: Viboko katika bwawa la Milala Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi waanza kuhamishwa

Katavi: Viboko katika bwawa la Milala Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi waanza kuhamishwa

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
693
Reaction score
889
Bodi ya mamlaka ya wanyamapori nchini TAWA imeanza kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufu kuhusu kuwaondoa viboko katika bwawa la Milala katika Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Wanyamapori TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko amesema agizo la Rais lazima litekelezwe haraka sana na kazi hi
yo imea

Hivi karibuni rais John Magufuli aliwapongeza viboko wa Mkoa wa Katavi waliohamia kwenye bwawa lililochimbwa katika mji wa Mpanda baada ya mto waliokuwa wakikaa kukauka.

Rais Magufuli alitoa pongezi hizo siku ya Ijumaa Oktoba 11, 2019 na kuzitaka mamlaka mkoani humo kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kuchimba mabwawa ndani ya Hifadhi ya Katavi kwa ajili ya wanyama hao.

Rais alitoa kauli hiyo kufuatia maagizo aliyoyatoa kwa Tanapa kujaza maji katika mto waliopo viboko hao na alisema tayari maji yameshaanza kujazwa.

“Hapa mjini kuna bwawa lilichimbwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu, kwa hiyo wale viboko wamekosa maji wamehamia kwenye bwawa lenu la mjini. Wale viboko hawajakosea, kwanza nawapongeza sana, wana akili sana. Wana akili kweli,” alisema Rais Magufuli.

“Nasikia mlikuwa mnataka kutoa maagizo wale viboko wauliwe hapana. Wale viboko wamekuja mjini, kwanza mmewazibia maji kule lakini pili Tanapa hawajawachimbia mabwawa.”


Aliongeza, “Kwa sababu Tanapa wangekuwa na akili kama viboko walivyo na akili wangewachimbia mabwawa mle ndani wale viboko wasingeondoka kwa sababu kule kuna majani wangeyapata kwa ajili ya ku-protect maisha yao. Lakini mlivyo mkachiba bwawa mjini kwa hiyo wakawafuata huko.”

Rais John Magufuli aliagiza Mamlaka ya Hifadhi za Wanyamapori nchini (Tawa) kuchimba bwawa na kujaza maji kwa ajili ya viboko wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Pia aliitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kufungua mabucha ya nyamapori kwa ajili ya watu wa Mpanda. Amesema maisha bora kwa Watanzania ni pamoja na kunufaika na rasilimali zao.
nza rasmi.
 
Hii nchi imeoza nyama hadi mifupa mae mae, yaani hata vidogo kama hivi vinasubiri hadi rais aingilie kati? Sasa ni ipi kazi ya wasomi na wataalamu?
Inasikitisha sana kwa kweli....
 
Nimeipenda hii paragraph
"Hivi karibuni rais John Magufuli aliwapongeza viboko wa Mkoa wa Katavi waliohamia kwenye bwawa lililochimbwa katika mji wa Mpanda baada ya mto waliokuwa wakikaa kukauka."
 
Hapa mjini kuna bwawa lilichimbwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu, kwa hiyo wale viboko wamekosa maji wamehamia kwenye bwawa lenu la mjini. Wale viboko hawajakosea, kwanza nawapongeza sana, wana akili sana. Wana akili kweli,” alisema Rais Magufuli.


Imekaa vizuri
 
Nimeipenda hii paragraph
"Hivi karibuni rais John Magufuli aliwapongeza viboko wa Mkoa wa Katavi waliohamia kwenye bwawa lililochimbwa katika mji wa Mpanda baada ya mto waliokuwa wakikaa kukauka."



Imedhihirisha kuwa wanyama pori wanafikiria ahead of us, wasomi wazima walikaa tu bila kufikiri lolote
 
Kweli mpaka viboko wanawashinda akili ,yaani mnajaza maji kwenye mto kwa kutumia magari,hongera zake huyo aliyepata hiyo tenda ya kusomba maji
 
1574486679616.png


KATIKA kutekeleza agizo la Rais John Magufuli, Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limechimba mabwawa matatu ambayo yatajazwa maji ili viboko wanaoishi katika bwawa la Milala lililopo jirani na makazi ya watu waweze kuhamishiwa na kuishi humo.

Mabwawa hayo ambayo kila moja limegharimu zaidi ya Sh milioni 104 yamechimbwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi iliyopo wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi jirani na mkondo wa Mto Katuma. Bwawa la Milala ambalo liko jirani na makazi ya binadamu ni chanzo kikubwa na muhimu cha maji kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), Hamisi Semfuko, wakati akifunga mafunzo ya Jeshi Usu la kulinda wanyamapori kwa wahitimu kwenye kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi juzi. Baadhi ya wahitimu hao wanatoka katika taasisi za uhifadhi zilizoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo 148 wanatoka Tawa, 374 Tanapa, saba Mamlaka ya Eneo la Hifadhi la Ngorongoro ((NCAA), wanne Chuo cha Wanyamapori Mweka na mmoja kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Idadi hiyo wahitimu pia inajumuisha naibu kamishna wa uhifadhi mmoja, makamishna wasaidizi waandamizi sita kutoka NCAA, maofisa wa kati watano na askari wahifadhi 523 wakiwamo wahifadhi na wasio wahifadhi. Oktoba mwaka huu, Rais Magufuli alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Katavi, aliiagiza Tanapa kuwapelekea maji viboko walioko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi kutokana na kukaukiwa hivyo kuishi kwa mateso na kukataza wasiuawe.

Aidha, Rais Magufuli aliiagiza Tanapa kuchimba bwawa ndani ya hifadhi hiyo na kujaza maji kwa ajili ya viboko hao. Alitoa maagizo hayo Oktoba, mwaka huu wilayani Mpanda baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa kuunganisha mkoa wa Katavi na umeme wa gridi ya taifa. Agosti, mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla, alisema serikali ina mpango wa kuuza asilimia 10 ya viboko na mamba wanaoishi katika mabwawa jirani na makazi ya binadamu.

Alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto zilizopo kati ya binadamu na wanyamapori hao wanaoishi katika mabwawa yaliyopo jirani na makazi ya watu. Aliitaja miji ya Mpanda (Katavi), Babati (Manyara) na Mafia (Pwani) kama maeneo ambayo baadhi ya wakazi wake ama wamepoteza maisha au kusababishiwa ulemavu wa maisha baada ya kushambuliwa na wanyama hao.
 
Ina maana kuna emergency procurement ilifanyika...hasara za kufanya emergency procurement ni kubwa sana! Sawa ngoja twende
 
Back
Top Bottom