Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Tukio hilo la kufyekewa mahindi limetokea hivi karibuni kutokana na kile kinachotajwa ni uvamizi katika maeneo ya misitu ambayo inazuio la shughuli za binadamu.
Moja wa wahanga wa kufyekewa mahidi, Georgina Joseph mkazi wa kata ya Kasekese amedai kuwa suala la kufyekewa mahidi yao ni uonevu ambao haukubaliki kwa masirahi ya kupambana na umasikini.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amesema kuwa wilaya hiyo imetenga maeneo ya kilimo na uhifadhi hivyo idara ya maliasili imnekuwa imara kusimamia rasilimali ya misitu kwa kutumia sheria ili kuhifadhi misitu.
Pia soma ~ RC Mrindoko ufyekaji wa Mahindi kwa Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika si maelekezo ya Serikali